Yobu 25
BHNTLK

Yobu 25

25
Jibu la Bildadi#25:1-6 Hii ni hoja ya tatu ya Bildadi (rejea 8:1-22; 18:1-21; na ya nne: 26:5-14). Katika hoja hii yake, Bildadi anakazia juu ya ukuu wake Mungu ambao mbele yake hakuna binadamu anayeweza kuwa bila hatia.
1Kisha Bildadi, Mshuhi, akajibu:
2“Mungu ni mwenye uwezo mkuu,
watu wote na wamche.
Yeye huweka amani mpaka juu kwake mbinguni.
3Nani awezaye kuhesabu majeshi yake?
Ni nani asiyeangaziwa na mwanga wake?
4Mtu awezaje basi, kuwa mwadilifu mbele ya Mungu?
Binadamu tu awezaje kujidai kuwa safi?
5Kwake Mungu, hata mwezi haung'ai vya kutosha;
nyota nazo si safi mbele yake;
6sembuse mtu ambaye ni mdudu,
binadamu ambaye ni buu tu!”

Copyright The Bible Society of Tanzania, 1993

The Bible Society of Kenya 1993

Learn More About Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza