33
Mose anayabariki makabila ya Israeli#33:1-29 Mose anayabariki makabila ya Israeli: Mose, kama baba wa Waisraeli, anawaaga watu wa makabila yale kumi na mawili kwa kuwapa baraka, kama ilivyokuwa desturi katika A.K. kwa mzee kuwabariki watoto wake kabla ya kufa (Mwa 27:27-40; 48:15-16; 49:1-28). Katika orodha ya hayo makabila jina la Simeoni limeachwa, hata hivyo idadi ya kumi na mbili inazingatiwa kwa kutaja badala ya Yosefu, watoto wake wawili, Efraimu na Manase (Mwa 48:8-14).
1Hii ndiyo baraka ambayo Mose, mtu wa Mungu#33:1 Mose, mtu wa Mungu: “Mtu wa Mungu” ni jina la sifa ambalo manabii waliitwa (taz 1Fal 17:18; 2Fal 4:7,9). Jina hili la sifa anapewa Mose pia katika kichwa cha Zab 90 na katika Yos 14:6. aliwatakia Waisraeli kabla ya kufariki kwake. Alisema:
2Mwenyezi-Mungu alikuja kutoka mlima Sinai,
alitutokea kutoka mlima Seiri;
aliiangaza kutoka mlima Parani.#33:2 Mwenyezi-Mungu alikuja kutoka mlima Sinai …Seiri … Parani: Katika aya hii na hasa kulingana na mpangilio wake, mlima Parani huenda ni sawa na mlima Sinai. Jangwa la Parani (Hes 10:13) lilikuwa kwenye eneo la peninsula ya Sinai. Na kuhusu “Seiri” tunachojua ni kwamba ni jina lingine la Edomu. Watu wa Edomu walikuwa wazawa wa Esau, ndugu-pacha wa Yakobo.
Alitokea kati ya maelfu ya malaika,
na moto uwakao katika mkono wake wa kulia.
3Mwenyezi-Mungu aliwapenda watu wake;
na huwalinda watakatifu wake wote.
Hivyo, malaika wake walifuata nyayo zake,
na kupata maagizo kutoka kwake.
4Mose alituamuru tutii sheria;
kitu cha thamani kuu cha taifa letu.
5Mwenyezi-Mungu akawa mfalme wa Israeli,
wakati viongozi wao walipokutana,
na makabila yote yalipokusanyika.
6Mose alisema juu ya kabila la Reubeni:#33:6 Kabila la Reubeni: Reubeni alipoteza haki yake ya kuwa mzaliwa wa kwanza wa Yakobo kwa kosa lake na mmoja wa wake za baba yake (Mwa 35:22) na kabila linalotajwa kwa jina lake lilikuwa dogo.
“Reubeni aishi wala asife,
na watu wake wasiwe wachache.”
7Juu ya kabila la Yuda#33:7 Kabila la Yuda: Yuda, mwanawe Yakobo na Lea alikuwa na baraka ya pekee kutoka kwa baba yake (Mwa 49:8-12). Ling Mwa 49:8. alisema:
“Ee Mwenyezi-Mungu usikilize kilio cha kabila la Yuda;
umrudishe tena kwa watu wale wengine.
Upigane kwa mikono yako kwa ajili yake,
ulisaidie kabila la Yuda dhidi ya adui zake.”
8Juu ya kabila la Lawi,#33:8 Kabila la Lawi: Lawi alikuwa mtoto mwingine wa Yakobo na Lea (Mwa 49:4-7). Kuhusu “Urimu” na “Thumimu”, taz Kut 28:30 maelezo. Walawi walipewa jukumu la kutunza sanduku la agano ambalo lilikuwa na amri za Mungu. alisema:
“Ee Mwenyezi-Mungu ulipatie Lawi kauli yako ya Urimu,
kauli yako ya thumimu kwa hao waaminifu wako,
ambao uliwajaribu huko Masa.
9Ulishindana nao kwenye maji ya Meriba.
Walawi walioamua kuwaacha wazee wao,
wakawasahau jamaa zao,
wasiwatambue hata watoto wao
maana walizingatia amri zako,
na kushika agano lako.
10Na wawafundishe wazawa wa Yakobo maagizo yako;
wawafundishe watu wa Israeli sheria yako.
Walawi na wafukize ubani mbele yako,
sadaka nzima za kuteketezwa madhabahuni pako.
11Ee Mwenyezi-Mungu, uzibariki nguvu zao,
uzikubali kazi za mikono yao;
uzivunjilie mbali nguvu za maadui zao,
nguvu za wanaowachukia hata wasiinuke tena.”
12Juu ya kabila la Benyamini#33:12 Kabila la Benyamini: Benyamini alikuwa mtoto wa mwisho wa Yakobo na Raheli. Katika Mwa 49:27 anaitwa “mbwamwitu mkali”. Watu wa kabila hili walikuwa hodari katika kupigana vita. alisema:
“Hili ni kabila alipendalo Mwenyezi-Mungu,
nalo hukaa salama karibu naye.
Yeye hulilinda mchana kutwa,
na kukaa kati ya milima yake.”
13Juu ya kabila la Yosefu alisema:
“Mwenyezi-Mungu na aibariki nchi yake,
kwa baraka nzuri kabisa kutoka juu,
14ibarikiwe kwa matunda bora yalioiva kwa jua,
kwa matunda ya kila mwezi;
15kwa mazao bora ya milima ya kale,
na mazao tele ya milima ya kale,
16Nchi yake ijae yote yaliyo mema,
ibarikiwe kwa wema wa Mwenyezi-Mungu,
ambaye alitokea katika kichaka.
Baraka hizi ziwashukie watu wa kabila la Yosefu,
aliyekuwa mkuu miongoni mwa ndugu zake.
17Fahari yake ni fahari ya fahali wa kwanza,
pembe zake ni za nyati dume.
Atazitumia kuyasukuma mataifa;
yote atayasukuma mpaka miisho ya dunia.
Efraimu atakuwa na pembe hizo 10,000
na Manase#33:13-17 Kabila la Yosefu …Efraimu na Manase: Hapa baraka anazotakiwa Yosefu zinaambatishwa na za Efraimu na Manase. Lakini katika Mwa 49:22-27 ni Yosefu peke yake ambaye anapata baraka. Na hiyo ni sawa kwani Efraimu na Manase walikuwa bado watoto wadogo kadiri ya simulizi la Mwanzo. kwa maelfu.”
18Juu ya kabila la Zebuluni na kabila la Isakari,#33:18-19 Zebuluni …Isakari: Taz Mwa 49:13-15. Zebuluni na Isakari walikuwa watoto wa Yakobo na Lea. alisema,
“Zebuluni, furahi katika safari zako;
nawe Isakari, furahi katika mahema yako.
19Watawaalika wageni kwenye milima yao,
na huko watu watatoa sadaka zinazotakiwa.
Maana wao watapata utajiri wao kutoka baharini
na hazina zao katika mchanga wa pwani.”#33:19 Utajiri kutoka baharini …katika mchanga wa pwani: Inachukuliwa kwamba makabila hayo mawili yalikuwa na maeneo yao kwenye mwambao wa Bahari ya Mediteranea. Kwamba utajiri wao wataupata pia katika mchanga wa pwani si dhahiri, lakini wengi wanafikiri ilihusu shughuli za kutengeneza vioo ambavyo vilitengenezwa kwa madini ya ulanga na wakati huo vilikuwa na thamani kubwa.
20Juu ya kabila la Gadi,#33:20 Kabila la Gadi: Taz Mwa 49:19. Gadi alikuwa mtoto wa Yakobo na Zilpa ambaye alikuwa mtumishi wa kike wa Lea. Jina “Gadi”, Kiebrania, maana yake ni bahati (njema); taz Mwa 30:11. alisema:
“Atukuzwe Mungu ampatiaye Gadi sehemu kubwa.
Gadi hunyemelea kama simba
akwanyue mkono na utosi wa kichwa.
21Alijichagulia eneo zuri kuliko yote,
mahali ilipotengwa sehemu ya kiongozi.
Aliwaongoza watu na kumtii Mwenyezi-Mungu,
alitekeleza mpango wa Mungu kwa Israeli.”
22Juu ya kabila la Dani#33:22 Kabila la Dani: Dani alikuwa mtoto wa Yakobo na Raheli. Taz pia Mwa 49:16-17. alisema hivi:
“Dani ni mwanasimba
arukaye kutoka Bashani.”
23Juu ya kabila la Naftali#33:23 Kabila la Naftali: Naftali alikuwa mwanawe Yakobo na Bilha ambaye alikuwa mtumishi wa kike wa Raheli. Taz Mwa 49:21. alisema:
“Ee Naftali fadhili,
uliyejaa baraka za Mwenyezi-Mungu,
nchi yako ni kusini kwenye ziwa Kinerethi.”
24Juu ya kabila la Asheri#33:24 Kabila la Asheri: Asheri alikuwa mtoto wa Yakobo na Zilpa ambaye alikuwa mtumishi wa kike wa Lea. Taz Mwa 49:20. alisema:
“Asheri abarikiwe kuliko watoto wote wa Yakobo,
na upendelewe na ndugu zako wote;
na achovye mguu wake katika mafuta.
25Miji yako ni ngome za chuma na shaba.
Usalama wako utadumu maisha yako yote!”
26Mose akamalizia kwa kusema,
“Ee Israeli, hakuna aliye kama Mungu wako,
yeye hupita mbinguni kuja kukusaidia,
hupita juu angani katika utukufu wake.
27Mungu wa milele ndiye kimbilio lenu;
nguvu yake yaonekana duniani.
Aliwafukuza maadui mbele yenu;
aliwaamuru: ‘Waangamizeni.’
28Kwa hiyo, watu wa Israeli wakakaa salama,
wazawa wa Yakobo peke yao,
katika nchi iliyojaa nafaka na divai,
nchi ambayo anga lake hudondosha umande.
29Heri yenu nyinyi Waisraeli.
Nani aliye kama nyinyi, watu mliookolewa na Mwenyezi-Mungu,
ambaye ndiye ngao ya msaada wenu,
na upanga unaowaletea ushindi!
Adui zenu watakuja wananyenyekea mbele yenu,
nanyi mtawakanyaga chini.”