Zaburi 150
SRUV

Zaburi 150

150
Sifa kwa ukuu Mwingi wa Mungu
1Haleluya.
Msifuni Mungu katika patakatifu pake;
Msifuni katika anga la uweza wake.
2Msifuni kwa matendo yake makuu;
Msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake.
3Msifuni kwa mvumo wa baragumu;
Msifuni kwa kinanda na kinubi;
4 # Kut 15:20; Isa 38:20 Msifuni kwa matari na kucheza;
Msifuni kwa zeze na filimbi;
5Msifuni kwa matoazi yaliayo;
Msifuni kwa matoazi yavumayo sana.
6 # Ufu 5:13 Kila mwenye pumzi na amsifu BWANA.
Haleluya.

Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

Learn More About Swahili Revised Union Version