5
Wakufunzi wabaya wa Israeli
1“Haya! Sikilizeni enyi makuhani!
Tegeni sikio, enyi Waisraeli!
Sikilizeni enyi ukoo wa kifalme!
Nyinyi mlipaswa kuzingatia haki,
badala yake mmekuwa mtego huko Mizpa,#5:1 Mizpa: Jina hili laweza kuwa linataja mahali pa ibada karibu na Mto Yordani upande wa mashariki katika eneo la Gileadi (rejea Mwa 31:49; Amu 10:17; 11:11,29), au mahali pengine kaskazini mwa Yerusalemu (Amu 20:1-3; 21:1-8; 1Sam 7:5-6; 10:17).
mmekuwa wavu#5:1 Mtego …wavu: Taz Amo 3:5. Mtego wa ndege wa aina fulani. Wavu kawaida ulisambazwa njiani kunasa mawindo: hapa ni fumbo kwa wale wategao viongozi. Taz pia Yob 18:8-10; Zab 140:5; Meth 29:5; Omb 1:13. wa kuwanasa huko Tabori.#5:1 Tabori: Mlima maarufu uliokuwa upande wa kaskazini mashariki mwa Bonde la Yezreeli. Palikuwa pia mahali Ibada za Baali wa Tabor zilifanyiwa. (Taz pia Kumb 33:9; Amu 4:6,12). Palikuwa ni mahali pa chini kipindi cha waamuzi pia. Taz Amu 8:19; Yos 19:22; Zab 89:12; Jer 46:18.
2Mmechimba shimo refu la kuwanasa#5:2 Shimo refu la kuwanasa: Shimo lililochimbwa na kufunika kama mtego. Viongozi wa dini na serikali wamekuwa mtego kwa watu. Huwakamata na kuwafunga. huko Shitimu.#5:2 Shitimu: Yawezekana ni Abeli Shitimu. Ilikuwa katika upande wa mashariki mwa bonde la mdomo wa mlima Yordani. Pia hekalu la Baal-Peori (taz Hes 25:1; Yos 2:1; 3:1).
Lakini mimi nitawaadhibuni#5:2 Nitawaadhibuni: Kama mzazi amrudipo mtoto. (Taz Meth 1:8; 4:1; 13:1). Waisraeli walipovunja Agano waliadhibiwa (Kumb 11:2; ling Hos 11:1). Lengo la adhabu ni kuokoa (taz 2:6-7,14; 3:5). nyote.#5:2 Aya hii haina maana dhahiri katika makala ya Kiebrania.
3Nawajua watu wa Efraimu,
Waisraeli hawakufichika kwangu.
Nyinyi watu wa Efraimu mmefanya uzinzi,
watu wote wa Israeli wamejitia najisi.#5:3 Wamejitia najisi: Kwa kufanya uzinzi (taz 1:2; 4:11-14); ling 6:10. Taz pia Lawi 10 na Hos 4:4-10.
Hosea aonya dhidi ya ibada za miungu
4“Matendo yao yanawazuia wasimrudie Mungu wao.
Mioyoni mwao wamejaa uzinzi;
hawanijui mimi Mwenyezi-Mungu.
5Kiburi cha Waisraeli chaonekana wazi;
watu wa Efraimu watajikwaa katika hatia yao,
nao watu wa Yuda watajikwaa pamoja nao.
6Watakwenda na makundi yao ya kondoo na ng'ombe,#5:6 Kondoo na ng'ombe: Taz 4:8,13; Isa 1:11-15; ling 3:5 na 5:15; Amu 5:4. Atakataa matambiko yao na kuwaadhibu. Taz Hos 5:15; Meth 1:28. Ling Yoh 7:34. Mungu alihitaji kutolewa kwa moyo wa kweli sawa na Agano lake. Taz Amo 5:21-22, 6:56; Isa 1:10-17; Yer 7:21-26; pia Meth 21:3.
kumtafuta Mwenyezi-Mungu;
lakini hawataweza kumpata,
kwa sababu amejitenga nao.
7Wamevunja uaminifu#5:7 Wamevunja uaminifu: Taz maelezo ya 5:3. Pia 1:2; 2:4. Ling Yer 2:27; wamegeukia Mungu. kwa Mwenyezi-Mungu,
wamezaa watoto walio haramu.
Mwezi mwandamo#5:7 Mwezi mwandamo: Taz Zek 11:8. Kupatwa kwa mwezi: Hapa analinganisha maangamizi yasiyokwepeka yajayo punde si punde (kama mwezi mmoja hivi). Pia ilikuwa wakati wa sikukuu ya mavuno. Taz 2:11; Isa 20:5,18; Amu 8:5; Kol 2:16, hapa yaweza kumaanisha mavuno ya adhabu ya hukumu yatayotokea punde. utawaangamiza,
pamoja na mashamba yao.
Vita kati ya Yuda na Israeli
8“Pigeni baragumu huko Gibea,
na tarumbeta huko Rama.
Pigeni king'ora#5:8 Baragumu …tarumbeta … king'ora: Vifaa vilivyotumiwa kutoa sauti mbalimbali kuashiria vita. Taz pia Yer 4:5, 6:1; Yoe 2:1. Ling 8:1; Hes 10:2. huko Beth-aveni.
Enyi watu wa Benyamini, adui yenu yuko nyuma!#5:8 Adui yenu yuko nyuma: Taz Isa 10:29; Yuda; 2Fal 16:7-9. Gibea, Rama (taz Yos 18:21-26). Bethlehemu au Betheli (taz Yos 7:2). Hii ilikuwa miji ya Benyamini.
9Siku nitakapotoa adhabu
Efraimu itakuwa kama jangwa!
Ninachotangaza miongoni mwa makabila ya Israeli,
ni jambo litakalotukia kwa hakika.
10Viongozi wa Yuda wamekuwa
wenye kubadili mipaka#5:10 Kubadili mipaka: Taz Kumb 19:14, 27:17; Yobu 24:4; Meth 22:28; 23:10. Yuda kukiuka mipaka yao inalinganishwa na Israeli kuvunja agano lake na Mungu (taz 8:5, 3:11-14). Taz pia aya ya 8. ya ardhi.
Mimi nitawamwagia hasira yangu kama maji.
11 # 5:11 Aya hii maana yake sio dhahiri katika makala ya Kiebrania. Efraimu ameteswa,
haki zake zimetwaliwa;
kwani alipania kufuata upuuzi.#5:11 Alipania kufuata upuuzi: Taz 4:17; 5:3,13; 6:10; 7:11; 8:9-11; 12:2,7,8; 13:1.
12Hivyo mimi Mungu niko kama nondo kwa Efraimu,
kama donda baya#5:12 Nondo …donda baya: Vitu vyote hivi huonesha uharibifu. Taz pia Yobu 13:28; Zab 39:11; Isa 50:9. Nondo huharibu nguo. Donda baya huharibu mwili. Taz pia aya ya 11; Yuda 10; ling 6:1; 7:1. kwa watu wa Yuda.
13Watu wa Efraimu walipogundua ugonjwa wao,
naam, watu wa Yuda walipogundua donda lao,
watu wa Efraimu walikwenda Ashuru
kuomba msaada kwa mfalme mkuu;#5:13 Mfalme mkuu: Taz 3:4.
lakini yeye hakuweza kuwatibu,
hakuweza kuponya donda lenu.
14Maana mimi nitakuwa kama simba#5:14 Simba: Vinyago vya wanyama vilivyokuwa vinaabudiwa kama mungu katika Asia ndogo. Taz 13:4-8. kwa Efraimu,
kama mwanasimba kwa watu wa Yuda.
Mimi mwenyewe nitawararua na kuondoka,
nitawachukua na hakuna atakayewaokoa.
15Nitarudi mahali pangu#5:15 Mahali pangu: Waisraeli waliamini Mungu anakaa Mlimani Siyoni au hekaluni mwake. Taz Kumb 33 au Zab 18:6; 46:4. na kujitenga#5:15 Nitarudi mahali pangu na kujitenga: Mwenyezi-Mungu atawaacha mikononi mwa adui mpaka wajifunze kisha wamrudie. Taz 10:2; 14:1; ling Zab 63:1; 78:34, pia Amo 2:7,14; 3:5. nao
mpaka wakiri kosa lao na kunirudia.
Taabu zao zitawafundisha wanitafute, wakisema: