4
1Nanyi wakuu, watendeeni watumwa wenu kwa uadilifu na haki, mkikumbuka kwamba nanyi pia mnaye Bwana mbinguni.
Maagizo#4:2-6 Kisehemu hiki kina maagizo ya jumla kuhusu sala (aya 2-4) na juu ya uhusiano wa waumini Wakolosai na watu wasio Wakristo (aya 5-6).
2Dumuni katika sala, na mnaposali muwe waangalifu, mkimshukuru Mungu.#4:2 Kuhusu agizo la kudumu katika sala, taz pia Rom 12:12; Efe 6:18; Fil 4:6; 1Thes 5:17. 3Vilevile, mtuombee sisi pia ili Mungu atupe fursa ya kuuhubiri ujumbe wake kuhusu siri ya Kristo.#4:3 Siri ya Kristo: Taz Efe 1:9 maelezo. Kwa ajili hiyo mimi niko sasa kifungoni. 4Basi, ombeni ili niweze kusema kama inavyonipasa na kwa namna itakayodhihirisha siri hiyo.
5Muwe na hekima katika uhusiano wenu na watu wasioamini, mkitumia vizuri wakati mlio nao. 6Mazungumzo yenu yanapaswa kuwa daima mema na yaliyokolezwa kwa chumvi na ya kuvutia, na mnapaswa kujua jinsi ya kumjibu vizuri kila mmoja.
Salamu za mwisho#4:7-18 Sehemu hii ya mwisho ya Barua kwa Wakolosai ina salamu na ujumbe kwa watu kadha wa kadha: Tukiko na Onesimo ambao watapeleka hii barua kwa Wakolosai na kuwapa habari za Paulo na wenzake (aya ya 7-9), salamu kutoka kwa watu sita walio pamoja na Paulo (aya ya 10-14), salamu kwa waumini wa Laodikea, kwa Nimfa na Arkipo (aya ya 14-17); na hatima ambayo imeandikwa na Paulo mwenyewe (aya ya 18).
7Ndugu yetu mpenzi Tukiko,#4:7 Tukiko: Rejea Mate 20:4; 2Tim 4:12. Tukiko, mwenyeji wa Asia, alikuwa mwenzake Paulo katika kuhubiri Injili. Paulo alimpa hii barua aipeleke kwa Kanisa la Kolosai. Kulingana na Efe 6:21 Tukiko ndiye pia aliyewapelekea Waefeso ile Barua yao. mfanyakazi mwaminifu na mtumishi mwenzetu katika kazi ya Bwana, atawapeni habari zangu zote. 8Ndiyo maana ninamtuma, ili aichangamshe mioyo yenu kwa kuwaambieni habari zetu. 9Anakuja pamoja na Onesimo,#4:9 Onesimo: Huyu alikuwa mtumwa mkimbizi ambaye Paulo alimrudisha kwa bwana wake, yaani Filemoni (File 10-12). ndugu yetu mpenzi na mwaminifu, ambaye ni mwananchi mwenzenu. Watawapeni habari za mambo yote yanayofanyika hapa.
10Aristarko,#4:10 Aristarko: Huyu alikuwa mwenzake Paulo katika kuhubiri Injili; alikuwa mwenyeji wa Thesalonike (Mate 19:29; 27:2; File 24). ambaye yuko kifungoni pamoja nami, anawasalimuni; hali kadhalika Marko,#4:10 Marko: Anaitwa pia Yohane Marko, kutoka Yerusalemu (Mate 12:12,25; 13:5,13; 15:37-38); alikuwa binamu yake Barnaba na aliandamana na Paulo katika miaka ya mwanzo ya huduma zake za kitume (Mate 4:36; 13:1—15:39; File 24). binamu yake Barnaba, (mmekwisha pata maagizo juu yake; akifika kwenu mkaribisheni). 11Naye Yoshua aitwaye Yusto,#4:11 Yoshua aitwaye Yusto: Hakuna habari nyingine juu yake. anawasalimuni. Miongoni mwa Wayahudi waliokwisha pokea imani, hawa tu peke yao, ndio wanaofanya kazi pamoja nami kwa ajili ya ufalme wa Mungu; nao wamekuwa msaada mkubwa kwangu. 12Epafra,#4:12-13 Epafra: Kol 1:7. Yaonekana kwamba Epafra alikuwa na madaraka fulani huko Kolosai na pia katika vijiji vya karibu kama vile Laodikea (taz Kol 2:1 maelezo) na pia kule Hierapoli. mwananchi mwenzenu na mtumishi wa Kristo Yesu, anawasalimuni. Daima anawaombeeni nyinyi kwa bidii ili mpate kusimama imara, mkomae na kuwa thabiti kabisa katika mambo yote anayotaka Mungu. 13Naweza kushuhudia kwamba anafanya kazi kwa bidii kwa ajili yenu na kwa ajili ya watu wa Laodikea na Hierapoli. 14Luka,#4:14 Luka: 2Tim 4:11; File 24. Kadiri ya mapokeo ya kale, Luka aliandamana na Paulo katika safari zake nyingi za kuhubiri Habari Njema na ni mwandishi wa Injili ambayo inajulikana kwa jina lake na pia Kitabu cha Matendo ya Mitume. Hapa anaitwa “daktari”, na wafafanuzi wengi wa Biblia wanafikiri kwamba hakuwa Myahudi (hasa kwa vile hatajwi pamoja na waumini wa Kiyahudi waliotajwa katika aya ya 11). daktari wetu mpenzi, na Dema,#4:14 Dema: 2Tim 4:10; File 24. wanawasalimuni.
15Salamu zetu kwa ndugu wa Laodikea. Msalimuni dada Nimfa pamoja na jumuiya yote ya waumini inayokutana nyumbani kwake.#4:15 Nimfa …jumuiya yote ya waumini inayokutana nyumbani kwake: Nimfa ni jina la mwanamke. Maneno yanayofuata baada ya kumtaja Nimfa yanadokezea kwamba mwanzoni mwa kanisa waumini walikuwa na desturi ya kukutana katika nyumba za pekee zilizokuwa za waumini (taz Rom 16:5 maelezo). 16Mkisha soma barua hii, hakikisheni kwamba inasomwa na Wakristo wa Laodikea; na nyinyi fanyeni mpango mpate kuisoma barua waliyoipata wao.#4:16 Laodikea …barua waliyoipata wao: Inavyoonekana ni kwamba Paulo, kabla ya kuandika barua hii, alikuwa amewaandikia waumini wa Laodikea barua nyingine, lakini hii haikuhifadhiwa na kutufikia sisi. Baadhi wanasema inaweza kuwa ni barua ile ile aliyowaandikia Waefeso. 17Mwambieni Arkipo#4:17 Arkipo: File 2. aitekeleze vizuri ile huduma aliyokabidhiwa na Bwana. 18Naandika haya kwa mkono wangu mwenyewe:#4:18 Naandika …kwa mkono wangu mwenyewe: Taz 1Kor 16:21 maelezo. Salamu kutoka kwangu, mimi Paulo. Kumbukeni kwamba niko kifungoni. Neema ya Mungu iwe nanyi.