3
Adhabu, toba na tumaini#3:1-66 Mimi ni mtu …mateso …: Anayehusika katika matumizi ya maneno “mimi…” anaweza kuwa huyo mwandishi mwenyewe au yeye akiwakilisha jumuiya yote ya wanaoomboleza maafa hayo kama inavyoonekana katika 3:33,40-45. Ombolezo hili lina mtindo wa kawaida kuhusu theolojia yake, yaani ingawa Mungu huwaadhibu watu yeye ni mwenye huruma pia na hatawaacha watu wake kabisa; kama wakitubu na kuungama dhambi zao yeye atawarekebisha tena. Mwishoni mshairi huyu anaomba kwamba Mungu ataadhibu maadui za watu wake (3:64-66).
1Mimi ni mtu niliyepata mateso
kwa fimbo ya ghadhabu yake Mungu.
2Amenichukua akanipeleka
mpaka gizani kusiko na mwanga.
3Amenyosha mkono wake dhidi yangu mimi tu,
akanichapa tena na tena mchana kutwa.
4Amenichakaza ngozi na nyama,
mifupa yangu ameivunja.
5Amenizingira na kunizungushia
uchungu na mateso.
6Amenikalisha gizani
kama watu waliokufa zamani.
7Amenizungushia ukuta nisitoroke,
amenifunga kwa minyororo mizito.#3:5-7 Kama vile katika Zab 107:10-14 maneno ya aya hizi yanamwonesha mshairi kama yupo kifungoni na picha ya hicho kifungo ni ile ya kuzimu (Zab 88:6,12,18; 14:3).
8Ingawa naita na kulilia msaada
anaizuia sala yangu isimfikie.
9Njia zangu ameziziba kwa mawe makubwa
amevipotosha vichochoro vyangu.
10Yeye ni kama dubu anayenivizia;
ni kama simba#3:10 Dubu …simba: Mungu analinganishwa na mnyama anayeotea kwa uvumilivu mawindo yatokee na kushambulia vikali. aliyejificha.
11Alinifukuza njiani mwangu,
akanilemaza na kuniacha mkiwa.
12Aliuvuta upinde wake,
akanilenga mshale wake.
13Alinichoma moyoni kwa mishale,
kutoka katika podo lake.
14Nimekuwa kitu cha dhihaka kwa watu wote,
mchana kutwa nimekuwa mtu wa kuzomewa.
15Amenijaza taabu,
akanishibisha uchungu.#3:15 Uchungu: Tafsiri nyingine “pakanga” neno ambalo linatumiwa hapa kama mfano kuonesha maafa makubwa sana au masikitiko (Taz Aya ya 19; Yer 9:15; 23:15).
16Amenisagisha meno katika mawe,
akanifanya nigaegae majivuni.
17Moyo wangu haujui tena amani,
kwangu furaha ni kitu kigeni.
18Nimewaza “Nimekata tamaa kabisa,
tumaini langu kwa Mwenyezi-Mungu limetoweka.”
19Kukumbuka taabu na kutangatanga kwangu
kwanipa uchungu kama wa nyongo.
20Nayafikiria hayo daima,
nayo roho yangu imejaa majonzi.
21Lakini nakumbuka jambo hili moja,
nami ninalo tumaini:#3:21 Baada ya mshairi huyu kumaliza kueleza mateso yanayomkabilia katika aya 1-20 anaweza sasa kutaja kitu ambacho kinamjaza matumaini rohoni (3:21-24). Jambo hili linatokana na tumaini lake kwa Mungu na anaweza pia kuwatangazia wengine wanaokumbwa na mateso hayo (3:25-40).
22Kwamba fadhili za Mwenyezi-Mungu hazikomi,
huruma zake hazina mwisho.#3:22-23 Huruma zake hazina mwisho: Ingawa katika aya 22b “huruma” inaendana na “fadhili” katika 22a inafaa kutaja kwamba neno huruma au “rehema” (Kiebrania “raham”) ni neno lile lile linalotumiwa kutaja tumbo la mama la uzazi ambamo kitoto kichanga hutulia kwa raha mustarehe, mahali ambamo mtoto hupata uhai mpya na ulinzi. Hiyo ndiyo picha inayotumiwa kwa Mungu mahali pengi katika Zaburi; taz k.m. Zab 78:38; 86:15; 111:4; 145:8.
23Kila kunapokucha ni mpya kabisa,
uaminifu wake ni mkuu mno.
24Mwenyezi-Mungu ndiye hazina yangu#3:24 Hazina yangu: Tafsiri ya neno la Kiebrania ambalo laweza kutafsiriwa kwa namna nyingi zinazofanana. Wazo muhimu hapa ni kwamba mshairi anamwona Mwenyezi-Mungu kuwa ndiye tu anayemhitaji katika maisha. Tafsiri nyingine ni “hazina kuu”, n.k.
hivyo nitamwekea tumaini langu.
25Mwenyezi-Mungu ni mwema kwa wanaomtegemea,
ni mwema kwa wote wanaomtafuta.
26Ni vema mtu kungojea kwa saburi
ukombozi utokao kwa Mwenyezi-Mungu.
27Ni vema mtu kujifunza uvumilivu
tangu wakati wa ujana wake.#3:27-30 Aya hizi kwa lugha ya hekima zinaelezea faida ya kuwa mvumilivu na mwishoni mshairi anatamka tumaini lake kwamba Mungu hataendelea kuwakasirikia watu wake milele.
28Heri kukaa peke na kimya,
mazito yanapompata kutoka kwa Mungu.
29Yampasa kuinama na kujinyenyekesha,
huenda ikawa tumaini bado lipo.
30Yampasa kumgeuzia shavu mwenye kumpiga,
na kuwa tayari kupokea matusi yake.
31Mwenyezi-Mungu hatatutupa milele.
32Ingawa atufanya tuhuzunike,
atakuwa na huruma tena
kadiri ya wingi wa fadhili zake.
33Yeye hapendelei kuwatesa
wala kuwahuzunisha wanadamu.
34Wafungwa wote nchini
wanapodhulumiwa na kupondwa;
35haki za binadamu zinapopotoshwa
mbele yake Mungu Mkuu,
36kesi ya mtu inapopotoshwa mahakamani,
je, Mwenyezi-Mungu haoni hayo?
37Nani awezaye kuamuru kitu kifanyike
Mwenyezi-Mungu asipopanga iwe hivyo?
38Maafa na mema hutokea tu
kwa amri yake Mungu Mkuu.#3:38 Kwamba huleta mema na mabaya taz Isa 45:7; Amo 3:6.
39Kwa nini mtu anung'unike,
ikiwa ameadhibiwa kwa dhambi zake?
40Na tupime na kuchunguza mwenendo wetu,
tupate kumrudia Mwenyezi-Mungu.#3:40-41 Kujichunguza na kujipima moyoni kunaweza kumwezesha mtu kutubu na hivyo kumrudia Mwenyezi-Mungu.
41Tumfungulie Mungu huko mbinguni
mioyo yetu na kumwomba:
42“Sisi tulikukosea na kukuasi
nawe bado hujatusamehe.
43“Umejizungushia hasira yako ukatufuatia,
ukatuua bila huruma.
44Umejizungushia wingu zito,
sala yeyote isiweze kupenya humo.
45Umetufanya kuwa takataka na uchafu
miongoni mwa watu wa mataifa.
46“Maadui zetu wote wanatuzomea.
47Kitisho na hofu vimetuandama,
tumepatwa na maafa na maangamizi.
48Macho yangu yabubujika mito ya machozi
kwa sababu ya kuangamizwa kwa watu wangu.
49“Machozi yatanitoka bila kikomo,
50mpaka Mwenyezi-Mungu kutoka huko mbinguni
aangalie chini na kuona.
51Nalia na kujaa majonzi,
kuona yaliyowapata kina mama wa mji wangu.
52“Nimewindwa kama ndege#3:52 Nimewindwa kama ndege: Taz maneno kama hayo ambayo ni picha ya kifo katika 3:54-55. Taz pia Zab 69:1-2; 88:16-19; Yona 2:2-3.
na hao wanichukiao bila sababu.
53Walinitupa shimoni nikiwa hai
na juu yangu wakarundika mawe.
54Maji yalianza kunifunika kichwa,
nami nikafikiri, ‘Huu ni mwisho wangu.’
55“Kutoka chini shimoni
nilikulilia ee Mwenyezi-Mungu.
56Wewe umenisikia nikikulilia:
‘Usiache kusikia kilio changu cha msaada
bali unipatie nafuu.’
57Nilipokuita ulinijia karibu
ukaniambia, ‘Usiogope!’#3:57 Usiogope!: Zab 69:18; Isa 58:9; Yak 4:8
58“Umenitetea katika kisa changu ee Mwenyezi-Mungu,
umeyakomboa maisha yangu.
59Umeuona uovu niliotendewa ee Mwenyezi-Mungu,
uniamulie kwa wema kisa changu.
60Umeuona uovu wa maadui zangu,
na mipango yao yote ya hila dhidi yangu.
61“Umesikia matukano yao ee Mwenyezi-Mungu,
na mipango yao yote ya hila dhidi yangu.
62Maneno na mawazo ya maadui zangu siku nzima
ni juu ya kuniangamiza mimi.
63Wakati wote, wamekaa au wanakwenda,
mimi ndiye wanayemzomea.
64Uwalipize, ee Mwenyezi-Mungu
kadiri ya hayo matendo#3:64 Uwalipize …kadiri ya hayo matendo: Mwandishi anataja matumaini yake kwamba Mungu atawaadhibu pia maadui za watu wa Yuda, fikira ambazo hujitokeza pia mara kwa mara katika Zaburi k.m. Zab 3:7; 17:13; 35:26; 59:10-13). Taz pia Yer 11:20; 18:19-23. yao,
kadiri ya mambo waliyotenda wenyewe.
65Uipumbaze mioyo yao,
na laana yako iwashukie.
66Uwafuatie kwa hasira, uwaangamize,
uwafanye watoweke ulimwenguni.”