47
Tamko la Mwenyezi-Mungu juu ya Filistia#47:1-7 Ujumbe dhidi ya Filistia unapatikana pia katika maandishi mengine ya manabii: Isa 14:28-32; Eze 25:15-17; Yoe 3:4-8; Amo 1:6-8; Sef 2:4-7; Zek 9:5-7.
1Neno la Mwenyezi-Mungu lililomjia nabii Yeremia kuhusu Wafilisti, kabla Farao hajaushambulia mji wa Gaza:
2Mwenyezi-Mungu asema hivi:
“Tazama! Maji yanapanda kutoka kaskazini,
nayo yatakuwa mto uliofurika;
yataifunika nchi nzima na vyote vilivyomo,
mji na wakazi na wanaoishi humo.
Watu watalia,
wakazi wote wa nchi wataomboleza.
3Watasikia mshindo wa kwato za farasi,
kelele za magari ya vita,
na vishindo vya magurudumu yao.
Kina baba watawasahau watoto wao,
mikono yao itakuwa imelegea mno.
4Hiyo ni siku ya kuwaangamiza Wafilisti wote,
kukomesha msaada uliobakia kutoka Tiro na Sidoni.#47:4 Tiro na Sidoni: Miji ya Foinike. Inatajwa hapa labda kwa sababu wakazi wake walishirikiana na Wafilisti.
Maana Mwenyezi-Mungu anawaangamiza Wafilisti,
watu waliosalia wa kisiwa cha Kaftori.
5Watu wa Gaza wamenyoa upara kuomboleza;
mji wa Ashkeloni#47:5 Ashkeloni: Mojawapo ya miji mitano ya Filistia; miji mingine ikiwa Gaza, Ashdodi, Gadi na Ekroni. Taz maelezo ya Yos 11:22. “Watu wa Anakimu”: Rejea Yos 11:22 na Taz Hes 13:33 maelezo. umeangamia.
Enyi watu wa Anakimu mliobaki
mpaka lini mtajikatakata kwa huzuni?
6Ee upanga wa Mwenyezi-Mungu!
Utachukua muda gani ndipo utulie?
Ingia katika ala yako,
ukatulie na kunyamaa!
7Lakini utawezaje kutulia,
hali Mwenyezi-Mungu ameupa kazi?
Ameuamuru ushambulie mji wa Ashkeloni
na watu wanaoishi pwani.”