1 Yohane 4
BHNTLK

1 Yohane 4

4
Roho wa ukweli na wa uongo#4:1-6 Aya hizi zawapa waumini kipimo cha kubainisha kati ya mambo ya Mungu na mambo ya ulimwengu; kati ya watu wanaoongozwa na Roho wa Mungu na wasioongozwa na Roho huyo.
1Wapenzi wangu, msimsadiki kila mtu asemaye kwamba ana Roho wa Mungu, bali chunguzeni kwa makini kama huyo mtu anaongozwa na Roho wa Mungu au la, maana manabii wengi wa uongo wamezuka ulimwenguni. 2Hii ndiyo njia ya kujua kama mtu anaongozwa na Roho wa Mungu: Kila anayekiri kwamba Kristo alikuja, akawa binadamu,#4:2 Anayekiri kwamba Kristo alikuja, akawa binadamu: Yoh 1:14. Kukiri hapa ni kukubali kwa moyo kama jambo la kweli na kuzingatia matokeo yake katika maisha ya mtu binafsi. Mwandishi hapa anawaweka kando wale ambao hawakukubali kwamba Mwana wa Mungu alikuwa na mwili kama sisi. mtu huyo anaye Roho wa Mungu. 3Lakini mtu yeyote asiyemkiri Kristo hivyo, hana huyo Roho atokaye kwa Mungu. Mtu huyo ana roho ambaye ni wa mpinzani wa Kristo;#4:2-3 Mpinzani wa Kristo: Taz 1Yoh 2:18 maelezo. nanyi mlikwisha sikia kwamba anakuja, na sasa tayari amekwisha wasili ulimwenguni!
4Lakini nyinyi, watoto, ni wake Mungu na mmekwisha washinda hao manabii wa uongo; maana Roho aliye ndani yenu#4:4 Roho aliye ndani yenu: Neno kwa neno: Yule aliye ndani yenu. “Yule” ni Roho wa Mungu kama tafsiri hii au Mungu mwenyewe; taz Yoh 14:16. ana nguvu kuliko roho aliye ndani ya hao walio wa ulimwengu.#4:4 Roho aliye ndani ya hao walio wa ulimwengu: Huyu roho ni kinyume cha Roho wa Mungu; ni Ibilisi au Shetani aliye “mtawala wa ulimwengu”. (1Yoh 3:10; Yoh 14:30). 5Wao#4:5 Wao: Yaani wale waliojitenga na jumuiya hiyo ya waumini (angalia 1Yoh 2:18 maelezo). husema mambo ya ulimwengu, nao ulimwengu huwasikiliza kwani wao ni wa ulimwengu. 6Lakini sisi ni wake Mungu. Mtu anayemjua Mungu hutusikiliza,#4:6 Hutusikiliza: Yoh 8:47; 18:37. mtu asiye wa Mungu hatusikilizi. Basi, kwa njia hiyo tunaweza kutambua tofauti kati ya Roho wa ukweli#4:6 Roho wa ukweli: Rejea Yoh 14:16-17. na roho wa uongo.
Mungu ni upendo
7Wapenzi wangu, tupendane, maana upendo hutoka kwa Mungu.#4:7 Upendo hutoka kwa Mungu: 1Yoh 3:23. Kila mtu aliye na upendo ni mtoto wa Mungu, na anamjua Mungu.#4:7—5:3 Sehemu hii yote inahusu upendo. Kwanza upendo wa Mungu kwa ulimwengu, (4:7-10) upendo ambao unakuwa msingi na sababu ya waumini kupendana (4:11—5:3). 8Mtu asiye na upendo hamjui Mungu, maana Mungu ni upendo.#4:8 Mungu ni upendo: Yaani kila anachotenda au kufanya hukitenda au hukifanya kwa upendo. 9Na Mungu#4:9 Na Mungu …: Au: Hivi ndivyo Mungu alivyoonesha upendo wake kwetu; alimtuma Mwanawe … alionesha upendo wake kwetu kwa kumtuma Mwanae wa pekee ulimwenguni, ili tuwe na uhai kwa njia yake. 10Hivi ndivyo upendo ulivyo: si kwamba sisi tulikuwa tumempenda Mungu kwanza, bali kwamba yeye alitupenda hata akamtuma Mwanae#4:10 Akamtuma Mwanae: Ling Rom 5:8. awe sadaka ya kutuondolea dhambi zetu.
11Wapenzi wangu, ikiwa Mungu alitupenda hivyo, basi, nasi tunapaswa kupendana. 12Hakuna mtu aliyekwisha mwona Mungu kamwe; lakini kama tukipendana, Mungu anaishi katika muungano nasi, na upendo wake unakamilika ndani yetu.
13Tunajua kwamba tunaishi katika umoja na Mungu, naye Mungu anaishi katika umoja nasi, kwani yeye ametupa Roho wake. 14Sisi tumeona na kuwaambia wengine kwamba Baba alimtuma Mwanae awe Mwokozi wa ulimwengu. 15Kila mtu anayekiri kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu, Mungu anaishi katika muungano na mtu huyo, naye anaishi katika muungano na Mungu. 16Basi, sisi tunajua na tunaamini upendo alio nao Mungu kwetu sisi.
Mungu ni upendo, na kila mtu aishiye katika upendo, anaishi katika muungano na Mungu, na Mungu anaishi katika muungano naye. 17Upendo umekamilika ndani yetu kusudi tuweze kuwa na ujasiri#4:17 Tuweze kuwa na ujasiri: Ling 1Yoh 2:28. siku ile ya hukumu; kwani maisha yetu hapa duniani ni kama yale ya Kristo.#4:17 Maisha yetu …kama … ya Kristo: Yaani, kufanana kwa waumini na Kristo ndio msingi wa kuwa na ujasiri kwamba hatutahukumiwa na Mungu. 18Palipo na upendo hapana woga; naam, upendo kamili hufukuza woga wote. Basi, mtu mwenye woga hajakamilika bado katika upendo, kwani woga huhusikana na adhabu.
19Sisi tuna upendo kwa sababu Mungu alitupenda kwanza. 20Mtu akisema kwamba anampenda Mungu, hali anamchukia ndugu yake, huyo ni mwongo. Maana mtu asiyempenda ndugu yake ambaye anamwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hamwoni. 21Basi, hii ndiyo amri aliyotupa Kristo: Anayempenda Mungu anapaswa pia kumpenda ndugu yake.

Copyright The Bible Society of Tanzania, 1993

The Bible Society of Kenya 1993

Learn More About Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza