Zaburi 57
SRUV

Zaburi 57

57
Sifa na hakikisho katika mateso
Kwa mwimbishaji: kwa mtindo wa Usiharibu. Utenzi wa Daudi alipomponyoka Sauli na kujificha pangoni.
1 # Isa 26:20 Unirehemu, Ee Mungu, unirehemu mimi,
Maana nafsi yangu imekukimbilia Wewe.
Nitaukimbilia uvuli wa mbawa zako,
Hadi misiba hii itakapopita.
2 # Zab 138:8 Nitamwita MUNGU Aliye Juu,
Mungu anitimiziaye mambo yangu.
3 # Zab 144:5; 40:11 Atanitumia msaada toka mbinguni na kuniokoa,
Atawaaibisha wale wanaotaka kunishambulia.
Mungu atazituma
Fadhili zake na kweli yake.
4 # Mit 30:14; Zab 64:3 Nafsi yangu i kati ya simba,
Nitastarehe kati yao waliowaka moto.
Wanadamu meno yao ni mikuki na mishale,
Na ndimi zao ni upanga mkali.
5 # Zab 108:5 Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu,
Na juu ya nchi yote uwe utukufu wako.
6 # Zab 9:15 Wameweka wavu ili kuninasa miguu;
Nimevunjika moyo;
Wamechimba shimo njiani mwangu;
Lakini wao wenyewe wametumbukia humo!
7 # Zab 108:1 Ee Mungu, moyo wangu ni thabiti,
Moyo wangu ni thabiti.
Nitaimba, nitaimba kwa sauti nzuri,
8 # Amu 5:12 Amka, ee moyo wangu.
Amka, kinanda na kinubi,
Nitaamka alfajiri.
9Ee Bwana, nitakushukuru kati ya watu,
Nitakuimbia sifa kati ya mataifa.
10 # Zab 108:4 Maana fadhili zako ni kubwa hata mbinguni,
Na uaminifu wako hata mawinguni.
11Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu,
Na juu ya nchi yote uwe utukufu wako.

Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

Learn More About Swahili Revised Union Version