29
Agano la Mwenyezi-Mungu na Waisraeli nchini Moabu
1Haya ni maneno ya agano ambalo Mwenyezi-Mungu aliwaamuru Mose kufanya na Waisraeli katika nchi ya Moabu,#29:1 Agano …Mwenyezi-Mungu alimwamuru Mose kufanya na Waisraeli … Moabu: Huku kufanya upya kwa lile agano kulikuwa lazima kwa sababu kizazi kile ambacho Mungu alifanya agano nacho kule Sinai, watu wale wote, walikwisha kufa kule jangwani, na sasa kulikuwa na kizazi kipya ambacho kilikuwa tayari kuingia katika ile nchi ambayo Mungu aliahidi kuwapa watu wake. Agano lile la Sinai na hili la Moabu yote mawili yana yale masharti, yaani Amri Kumi na Mbili lakini kila moja lina mambo yake tofauti na lingine. licha ya agano Mwenyezi-Mungu alilofanya nao mlimani Horebu. 2Mose aliwaita pamoja Waisraeli wote akawaambia, “Mliona nyinyi wenyewe jinsi Mwenyezi-Mungu alivyomtendea mfalme wa Misri,#29:2 Mliona …jinsi Mwenyezi-Mungu alivyomtendea mfalme wa Misri …: Taz Kut 1—12. Kuwakumbusha Waisraeli matendo ya Mungu kwa ajili yao ni njia moja ya kuwafanya wasisimke na kukiri tena imani yao kwa Mwenyezi-Mungu. maofisa, watumishi wake na nchi yake yote. 3Mliona maafa makubwa, ishara na maajabu aliyotenda. 4Lakini mpaka leo Mwenyezi-Mungu hajawapa akili ya kuelewa,#29:4-6 Mpaka hivi leo …hajawapa akili ya kuelewa: Mose anawaambia kwamba hata matendo hayo makuu ya Mungu hayakuwafanya Waisraeli wawe waaminifu. Taz pia Rom 11:8. Ni mabadiliko ya moyo ndiyo tu yatakayoweza kufanya hayo (Yer 31:31-34). macho ya kuona, wala masikio ya kusikia!
5“Kwa muda wa miaka arubaini, mimi niliwaongoza jangwani, nguo zenu mlizovaa hazikuchakaa wala viatu vyenu havikuchakaa miguuni mwenu. 6Hamkula mkate wala kunywa divai au kileo chochote kile, mpate kujua kwamba Mwenyezi-Mungu ni Mungu wenu.
7“Na mlipofika mahali hapa, mfalme Sihoni wa Heshboni na mfalme#29:7 Mfalme Sihoni wa Heshboni na mfalme: Kuhusu kushindwa kwa wafalme hao na Waisraeli taz Hes 21:21-35 na Kumb 2:26—3:11. Ogu wa Bashani walikuja kupigana nasi; lakini tukawashinda, 8tukaichukua nchi yao, tukayagawia makabila ya Reubeni na Gadi#29:8 Tukayagawia makabila ya Reubeni na Gadi …: Taz Hes 32:33. Sehemu ya nchi inayotajwa hapa ni mashariki ya mto Yordani. na nusu kabila la Manase iwe mali yao. 9Kwa hiyo muwe waangalifu kushika maneno yote ya agano hili ili mpate kufanikiwa katika kazi zenu zote.
10“Leo, mmesimama mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, nyinyi nyote viongozi wa makabila, wazee wenu, maofisa wenu, 11watoto wenu na wake zenu, wageni wanaoishi miongoni mwenu ambao hukata kuni na kuwatekea maji. 12Mko hapa leo ili kufanya agano hili ambalo Bwana Mungu wenu anafanya leo, 13kwamba atawathibitisha leo kuwa watu wake naye atakuwa Mungu wenu, kama alivyowaapia nyinyi na babu zenu: Abrahamu, Isaka na Yakobo. 14Wala sifanyi agano hili leo kwa niaba yenu tu na kutamka laana zake; sifanyi kwa niaba ya wale tu walio pamoja nasi leo mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, 15bali pia kwa niaba ya wale ambao hawapo pamoja nasi leo.
16“Mnajua jinsi tulivyoishi nchini Misri na jinsi tulivyosafiri katika nchi za mataifa mengine. 17Mliona sanamu#29:16-17 Tulivyoishi nchini Misri …mataifa mengine … mliona sanamu: Wamisri na watu wa mataifa mengine kule Mashariki ya Kati ya Kale waliabudu miungu wengi. Kule Misri kulikuwa na miungu hata yenye vichwa vya wanyama, kama yule aitwaye “Apis” (ng'ombe dume), “Mnevis” (ng'ombe jike), na “Khum” (kondoo dume). Hata Farao, mfalme wa Misri, alichukuliwa kuwa ni mungu. zao za kuchukiza, miungu ya miti na mawe, ya fedha na dhahabu. 18Chukueni hadhari kwamba hakuna mwanamume, mwanamke, jamaa au kabila lolote linalosimama hapa leo litakalomwacha Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, kwenda kutumikia miungu ya mataifa mengine. Jambo hili litakuwa kama mzizi utakaomea na kuzaa matunda machungu yenye sumu.#29:18 Mzizi …kuzaa matunda machungu yenye sumu: Mtu mmoja katika jamii atakayeabudu miungu ya uongo anaweza kuwavuta Waisraeli wengine nao wakamwiga na hivyo kupata adhabu. Taz pia Ebr 12:15. 19Kama baada ya kusikia maneno ya agano hili ambayo mmeapishwa, halafu mtu akajiamini mwenyewe moyoni mwake na kusema atakuwa salama, hata kama atafuata ukaidi wake mwenyewe, hiyo itawaangamiza wote, wabaya na wema. 20Mwenyezi-Mungu hatasamehe mtu huyo, nayo hasira ya Mwenyezi-Mungu na wivu wake vitamwakia mtu huyo; laana zote#29:20 Laana zote: Baadhi ya laana hizo zimeandikwa katika 27:11-26; ling Eze 14:7; 23:25; Zab 74:1; 79:5. zilizoandikwa katika kitabu hiki zitamjia, naye Mwenyezi-Mungu atalifuta kabisa jina la mtu huyo kutoka duniani. 21Mwenyezi-Mungu atamtenga kutoka miongoni mwa makabila yote ya Israeli apatwe na maafa kufuatana na laana zote za agano zilizoandikwa katika kitabu hiki. 22Katika vizazi vijavyo, wazawa wenu na wageni kutoka nchi ya mbali wataona jinsi Mwenyezi-Mungu alivyoiletea nchi hii maafa na mateso: 23imejaa madini ya kiberiti na chumvi, imeteketea na kuwa tupu, haikupandwa mbegu na haioti chochote. Ni kama ilivyokuwa wakati Mwenyezi-Mungu alipoangamiza Sodoma na Gomora, Adma na Seboimu,#29:23 Sodoma …Seboimu: Mungu aliangamiza Sodoma na Gomora kwa sababu ya uovu wa wakazi wake (Mwa 18:16-28; 19:24-25). Na kuhusu Adma na Seboimu, wafafanuzi wa Biblia wanafikiri ni miji iliyokuwa karibu na Sodoma na Gomora (Mwa 10:19) na hivyo huenda iliangamizwa pamoja nayo (taz Hos 11:8). kwa hasira yake kali. 24Naam, mataifa yote yatasema: ‘Kwa nini Mwenyezi-Mungu ameitendea hivyo nchi hii? Hasira hii kubwa inamaanisha nini?’ 25Na jibu litatolewa: ‘Ni kwa sababu walivunja agano la Mwenyezi-Mungu, Mungu wa wazee wao ambalo alifanya nao alipowatoa katika nchi ya Misri, 26wakaenda kuitumikia na kuiabudu miungu mingine, ambayo hawakuijua hapo awali, wala Mwenyezi-Mungu hakuwa amewapa. 27Kwa hiyo hasira ya Mwenyezi-Mungu iliwaka dhidi ya nchi hii, na kuiletea laana zote zilizoandikwa katika kitabu hiki. 28Naye Mwenyezi-Mungu, akawang'oa kutoka katika nchi yao kwa hasira na ghadhabu kubwa, akawatupa katika nchi nyingine kama ilivyo leo.’#29:24-28 Kisehemu hiki chenye mtindo wa mshangao wenye maswali na majibizano ya watu wengine kuhusu maafa yaliyowapata Waisraeli unatumika pia katika 1Fal 9:8-9. Taz pia Yer 16:10-11. Mtindo huu una shabaha ya kuonesha uzito wa jambo linalohusika.
29“Mambo ya siri ni ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, lakini yale ambayo ameyafunua ni yetu na wazawa wetu milele, ili tutekeleze maneno yote ya sheria hii.”