Baruku 1
BHNTLK

Baruku 1

1
Shabaha ya kitabu hiki
1Haya ni maneno yaliyoandikwa na Baruku mwana wa Neria, mjukuu wa Maaseya, wa ukoo wa Sedekia, Hasadia na Hilkia.#1:1 Baruku mwana wa Neria …Hilkia: Baruku, Neria na Maaseya wanatajwa katika Yer 32:12. Huyu Baruku alikuwa rafiki na katibu wa nabii Yeremia (taz Yer 36:4; 45:1). Baruku aliandika haya huko Babuloni#1:1 Huko Babuloni: Kadiri ya Yer 43:6-7, Baruku na Yeremia walipelekwa Misri mara baada ya kuuawa kwa Gedalia ambaye alikuwa mtawala wa mwisho huko Yerusalemu (2Fal 25:22-26). 2mnamo siku ya saba ya mwezi#1:2 Mwezi: Labda ni mwezi wa tano katika kalenda ya Kiebrania (taz 2Fal 25:8; Yer 52:12). katika mwaka wa tano#1:2 Siku ya saba ya mwezi …mwaka wa tano: Haisemwi ni mwezi gani lakini wengi wanafikiri ni mwezi wa tano katika kalenda ya Kiyahudi (taz aya 8 na rejea 2Fal 25:8 ambapo inasemwa Nebukadneza aliuteketeza mji wa Yerusalemu mnamo mwezi wa tano). Kuhusu “mwaka wa tano”, yaelekea kwamba mwandishi anahesabu tangu mji wa Yerusalemu ulipoteketezwa, yaani mwaka 586; kwa hiyo wakati wenyewe unaotajwa hapa ni mwaka 582 K.K., aghalabu siku ya ukumbusho ya tukio hilo. baada ya Wakaldayo kuuteka mji wa Yerusalemu na kuuteketeza.#1:2 Mji wa Yerusalemu ulitekwa mnamo mwaka 587 K.K. Kwa hiyo mwaka unaohusika hapa utakuwa yapata mwaka 582 K.K.
3Baruku aliyasoma maneno haya aliyoandika mbele ya mfalme Yekonia,#1:3 Yekonia: Jina lingine la Yoakimu, mfalme wa Yuda (taz Yer 22:24-30). Kuhusu aya yote rejea pia 2Fal 24:8-17. mwana wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, na mbele ya watu wote waliokuja kusikiliza, 4na mbele ya wakuu na wana wa wafalme,#1:4 Wakuu na wana wa wafalme: Rejea Yer 36:28; 38:6. na wazee; aliyasoma mbele ya watu wote, wakubwa kwa wadogo, ambao waliishi huko Babuloni pande za mto Sudi.#1:4 Mto Sudi: Mto huo haujulikani; hata hivyo, huenda ni mojawapo ya mifereji iliyopitia mjini Babuloni. Katika Eze 1:1 wale watu waliopelekwa uhamishoni kule Babuloni walikaa kwenye eneo la mto Kebari.
5Baada ya kuyasikia, waliomboleza, wakafunga chakula na kuomba dua kwa Bwana.#1:5 Bwana: Jina hili ambalo ni sawa na jina Mwenyezi Mungu kwa vile ni tafsiri ya Kigiriki ya jina hilo, linatumika mara nyingi sana katia sehemu ya kwanza ya kitabu hiki (1:15—3:8). Katika sehemu nyingine za kitabu hiki majina ya “Mungu” (kwa wingi zaidi), “Mungu wa milele” (4:35) “Mungu mtakatifu” (4:37; 5:5). Jambo hili la mtindo tofauti wa matumizi ya majina ya Mungu limesababisha kufikiri kwamba waandishi tofauti wanahusika. 6Kisha wakachanga fedha, kila mtu akatoa kadiri ya uwezo wake, 7wakizipeleka Yerusalemu kwa kuhani Yoakimu#1:7 Kuhani Yoakimu: Huyu kuhani hatajwi mahali pengine. mwanawe Hilkia, na mjukuu wa Shalumu, na kwa makuhani wengine pamoja na watu wote waliokuwa pamoja naye huko Yerusalemu.
8Siku ya kumi ya mwezi wa Siwani,#1:8 Mwezi wa Siwani: Huu ulikuwa mwezi wa tatu katika kalenda ya Kiyahudi (yapata Mei-Juni kadiri ya kalenda yetu). Katika 2Fal haitajwi kwamba mfalme Sedekia alitengeneza vyombo vya fedha mahali pa vile vilivyochukuliwa na majeshi ya Nebukadneza (rejea 2Fal 25:13-16). Baruku alitwaa vyombo vitakatifu vilivyokuwa vimetolewa katika nyumba ya Mungu, akavirudisha nchini Yuda.#1:8 Vyombo vitakatifu …akavirudisha nchini Yuda: Katika Ezra 1:7-11 tuna habari kwamba vyombo vitakatifu vilirudishwa Yerusalemu wakati wa mfalme Koreshi. Vyombo hivyo vya fedha vilikuwa vimetengenezwa na mfalme Sedekia mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, 9baada ya Nebukadneza mfalme wa Babuloni kumwondoa mfalme Yekonia huko Yerusalemu na kumpeleka Babuloni yeye pamoja na wakuu, wafungwa,#1:9 Wafungwa: Kigiriki. Katika tafsiri nyingine za kale tuna “mafundi”. wenye mamlaka na watu wengine wa kawaida.
Barua kwa watu wa Yerusalemu
10Basi, watu waliandika hivi:
Hizi ndizo fedha tunazowapelekeeni. Kwa fedha hizo tafadhali, nunueni wanyama wa sadaka za kuteketezwa na za kuondolea dhambi na ubani, mtayarishe na tambiko za nafaka, mzitoe juu ya madhabahu ya Bwana Mungu wetu; 11mwombeeni Nebukadneza#1:11 Mwombeeni Nebukadneza: Ezra 6:10; taz pia 1Tim 2:2 kuhusu kuwaombea walio na mamlaka ya kidunia, na rejea Yer 29:7. mfalme wa Babuloni na mwanawe Belshaza#1:11 Belshaza: Kigiriki ni “Baltasari”. Huyu hakuwa mwanawe Nebukadneza kama inavyotajwa hapa, ila alikuwa mwanawe Nabonido aliyekuwa mfalme wa mwisho katika himaya mpya ya Wababuloni (556-539 K.K.). waishi maisha marefu kama vile mbingu.#1:11 Maisha marefu kama vile mbingu: Kumb 11:21; Ezra 6:10; taz pia Zab 89:29. 12Hapo Bwana atatujalia nguvu na kuyaangaza macho yetu.#1:12 Kuyaangaza macho yetu: Rejea Zab 13:3 na 19:8 ambapo tafsiri hii inatoa maana ya msemo: “Huyaangazia macho” kama “kumwelimisha mtu”. Tutakaa chini ya ulinzi mwema wa Nebukadneza mfalme wa Babuloni na mwanawe Belshaza na kuwatumikia kwa muda wa siku nyingi na kupata kibali mbele yao. 13Hali kadhalika, mtuombee na sisi kwa Bwana Mungu wetu, maana tumetenda dhambi dhidi yake Bwana Mungu wetu na mpaka hivi sasa ghadhabu na hasira yake bado vinatukabili. 14Tafadhali, someni kitabu hiki tunachowapelekeeni, mkaungame dhambi zenu nyumbani mwa Bwana siku ya sikukuu ya vibanda na katika sikukuu nyingine.
Kuungama dhambi#1:15—2:10 Kuungama dhambi: Sehemu hii aghalabu ina shabaha ya kusema moja kwa moja juu ya uadilifu wa Mungu kwa upande mmoja, na uhalifu au uovu wa binadamu kwa upande mwingine: “Bwana Mungu wetu ni mwadilifu … sisi … tumejaa aibu” (1:15; 2:6); vile vile sehemu hii imeangaziwa na yanayosemwa katika Dan 9.
15Hivi ndivyo mtakavyosema:
“Bwana Mungu wetu ni mwadilifu, lakini sisi tulivyo leo tumejaa aibu!#1:15 Tumejaa aibu: Rejea Ezra 9:7; Bar 2:6; Dan 9:7; Zab 44:15; Yer 7:19. Sisi sote, watu wa Yuda na wakazi wa Yerusalemu, 16wafalme wetu, wakuu wetu, makuhani wetu, manabii wetu na wazee wetu.#1:16 Wafalme wetu …na wazee wetu: Yer 32:32. Katika Yer maneno: “wazee wetu” hayatajwi; badala yake tuna: “watu wa Yuda … na wakazi wa Yerusalemu”; rejea Bar 1:15. 17Sisi tumetenda dhambi dhidi ya Bwana. 18Tulimwasi, wala hatukutii sauti ya Bwana Mungu wetu aliposema tuishi kufuatana na amri alizotupa sisi. 19Tangu siku ile Bwana alipowatoa wazee wetu nchini Misri mpaka leo, tumeendelea kukosa utii kwa Bwana Mungu wetu, tukawa wazembe kuhusu jambo la kusikia sauti yake. 20Kwa hiyo, mpaka leo hii tumekabiliwa na balaa na laana zile alizotamka Mose#1:20 Laana zile alizotamka Mose: Kumb 28:15-68; Lawi 26:14-39. mtumishi wa Bwana kwa amri yake, siku ile alipowatoa wazee wetu nchini Misri ili kutupa nchi inayotiririka maziwa na asali. 21Sisi hatukusikiliza maneno ya manabii ambao Bwana Mungu wetu aliwatuma kwetu. 22Badala yake, kila mmoja wetu amepania kufuata mipango ya moyo wake mwovu, kwa kutumikia miungu mingine na kufanya yaliyo maovu mbele ya Bwana Mungu wetu.

Copyright The Bible Society of Tanzania, 1993

The Bible Society of Kenya 1993

Learn More About Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza