Zaburi 128
SRUV

Zaburi 128

128
Nyumba ya mwumini yenye furaha
Wimbo wa kupanda mlima.
1Heri kila mtu amchaye BWANA,
Aendaye katika njia yake.
2 # Isa 3:10 Taabu ya mikono yako hakika utaila;
Utakuwa heri, na kwako kwema.
3Mkeo atakuwa kama mzabibu uzaao,
Katika nyumba yako.
Wanao watakuwa kama miche ya mizeituni
Wakiizunguka meza yako.
4Tazama, atabarikiwa hivyo, yule amchaye BWANA.
5 # Zab 134:3 BWANA akubariki toka Sayuni;
Uone uheri wa Yerusalemu siku zote za maisha yako;
6 # Mwa 50:23 Naam, ukawaone wana wa wanao.
Amani ikae na Israeli.

Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

Learn More About Swahili Revised Union Version