Zab 67
SUV

Zab 67

67
Mataifa Yaitwa Kumsifu Mungu
Kwa mwimbishaji: kwa ala za nyuzi za muziki. Zaburi. Wimbo.
1 # Zab 4:6; 31:16; 119:135; Hes 6:25,26; 2 Kor 4:6 Mungu na atufadhili na kutubariki,
Na kutuangazia uso wake.
2 # Mdo 13:10; Tit 2:11; Lk 2:30-32 Njia yake ijulike duniani,
Wokovu wake katikati ya mataifa yote.
3 # Isa 24:15,16 Watu na wakushukuru, Ee Mungu,
Watu wote na wakushukuru.
4 # Zab 96:10 Mataifa na washangilie,
Naam, waimbe kwa furaha,
Maana kwa haki utawahukumu watu,
Na kuwaongoza mataifa walioko duniani.
5Watu na wakushukuru, Ee Mungu,
Watu wote na wakushukuru.
6 # Law 26:4; Isa 1:19; Zab 85:9-12 Nchi imetoa mazao yake
MUNGU, Mungu wetu, ametubariki.
7 # Zab 22:27 Mungu atatubariki sisi;
Miisho yote ya dunia itamcha Yeye.

Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.

Learn More About Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia