6
1Basi, tuyaache nyuma yale mafundisho ya mwanzomwanzo juu ya Kristo, tusonge mbele kwa yale yaliyokomaa, na sio kuendelea kuweka msingi kuhusu kuachana na matendo ya kifo, na juu ya kumwamini Mungu;#6:1-2 Mwandishi anaorodhesha kanuni sita za msingi au za mwanzo katika maisha ya Kikristo. 2mafundisho juu ya ubatizo#6:2 Mafundisho juu ya ubatizo: Msemo ambao unaweza kujumuisha namna za kutawadha za Kiyahudi ambazo zilichukuliwa kuwa zimepitwa na wakati kutokana na ubatizo wa Kikristo. na kuwekewa mikono;#6:2 Kuwekewa mikono: Rejea Mate 8:17; 19:6. ufufuo wa wafu na hukumu ya milele. 3Hilo tutafanya, Mungu akipenda.
4Maana watu waliokwisha kuangaziwa,#6:4 Waliokwisha kuangaziwa: Yamkini yahusu kupokea imani. wakaonja zawadi za mbinguni, wakashirikishwa Roho Mtakatifu 5na kuonja wema wa neno la Mungu na nguvu za ulimwengu ujao, 6kisha wakaiasi imani yao, haiwezekani kuwarudisha hao watubu tena. Hao wanamsulubisha tena#6:4-6 Hao wanamsulubisha tena: Yaani, wanamkataa kwa makusudi kabisa Mwana wa Mungu. Mwandishi lakini anafikiri kwamba walengwa wake au wasomaji wake hawajafikia kiwango hicho cha mwisho (aya ya 9). Rejea Ebr 10:26-31. Mwana wa Mungu kwa makusudi na kumwaibisha hadharani.
7Ardhi ambayo huipokea mvua inayoinyeshea mara kwa mara na kuotesha mimea ya faida kwa mkulima imebarikiwa na Mungu. 8Ardhi ikiota miti ya miiba na magugu, haina faida; karibu italaaniwa na Mungu na mwisho wake ni kuchomwa moto.
9Ingawa twasema namna hii, wapenzi wetu, tuna uhakika wa kupewa mambo mema zaidi: yaani wokovu. 10Mungu hakosi haki; yeye hataisahau kazi mliyoifanya au upendo mliyoonesha kwa ajili yake katika huduma mliyowapa na mnayowapa sasa watu wake. 11Hamu yetu ni kwamba kila mmoja wenu aoneshe bidii hiyohiyo mpaka mwisho, ili yale mnayotumainia yapate kutimia. 12Hivyo msiwe wavivu, bali muwe kama wale wanaoamini na wenye uvumilivu, wakapokea yale aliyoahidi Mungu.
Ahadi ya Mungu ni ya kweli
13Mungu alipompa Abrahamu ahadi, aliapa kwa jina lake mwenyewe, maana hakuna aliye mkuu kuliko Mungu ambaye kwa huyo angeweza kuapa. 14Mungu alisema: “Hakika nitakubariki na nitakupa wazawa wengi.” 15Abrahamu alisubiri kwa uvumilivu na hivyo akapokea kile alichoahidiwa na Mungu. 16Watu wanapoapa, huapa kwa mmoja aliye mkuu kuliko wao, na kiapo husuluhisha ubishi wote. 17Naye Mungu aliimarisha ahadi yake kwa kiapo; na kwa namna hiyo akawaonesha wazi wale aliowaahidia kwamba hatabadili nia yake. 18Basi, kuna vitu hivi viwili: ahadi na kiapo, ambavyo haviwezi kubadilika na wala juu ya hivyo Mungu hawezi kusema uongo.#6:18 Mungu hawezi kusema uongo: Hes 23:19; 1Sam 15:29. Kwa hiyo sisi tuliokimbilia usalama kwake, tunapewa moyo wa kushikilia imara tumaini lililowekwa mbele yetu. 19Tunalo tumaini hilo kama nanga ya maisha yetu. Tumaini hilo lapenya mpaka mahali patakatifu mbinguni.#6:19 Lapenya mpaka mahali patakatifu mbinguni: Katika Lawi 16:2 yahusu lile hema la mkutano. Hapa, lakini kwa lugha ya mfano, yahusu hekalu la mbinguni ambamo Yesu aliingia akiwa Kuhani Mkuu na kwa kufanya hivyo akawapa watu uwezekano wa kumwendea Mungu (aya 20 Ebr 9:7). Tazama pia Mat 27:51. 20Yesu mwenyewe ametangulia kuingia humo kwa ajili yetu na amekuwa kuhani mkuu milele, kwa utaratibu wa ukuhani wa Melkisedeki.#6:20 Zab 110:4; taz Ebr 5:6 maelezo.