22
1 #
Kum 12:5; 2 Sam 24:18; 1 Nya 21:18-28; 2 Nya 3:1 Ndipo Daudi akasema, Hii ndiyo nyumba ya BWANA Mungu, na hii ndiyo madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya Israeli.
Daudi ajitayarisha kujenga hekalu
2 #
1 Fal 9:21
Basi Daudi akaamuru wakusanyike wageni waliokuwa katika nchi ya Israeli; akaweka waashi wachonge mawe ili kujenga nyumba ya Mungu. 3#1 Fal 7:47 Daudi akaweka akiba tele ya chuma kwa misumari ya tarabe za malango, na kwa mafungo; na ya shaba akiba tele isiyoweza kupimika; 4#1 Fal 5:6 na mierezi isiyo na idadi; kwa kuwa Wasidoni na watu wa Tiro walimletea Daudi mierezi tele. 5#1 Fal 3:7; 1 Nya 29:1 Daudi akasema, Sulemani mwanangu angali ni mchanga bado, na hana uzoefu, nayo nyumba atakayojengewa BWANA haina budi kuwa nzuri mno, yenye sifa na yenye fahari katika nchi zote; kwa hiyo mimi nitaiwekea akiba. Basi Daudi akaweka akiba tele kabla hajafa.
Maagizo ya Daudi kwa Sulemani na viongozi
6Ndipo akamwita Sulemani mwanawe, akamwagiza amjengee BWANA, Mungu wa Israeli, nyumba. 7#2 Sam 7:2; 1 Fal 8:17; 1 Nya 17:1; 28:2; Mdo 7:46; Kum 12:5 Daudi akamwambia Sulemani mwanawe, Kwangu mimi nia yangu ilikuwa kujenga nyumba kwa ajili ya jina la BWANA, Mungu wangu. 8#1 Fal 5:3; 1 Nya 28:3 Lakini neno la BWANA likanijia, kusema, Wewe umemwaga damu nyingi, na vita vikubwa umevifanya; wewe hutajenga nyumba kwa ajili ya jina langu, kwa sababu umemwaga damu nyingi juu ya nchi machoni pangu; 9#1 Nya 28:5; 1 Fal 4:25; 5:4 tazama, utapata mwana, atakayekuwa mtu wa amani; nami nitampa amani mbele ya adui zake pande zote; kwani jina lake litakuwa Sulemani,#22:9 Sulemani: maana yake ni Mtulivu. nami nitawapa Israeli amani na utulivu siku zake; 10#2 Sam 7:13; 1 Fal 5:5; 1 Nya 17:12; 28:6; Zab 89:26,27; Ebr 1:5 huyo ndiye atakayejenga nyumba kwa ajili ya jina langu; naye atakuwa mwanangu, nami nitakuwa babaye; nami nitakiimarisha milele kiti cha ufalme wake juu ya Israeli. 11#Rum 8:31 Sasa mwanangu, BWANA na awe pamoja nawe; ukafanikiwe, na kuijenga nyumba ya BWANA, Mungu wako, kama alivyonena kuhusu habari zako. 12#Kum 4:6; 1 Fal 3:9; Zab 72:1 BWANA na akupe busara na akili, akakuagizie juu ya Israeli; ili uishike Torati ya BWANA, Mungu wako. 13#Yos 1:7; 1 Fal 6:12,13; 9:4,5; 1 Nya 11:9,15; 28:7; Isa 3:10; Kum 31:7; 1 Nya 28:20 Ndipo utakapofanikiwa, ukiangalia kuzitenda amri, na hukumu, BWANA alizomwagizia Musa juu ya Israeli; uwe hodari, na wa moyo mkuu; usiogope wala usifadhaike. 14Basi sasa, tazama, katika shida yangu, nimeiwekea akiba nyumba ya BWANA, talanta laki moja za dhahabu, na talanta milioni moja za fedha; na shaba na chuma isiyo na uzani; kwa vile zilivyo tele; miti tena na mawe nimeweka akiba, nawe utaweza kuongeza. 15Tena kwako kuna mafundi wengi, wenye kuchonga na kufanya kazi ya mawe na miti, na kila aliye stadi kwa kazi yoyote; 16ya dhahabu, ya fedha, na ya shaba, na ya chuma, hapana hesabu; basi inuka ushike kazi, naye BWANA na awe pamoja nawe. 17Tena Daudi akawaamuru viongozi wote wa Israeli, kwamba wamsaidie Sulemani mwanawe, akisema, 18#Kum 12:10; Yos 22:4; 2 Sam 7:1; 1 Nya 23:25 Je! Si BWANA, Mungu wenu, aliye pamoja nanyi? Na kuwapa amani pande zote? Kwa kuwa wenyeji wa nchi amewatia mkononi mwangu; nayo nchi imetiishwa mbele za BWANA, na mbele ya watu wake. 19#2 Nya 20:3; 1 Fal 8:6; 2 Nya 5:7; 6:11 Basi sasa jitieni moyo na nia kumtafuta BWANA, Mungu wenu; inukeni basi, mkamjengee BWANA Mungu mahali patakatifu, ili kulileta sanduku la Agano la BWANA, na vyombo vitakatifu vya Mungu, ndani ya nyumba itakayojengwa kwa ajili ya jina la BWANA.