Wagalatia 1
SRUV

Wagalatia 1

1
Salamu
1 # Gal 1:11,12 Paulo, mtume, (si mtume wa wanadamu, wala kutumwa na mwanadamu, bali na Yesu Kristo, na Mungu Baba aliyemfufua kutoka kwa wafu), 2na ndugu wote walio pamoja nami, kwa makanisa ya Galatia; 3#Rum 1:7 Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba, na kwa Bwana wetu Yesu Kristo; 4#Gal 2:20; 1 Tim 2:6; Tit 3:14; 1 Yoh 5:19 ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili ya dhambi zetu, ili atuokoe na dunia hii mbovu iliyopo sasa, kama alivyopenda Mungu, Baba yetu. 5Utukufu una yeye milele na milele, Amina.
Hakuna Injili nyingine
6Nashangaa kwa kuwa mnamwacha upesi hivi yeye aliyewaita katika neema ya Kristo, na kugeukia Injili ya namna nyingine. 7#Mdo 15:1,24 Wala si nyingine; lakini wapo watu wawataabishao na kutaka kuigeuza Injili ya Kristo. 8#1 Kor 16:22 Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiria ninyi Injili yoyote isipokuwa hiyo tuliyowahubiria, na alaaniwe. 9Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiria ninyi Injili yoyote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe.
10 # 1 The 2:4 Maana, sasa je! Ni wanadamu ninaowashawishi, au Mungu? Au nataka kuwapendeza wanadamu? Kama ningekuwa hata sasa nawapendeza wanadamu, singekuwa mtumwa wa Kristo.
Paulo athibitisha utume wake
11Kwa maana, ndugu zangu, Injili hiyo niliyowahubiria, nawajulisha ya kuwa siyo ya namna ya kibinadamu. 12Kwa kuwa sikuipokea kwa mwanadamu wala sikufundishwa na mwanadamu, bali kwa ufunuo wa Yesu Kristo. 13#Mdo 8:3; 22:4-5; 26:9-11 Maana mmesikia habari za mwenendo wangu zamani katika dini ya Kiyahudi, kwamba nililitesa kanisa la Mungu kupita kiasi, nikaliharibu. 14#Mdo 22:3 Nami niliendelea katika dini ya Kiyahudi kuliko wengi walio hirimu zangu katika kabila yangu, nikajitahidi sana katika kuyashika mapokeo ya baba zangu. 15#Mdo 9:3-6; 22:6-10; 26:13-18 Lakini Mungu, aliyenitenga tangu tumboni mwa mama yangu, akaniita kwa neema yake, #Rum 1:1; Yer 1:5; Isa 49:1 16#Gal 2:7; Mt 16:17 alipoona vema kumdhihirisha Mwanawe ndani yangu, ili niwahubirie Mataifa habari zake; mara sikufanya shauri na watu wenye mwili na damu; 17wala sikupanda kwenda Yerusalemu kwa hao waliokuwa mitume kabla yangu; bali nilikwenda zangu Arabuni, kisha nikarudi tena Dameski.
18 # Mdo 9:26-30 Kisha, baada ya miaka mitatu, nilipanda kwenda Yerusalemu ili nionane na Kefa, nikakaa kwake siku kumi na tano. 19#Mt 13:55 Lakini sikumwona mtume mwingine, ila Yakobo, ndugu yake Bwana. 20Na hayo ninayowaandikia, angalieni, mbele za Mungu, sisemi uongo. 21#Mdo 9:30 Baadaye nilikwenda pande za Shamu na Kilikia. 22Lakini sikujulikana uso wangu na makanisa ya Yudea yaliyokuwa katika Kristo; 23ila wamesikia tu ya kwamba huyo aliyetutesa hapo kwanza, sasa anaihubiri imani ile aliyoiharibu zamani. 24Wakamtukuza Mungu kwa ajili yangu.

Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

Learn More About Swahili Revised Union Version