Zaburi 142
SRUV

Zaburi 142

142
Sala ya ukombozi kutoka kwa watesi
Utenzi wa Daudi. Alipokuwa pangoni. Ombi.
1 # 1 Sam 22:1; 24:3 Kwa sauti yangu nitamlilia BWANA,
Kwa sauti yangu nitamwomba BWANA dua.
2Nitafunua mbele zake malalamiko yangu,
Shida yangu nitaitangaza mbele zake.
3Roho yangu inapozimia unayajua mapito yangu;
Katika njia niendayo wamenifichia mtego.
4Utazame mkono wangu wa kulia ukaone,
Kwa maana sina mtu anijuaye.
Makimbilio yamenipotea,
Hakuna wa kunitunza roho.
5 # Omb 3:24 BWANA, nimekuita nikasema, Ndiwe kimbilio langu,
Fungu langu katika nchi ya walio hai.
6 # Zab 116:6; 7:1 Ukisikilize kilio changu,
Kwa maana nimedhilika sana.
Uniponye kutoka kwa wanaonifuatia,
Kwa maana wao ni hodari kuliko mimi.
7 # Zab 34:2; 119:17 Uitoe nafsi yangu kifungoni.
Nipate kulishukuru jina lako.
Wenye haki watanizunguka,
Kwa kuwa Wewe unanikirimu.

Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

Learn More About Swahili Revised Union Version