Zaburi 124
SRUV

Zaburi 124

124
Shukrani kwa ukombozi wa Israeli
Wimbo wa kupanda mlima.
1 # Mwa 15:1; Hes 14:9; Yos 1:5; Ebr 13:5; Rum 8:31 Kama si BWANA aliyekuwa pamoja nasi,
Israeli na aseme sasa,
2Kama si BWANA aliyekuwa pamoja nasi,
Wanadamu walipotushambulia.
3 # Zab 35:25; Mit 1:12; Yer 51:34 Papo hapo wangalitumeza hai,
Hasira yao ilipowaka juu yetu.
4Papo hapo maji yangalitugharikisha,
Mto ungalipita juu ya roho zetu;
5Papo hapo maji yafurikayo
Yangalipita juu yetu.
6Na ahimidiwe BWANA;
Asiyetutoa kuwa mawindo kwa meno yao.
7Nafsi yetu imeokoka kama ndege
Katika mtego wa wawindaji,
Mtego umevunjika, nasi tumeokoka.
8 # Kut 18:4; Zab 12:2; Mit 18:10; Isa 50:10; Ebr 13:6 Msaada wetu u katika jina la BWANA,
Aliyeziumba mbingu na nchi.

Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

Learn More About Swahili Revised Union Version