11
Afanyavyo mwenye busara
1Jishughulishe na biashara
hata kama kwa kubahatisha;
yawezekana baadaye
ukapata chochote kile.
2Wagawie watu#11:1-2 Wagawie watu …: Tafsiri ya aya ya 1 ni ya makala ya Kiebrania iliyo ngumu na ambayo neno kwa neno ni : “Tupa chakula chako usoni pa maji … utakiona baada ya siku nyingi”. Wengi wamechukua maneno hayo kuwa na maana ya kuwasaidia maskini (Kumb 15:10; Gal 6:9,10). Lakini huenda kuna uhusiano wa namna hii ya kusema na Isa 18:2 ambapo yahusu kufanya biashara. saba hata wanane sehemu yako,
maana, hujui balaa litakalofika duniani.
3Mawingu yakijaa maji, mvua hunyesha;
mti ukiangukia kusini au kaskazini,
hapo uangukiapo ndipo ulalapo.
4Anayengoja upepo hatapanda mbegu,
anayesubiri mawingu yatoweke, hatavuna#11:4-6 Anayesubiri mawingu …hatavuna: Ni msemo ulio na madhumuni ya kumwonya mtu kwamba kila kitu kiko katika uwezo wake Mungu na kwamba anachotakiwa mtu ni kufanya bidii kwani hajui litakalotokea. kitu.
5Usivyojua jinsi uhai unavyoingia katika mifupa ya mtoto tumboni mwa mamake, kadhalika huwezi kuelewa matendo ya Mungu, ambayo hufanya kila kitu. 6Panda mbegu asubuhi na jioni usiache kupanda, maana, hujui zipi zitaota; za asubuhi, za jioni, au zote zitakuwa nzuri. 7Mwanga wafaa, na kuliona jua kwapendeza macho. 8Mtu akiishi miaka mingi, na aifurahie miaka hiyo yote; lakini akumbuke kuwa siku za giza#11:7-8 Mwanga …giza: Mwandishi anakiri kwamba katika maisha kuna uzuri (aya 7); na kwamba kuna siku za giza (kwa maana ya siku mbaya au kifo) zitakuwa nyingi. Ulinganisho baina ya giza na mwanga ni wazo kawaida katika Biblia na wazo hilo lilijitokeza tangu 2:13-14. zitakuwa nyingi, na kwamba yote yatakayofuata ni bure.
Mawaidha kwa vijana
9Ewe kijana, furahia ujana wako, moyo wako, uchangamke wakati ungali kijana. Fuata mapenzi ya moyo wako na upeo wa macho yako. Lakini kumbuka kwamba Mungu atakuhukumu#11:9 Fuata mapenzi ya moyo wako …lakini … Mungu atakuhukumu: Sehemu ya kwanza ya aya hii inaonekana kwa jumla kwamba ni mtazamo wa kawaida wa huyo mwanafalsafa (taz 2:24-26; 3:12,13,22; 5:18-20; 9:7). Lakini mtazamo huo hauna lengo la kuhimiza maisha ya hovyo au ya kipumbavu (5:1-7). Ndio maana sehemu ya pili (hata kama wengine wanafikiri ilijumlishiwa hapo baadaye) inammwonya binadamu juu ya athari za kuishi bila kumtii Mungu (taz pia 12:14). kadiri ya hayo yote. 10Ondoa mahangaiko moyoni mwako, jikinge, usipate maumivu mwilini kwa sababu ujana na mwisho wa maisha ni bure kabisa.