Zaburi 82
SRUV

Zaburi 82

82
Ombi la kupata haki
Zaburi ya Asafu.
1 # Mhu 5:8; Kut 21:6 Mungu asimama katika kusanyiko la Mungu;
Katikati ya miungu anahukumu.
2 # Kum 1:17; Zab 58:1,2 Hadi lini mtahukumu kwa dhuluma,
Na kuzikubali nyuso za wabaya?
3Mfanyieni hukumu maskini na yatima;
Mtendeeni haki aliyeonewa, na fukara;
4Mwokoeni maskini na mhitaji;
Mwopoeni mikononi mwa wadhalimu.
5 # Zab 11:3 Hawajui wala hawafahamu, hutembea gizani;
Misingi yote ya nchi imetikisika.
6 # Ayu 21:32; Eze 31:14; Yn 10:34 Mimi nimesema, Ndinyi miungu,
Na wana wa Aliye Juu, enyi nyote.
7Lakini mtakufa kama wanadamu,
Mtaanguka kama mmoja wa wakuu.
8 # Zab 2:8; Ufu 11:15 Ee Mungu, usimame, uihukumu nchi,
Maana mataifa yote ni yako.

Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

Learn More About Swahili Revised Union Version