Zaburi 93
SRUV

Zaburi 93

93
Ukuu wa enzi ya Mungu
1 # Isa 52:7; Ufu 19:6; Ayu 40:10; Zab 104:1; Isa 59:17 BWANA ametamalaki, amejivika adhama,
BWANA amejivika, ukuu na nguvu, kama mavazi ya kifalme.
Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike;
2 # Mit 8:22 Kiti chako kimekuwa thabiti tokea zamani;
Wewe ndiwe uliye tangu milele.
3Ee BWANA, mito imepaza,
Mito imepaza sauti zake,
Mito imepaza uvumi wake.
4 # Zab 29:10 Kupita sauti ya maji mengi, maji makuu,
Kupita mawimbi ya bahari yaumkayo,
BWANA Aliye Juu ndiye mwenye ukuu.
5Shuhuda zako ni amini sana;
Utakatifu ndio uifaao nyumba yako,
Ee BWANA, milele na milele.

Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

Learn More About Swahili Revised Union Version