3
Hitaji la maombi
1 #
Kol 4:3; 1 The 5:25 Hatimaye, ndugu, tuombeeni, neno la Bwana liendelee, na kutukuzwa kote kama ilivyo kwenu; 2na tukaokolewe kutoka kwa watu wasio haki, na waovu, maana si wote walio na imani. 3#1 The 5:24 Lakini Bwana ni mwaminifu, atakayewafanya imara na kuwalinda kutoka kwa yule mwovu. 4#1 The 4:10; Gal 5:10; 2 Kor 7:16 Nasi tumemtumaini Bwana kwa mambo yenu, kwamba mnayafanya tulivyowaagiza na kwamba mtaendelea kuyafanya. 5Bwana awaongoze mioyo yenu mkapate pendo la Mungu, na subira ya Kristo.
Onyo juu ya kutofanya kazi
6 #
Mt 18:17; Rum 16:17; 1 The 5:14; 4:1 Ndugu, tunawaagiza katika jina la Bwana Yesu Kristo, jitengeni nafsi zenu kutoka kwa kila ndugu aendaye bila utaratibu, wala si kwa kufuata mapokeo mliyoyapokea kwetu. 7#1 The 2:1; 1:6 Mnajua wenyewe jinsi iwapasavyo kutufuata; kwa sababu hatukuenda bila utaratibu kwenu; 8#1 Kor 4:12; Flp 3:17; 1 The 2:9 wala hatukula chakula kwa mtu yeyote bure; bali kwa taabu na masumbufu, usiku na mchana tulifanya kazi, ili tusimlemee mtu wa kwenu awaye yote. 9#Mt 10:10; 1 Kor 4:16; 1 The 1:6,7 Si kwamba hatuna haki hiyo, ila kwa makusudi ya kuwapa mfano wa kuiga, mtufuate. 10#Mwa 3:19; 1 The 3:4; 4:11 Kwa kuwa hata wakati ule tulipokuwapo kwenu tuliwaagiza neno hili, kwamba ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi, asile chakula. 11#1 The 5:14 Maana tunasikia kwamba wako watu kwenu waendao bila utaratibu, hawana shughuli zao wenyewe, lakini wanajishughulisha na mambo ya wengine. 12#1 The 4:11 Basi tunawaagiza hao, na kuwaonya katika Bwana Yesu Kristo, wafanye kazi kwa utulivu na kula chakula chao wenyewe. 13#Gal 6:9 Lakini ninyi, ndugu, msikate tamaa katika kutenda mema. 14#1 Kor 5:9,11 Na ikiwa mtu awaye yote halishiki neno letu la barua hii, jihadharini na mtu huyo, wala msizungumze naye, apate kutahayari; 15#1 The 5:13,14 lakini msimhesabu kuwa adui, bali mwonyeni kama ndugu.
Salamu za mwisho na baraka
16 #
1 The 5:23
Sasa, Bwana wa amani mwenyewe na awape amani daima kwa njia zote. Bwana awe pamoja nanyi nyote.
17 #
1 Kor 16:21
Salamu zangu mimi Paulo, kwa mkono wangu mwenyewe. Hii ndiyo alama katika kila barua yangu, ndio mwandiko wangu. 18Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi nyote.