1 Petro 5
BHNTLK

1 Petro 5

5
Kundi la Mungu
1Mimi mzee miongoni mwenu wazee#5:1 Wazee: Wale ambao walikuwa wakurugenzi wa jumuiya ya Kikristo; Mate 11:30. wenzangu, mimi ambaye nilishuhudia mateso ya Kristo na kushiriki ule utukufu utakaofunuliwa, nawasihini#5:1 Petro alishuhudia kwa macho yake mwenyewe mateso na kusulubiwa kwake Kristo. 2mlichunge lile kundi la Mungu#5:2 Kundi la Mungu: Mate 20:28. Rejea maneno ya Yesu kwa Petro katika Yoh 21:15-17. mlilokabidhiwa; mlitunze si kwa kulazimika, bali kwa hiari kama atakavyo Mungu. Fanyeni kazi hiyo si kwa tamaa ya fedha, bali kwa moyo wenu wote. 3Msiwatawale kwa mabavu hao waliowekwa chini ya ulinzi wenu, bali muwe mfano kwa hilo kundi. 4Na wakati Mchungaji Mkuu#5:4 Mchungaji Mkuu: Yaani, Yesu Kristo; taz Yoh 10:11 maelezo. atakapotokea, nyinyi mtapokea taji ya utukufu isiyofifia.#5:4 Taji ya utukufu isiyofifia: Taz 2Tim 4:8 maelezo.
5Kadhalika nanyi vijana mnapaswa kujiweka chini ya mamlaka ya wazee. Nyinyi nyote mnapaswa kuwa na unyenyekevu mpate kutumikiana; maana Maandiko Matakatifu yasema: “Mungu huwapinga wenye majivuno, lakini huwajalia neema wanyenyekevu.”#5:5 Meth 3:34 (LXX); yamenukuliwa pia katika Yak 4:6. 6Basi, nyenyekeeni chini ya mkono wa enzi wa Mungu, ili awainue wakati ufaao. 7Mwekeeni matatizo yenu yote, maana yeye anawatunzeni.
8Muwe macho; kesheni! Maana adui yenu, Ibilisi, huzungukazunguka kama simba angurumaye akitafuta mawindo. 9Muwe imara katika imani na kumpinga, mkijua kwamba ndugu zenu pote duniani wanapatwa na mateso hayohayo. 10Lakini mkisha teseka muda mfupi, Mungu aliye asili ya neema yote na ambaye anawaiteni kuushiriki utukufu wake wa milele katika kuungana na Kristo, yeye mwenyewe atawakamilisheni#5:10 Atawakamilisheni: Au, “Atawathibitisheni”. na kuwapeni uthabiti, nguvu na msingi imara. 11Kwake yawe mamlaka milele! Amina.
Salamu za mwisho
12Nimewaandikieni barua hii fupi kwa msaada wa Silwano,#5:12 Silwano: Labda ni yule yule anayetajwa kama Sila katika Mate 15:22,40, na ambaye Paulo anamtaja katika 2Kor 1:19 na katika 1Thes 1:1; 2Thes 1:1. ndugu ambaye namjua na kumwamini. Nataka kuwapeni moyo na kushuhudia kwamba jambo hili ni neema ya Mungu kweli. Kaeni imara katika neema hiyo.
13Jumuiya ya wenzenu walioteuliwa na Mungu hapa Babuloni#5:13 Wenzenu …hapa Babuloni: Wakristo wa kwanza walitumia jina Babuloni kutaja Roma na hivyo kuepa kuutaja moja kwa moja huo mji mkuu wa himaya ya Waroma (Ufu 14:8; 17:5; 18:2). Hapa yaonekana kwamba barua hii iliandikwa mjini humo. wanawasalimuni. Vilevile mwanangu Marko anawasalimuni. 14Salimianeni kwa ishara ya upendo#5:14 Salimianeni kwa ishara ya upendo: Taz Rom 16:16 maelezo. wa Kikristo.
Nawatakieni amani nyinyi mlio wake Kristo.

Copyright The Bible Society of Tanzania, 1993

The Bible Society of Kenya 1993

Learn More About Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza