62
Uthibitisho wa wokovu wa Sayuni
1Kwa ajili ya Sayuni sitanyamaza, na kwa ajili ya Yerusalemu sitatulia, hata haki yake itakapotokea kama mwangaza, na wokovu wake kama taa iwakayo. 2#Isa 65:15; Ufu 3:12 Na mataifa wataiona haki yako, na wafalme wote watauona utukufu wako; nawe utaitwa jina jipya, litakalotajwa na kinywa cha BWANA. 3#Zek 9:16 Nawe utakuwa taji la uzuri katika mkono wa BWANA, na kilemba cha kifalme mkononi mwa Mungu wako. 4#Hos 1:10; 1 Pet 2:10 Hutaitwa tena Aliyeachwa, wala nchi yako haitaitwa tena, Ukiwa; bali utaitwa Hefziba;#62:4 Hefziba: maana yake ni ‘namfurahia.’ na nchi yako Beula;#62:4 Beula: maana yake ni ‘ameolewa.’ kwa kuwa BWANA anakufurahia, na nchi yako itaolewa. 5Maana kama vile kijana amwoavyo mwanamwali, ndivyo wana wako watakavyokuoa wewe; na kama vile bwana arusi amfurahiavyo bibi arusi, ndivyo Mungu wako atakavyokufurahia wewe.
6 #
Wim 3:3; Isa 52:8; Eze 3:17; Ebr 13:17 Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, Ee Yerusalemu; hawatanyamaza mchana wala usiku; ninyi wenye kumkumbusha BWANA, msiwe na kimya; 7#Isa 61:11; Sef 3:20 wala msimwache akae kimya, mpaka atakapouimarisha Yerusalemu, na kuufanya usifike kote duniani. 8#Kum 28:31; Yer 5:17 BWANA ameapa kwa mkono wake wa kulia, na kwa mkono wa nguvu zake, Hakika sitawapa adui zako nafaka yako tena kuwa chakula chao; wala wageni hawatakunywa divai yako, uliyoifanyia kazi. 9#Kum 12:12 Lakini walioivuna, ndio watakaoila, na kumhimidi BWANA; na walioichuma, ndio watakaoinywa, ndani ya nyua za patakatifu pangu.
10Piteni, piteni, katika malango;
Itengenezeni njia ya watu;
Tutieni, tutieni barabara; toeni mawe yake;
Twekeni bendera kwa ajili ya makabila ya watu.
11 #
Zek 9:9; Mt 21:5; Yn 12:15; Isa 40:10; 49:4; Ufu 22:12 Tazama, BWANA ametangaza habari mpaka mwisho wa dunia,
Mwambieni binti Sayuni,
Tazama, wokovu wako unakuja;
Tazama, thawabu yake iko pamoja naye,
Na malipo yake yako mbele zake.
12Nao watawaita, Watu watakatifu,
Waliokombolewa na BWANA;
Nawe utaitwa, Aliyetafutwa,
Mji usioachwa.