12
1Umkumbuke Muumba wako#12:1 Umkumbuke Muumba wako: Ili kukumbuka kifo mwandishi anakwenda hadi mwanzoni mwa kila kitu, anamkuta Muumba ambaye ndiye chanzo cha “roho” (uhai wa binadamu) ambayo binadamu alipewa pale mwanzoni na ambayo sasa itamrudia mwenyewe, yaani Mungu (3:14-15; 9:1; taz pia Mwa 1:27; 2:7,21-23; Zab 8:3-5). siku za ujana wako,
kabla hazijaja siku na miaka ambapo utasema:
“Sifurahii tena vitu hivyo!”#12:1-12 Anapomalizia kitabu chake, huyu mwanafalsafa anawaza na kuwazua juu ya ujana, uzee na kifo. Kwa mtindo maalumu kabisa wa kishairi anatazama mabadiliko yanayokuja ya uzee na kuingia kwa kifo (12:6) na kumalizia katika aya 8 na maneno yale yale aliyoanzia nayo kitabu chake: “Yote ni bure kabisa! Yote ni bure.”
2Umkumbuke kabla ya wakati ambapo kwako mwanga wa jua utafifia;
mwezi na nyota haviangazi tena,
nayo mawingu yametanda#12:2 Mwanga …utafifia … mawingu yametanda: Mwandishi huyu stadi analinganisha uzee na siku ya mawingu ambapo na mwanga unafifia. Taz pia Yobu 3:1-6. tena baada ya mvua.
3Wakati ambapo mikono inayokulinda inatetemeka,
miguu yako imara imepindika,
meno yako ya kusagia hayafai kwa uchache,
na macho ya kuchungulia dirishani yamefifia.
4Wakati ambapo milango ya masikio yako imezibika,
na sauti za visagio ni hafifu;
lakini usiku hata kwa sauti ya ndege utagutuka.
5Wakati huo utaogopa kupanda mahali pa juu
na kutembea barabarani ni kitisho;
wakati miti ya mlozi inachanua na panzi wanashiba,#12:5 Miti ya mlozi …panzi wanashiba: Maana ya aya 5a ni dhahiri (mtu huyo ni mzee kiasi cha kutoweza kumudu kama alivyokuwa kijana). Lakini aya 5b si dhahiri. Hata hivyo, inaonekana kwamba hali ya huyo mzee bado inaelezwa, iwe kwa nywele nyeupe za uzee na kutokuwa tena na hamu ya chakula wakati kipo tele. Maneno: “makao yake ya milele” yanahusu aghalabu kaburi ambamo atazikwa karibuni.
lakini wewe hutakuwa na hamu tena.
Wakati huo binadamu anapaswa kwenda katika makao yake ya milele,
nao waombolezaji watapitapita barabarani.
6Wakati huo uzi wa dhahabu utakatika,
bakuli la dhahabu litapasuka,
mtungi wa maji utavunjikia kisimani,
kadhalika na gurudumu la kuvutia maji.#12:6 Uzi wa dhahabu …gurudumu la … maji Maji katika Biblia mara nyingine ni mfano wa uhai na kumwagika kwake ni ishara ya kifo. “Maji yaliyomwagika hayazoeleki” kama isemavyo methali ya Kiswahili; na hapa kama chombo cha kuchotea kuvunjika basi, hali yenyewe ni kifo.
7Nawe vumbi utarudia udongoni#12:7 Vumbi utarudia udongoni: Aya hii na 3:20 zinamkumbusha msomaji juu ya simulizi la kuumbwa ulimwengu na binadamu (Mwa 2:7 na 3:20). Uhai wote watoka katika pumzi ya Mungu na wakati wa kifo pumzi hiyo ya uhai inamrudia Muumba wake (taz pia Zab 104:29-30). Katika aya ya 8 Mwanafalsafa huyu anamalizia utenzi wake huu kwa kuweka “fremu” ya kubana sehemu yote na maneno yale yale aliyoanzia nayo: “Yote ni bure kabisa! (zingatia marudio ya “bure” katika Kiebrania) Yote ni bure.” ulimotolewa
na roho yako itamrudia Mungu aliyeiumba.
8Mimi Mhubiri nasema: Yote ni bure kabisa! Yote ni bure.
Hatima
9Basi, zaidi ya kuwa na hekima yake, Mhubiri aliwafundisha watu ujuzi. Alizipima, akazichunguza na kuzirekebisha methali kwa ustadi mwingi. 10Mhubiri alijitahidi kupata maneno ya kupendeza, akaandika kwa ufasaha maneno ya kweli.
11Misemo ya wenye hekima ni kama michokoo na methali zilizokusanywa pamoja na mchungaji mmoja ni kama vigingi vilivyopigiliwa imara ardhini. 12Zaidi ya hayo, mwanangu, jihadhari! Kuandika vitabu hakuna mwisho na kusoma kwingi huchokesha mwili.
13Baada ya hayo yote yaliyokwisha semwa bado kuna hili linalotakiwa: Mche Mungu, na uzishike amri zake;#12:13-14 Mche Mungu, na uzishike amri zake: Hili ndilo jambo muhimu kupita yote. kwa sababu hilo ndilo jukumu aliloumbiwa binadamu. 14Maana, Mungu atahukumu matendo yetu yote, hata yale yanayotendwa kwa siri, yawe mema au mabaya.