4
1Nakuamuru mbele ya Mungu, na mbele ya Kristo Yesu atakayewahukumu watu walio hai na wafu,#4:1 Yesu atakayewahukumu watu walio hai na wafu: Taz Mate 10:42; 1Pet 4:5. na kwa sababu anakuja kutawala akiwa Mfalme: 2hubiri huo ujumbe, sisitiza kuutangaza (iwe ni wakati wa kufaa au wakati usiofaa), karipia, onya na himiza watu ukiwafundisha kwa uvumilivu wote. 3Utakuja wakati ambapo watu hawatasikiliza mafundisho ya kweli, ila watafuata tamaa zao wenyewe na kujikusanyia waalimu tele watakaowaambia mambo yale tu ambayo masikio yao yako tayari kusikia. 4Watakataa kuusikia ukweli, watageukia hadithi za uongo. 5Wewe, lakini, uwe macho katika kila hali; vumilia mateso, fanya kazi ya mhubiri wa Habari Njema, timiza kikamilifu utumishi wako.
6Kwa upande wangu mimi, niko karibu kabisa kutolewa tambiko#4:6 Niko karibu kabisa kutolewa tambiko: Au, neno kwa neno, “mimi sasa namiminwa”, picha ya kutolewa kafara. na wakati wa kufariki kwangu umefika.#4:6 Tangu aya hii mpaka mwishoni mwa hii Barua mambo mengi yanajitokeza ambayo yanatupa picha ya mazingira ya Paulo gerezani kule Roma. 7#4:7 Mwandishi anatumia picha mbili kuelezea shughuli za mwaamini wa Kristo: vita (rejea 1Tim 1:18-19; 6:12), na mashindano katika riadha (rejea Mate 20:24; 1Kor 9:24; Ebr 12:1).Nimefanya bidii katika mashindano, nimemaliza safari yote na imani nimeitunza.#4:7 Imani nimeitunza: Kwa maana ya kutekeleza kila kitu kinachotakiwa kwa mtu anayemwamini Kristo na hata kutangaza hayo kwa uaminifu (1Tim 6:14). 8Na sasa imebakia tu kupewa tuzo la ushindi kwa maisha ya uadilifu,#4:8 Tuzo la ushindi kwa maisha ya uadilifu: Au, neno kwa neno: “taji ya uadilifu”. Yaweza pia kueleweka kama tuzo kwa maisha ya uadilifu. tuzo ambalo Bwana, Hakimu wa haki, atanipa mimi siku ile, na wala si mimi tu, ila na wale wote wanaotazamia kwa upendo kutokea kwake.
Maagizo
9Fanya bidii kuja kwangu karibuni. 10Dema#4:10 Dema: Kol 4:14; File 24. ameupenda ulimwengu huu akaniacha na kwenda zake Thesalonike. Kreske#4:10 Kreske: Anatajwa hapa tu. amekwenda Galatia,#4:10 Galatia: Mkoa wa utawala wa Waroma katika Asia Ndogo. na Tito#4:10 Tito: 2Kor 8:23; Gal 2:3; Tito 1:4. amekwenda Dalmatia.#4:10 Dalmatia: Sehemu ya Kusini ya mkoa wa Waroma wa Iluriko; eneo hili ndilo lililokuwa Yugoslavia ya zamani (Rom 15:19). 11Luka#4:11 Luka: Taz Kol 4:1 na rejea File 24. peke yake ndiye aliye hapa pamoja nami. Mpate Marko#4:11 Marko: Mate 12:12,25; 13:13; 15:37-39; Kol 4:10; File 24. uje naye, kwa maana ataweza kunisaidia katika kazi yangu. 12Nilimtuma Tukiko#4:12 Tukiko: Mate 20:4; Efe 6:21-22; Kol 4:7-8; Tito 3:12. kule Efeso. 13Utakapokuja niletee koti langu nililoacha kwa Karpo#4:13 Karpo: Haijulikani huyu alikuwa nani. kule Troa;#4:13 Troa: Bandari iliyopo Kusini kabisa na Magharibi mwa Asia Ndogo (Mate 16:8-11; 20:5-13; 2Kor 2:12-13). niletee pia vile vitabu, na hasa vile vya ngozi.#4:13 Vitabu hivyo vya papiri (mafunjo) au pengine vya ngozi, vilikuwa vya mviringo au msokoto, kwa Kiswahili cha zamani kidogo “gombo”. Hatujui kama vitabu hivyo vilihusu Maandiko Matakatifu ya kale au vitabu vya maandishi mengine.
14Yule sonara aitwaye Aleksanda#4:14 Aleksanda: Huyu aweza kuwa ni yule anayetajwa pia katika 1Tim 1:20. amenitendea maovu mengi; Bwana atamlipa#4:14 Bwana atamlipa …: Rejea Zab 62:11-12; Meth 24:12; Rom 2:5-6. kufuatana na hayo matendo yake. 15Jihadhari naye kwa sababu aliupinga ujumbe wetu kwa ukali.
16Wakati nilipojitetea kwa mara ya kwanza hakuna mtu aliyesimama upande wangu; wote waliniacha. Mungu asiwahesabie kosa hilo!#4:16 Mungu asiwahesabie kosa hilo: Maneno ambayo yalitumiwa pia na Stefano (Mate 7:60—8:1). 17Lakini Bwana alikaa pamoja nami, akanipa nguvu, hata nikaweza kuutangaza ujumbe wote, watu wa mataifa wausikie; tena nikaokolewa katika hukumu ya kifo kama kinywani mwa simba.#4:17 Kinywani mwa simba: Msemo wa kuelezea hatari ya kifo; rejea Zab 22:21; na pia Dan 6. 18Bwana ataniokoa na mambo yote maovu, na kunichukua salama mpaka katika ufalme wake wa mbinguni. Kwake uwe utukufu milele na milele! Amina.
Salamu za mwisho
19Wasalimu Priska na Akula,#4:19 Priska na Akula: Mate 18:2,18. Priska au Priskila ni jina la mtu yuleyule. pamoja na jamaa ya Onesiforo.#4:19 Onesiforo: Tazama 2Tim 1:16-18. 20Erasto#4:20 Erasto: Mate 19:22; Rom 16:23. alibaki Korintho, naye Trofimo#4:20 Trofimo: Mate 20:4; 21:29. nilimwacha Mileto#4:20 Mileto: Bandari pwani ya Bahari ya Ageo, Kusini mwa Efeso. kwa sababu alikuwa mgonjwa.
21Fanya bidii kuja kabla ya majira ya baridi.#4:21 Majira ya baridi: Wakati ambapo haikuwezekana kusafiri baharini. Ebulo, Pudensi, Lino na Klaudio wanakusalimu; vilevile ndugu wengine wote.#4:21 Hao wote wanaopeleka salamu zao ni Wakristo wa Kanisa la Roma.
22Bwana awe nawe rohoni mwako. Nawatakieni nyote neema.#4:22 Hati nyingine zinamalizia kwa neno “Amina”.