131
Kumtumainia Mungu kwa utulivu
Wimbo wa kupanda mlima.
1 #
Rum 12:16
BWANA, moyo wangu hauna kiburi,
Wala macho yangu hayainuki.
Wala sijishughulishi na mambo makuu,
Wala mambo yanayozidi nguvu zangu.
2 #
Mt 18:3
Hakika nimeituliza nafsi yangu,
Na kuinyamazisha.
Kama mtoto aliyeachishwa kunyonya
Kifuani mwa mama yake;
Roho yangu ni kama mtoto,
Aliyeachishwa kunyonya.
3Ee Israeli, umtarajie BWANA,
Tangu leo na hata milele.