Mathayo 3
BHNTLK

Mathayo 3

3
Mahubiri ya Yohane Mbatizaji
(Marko 1:1-8; Luka 3:1-18; Yoh 1:19-28)
1 # 3:1 Injili zote nne zinaafikiana kwa jumla juu ya kuhusisha mwanzo wa kazi yake Yesu na mahubiri ya Yohane Mbatizaji (rejea Marko 1:1-14; Luka 3:1-22; Yoh 1:19-36). Yohane Mbatizaji ni mjumbe yule aliyetangazwa na nabii Isaya (3:3); anatajwa kuwa mkuu kuliko watumishi wote wa Mungu wa hapo awali (11:7-11); anatajwa pia kuwa Elia ambaye angefika siku ile ya mwisho ya hukumu (Mal 3:1; 4:5; Mat 11:13-14; 17:10-13). Siku zile#3:1 Siku hizo: Yapata mwaka 27 B.K. karibu miaka 30 tangu matukio ya sura ya pili (Luka 3:1-3). Yohane Mbatizaji alitokea, akaanza kuhubiri katika jangwa la Yudea:#3:1 Jangwa la Yudea: Sehemu iliyokaliwa na watu wachache sana; sehemu yenyewe ilikuwa kusini mwa Yerusalemu kuelekea mji Hebroni hadi Bahari ya Chumvi. 2“Tubuni,#3:2 Tubuni: Neno lenyewe ni tafsiri ya neno la Kigiriki “metanoite” nalo lina maana ya kubadilisha mwenendo mbaya, kuacha maisha mabaya na kuishi maisha mema. Neno la kawaida lililotumika katika Kiebrania kuelezea jambo hilo ni “shub”, nalo lamaanisha “kurudi”, yaani kumrudia Mungu. maana ufalme wa mbinguni#3:2 Ufalme wa mbinguni: Kufuatana na desturi ya Wayahudi ya kutotamka jina la Mungu, Mathayo anapendelea kusema “Ufalme wa mbinguni” badala ya “Ufalme wa Mungu” maneno ambayo yanatumiwa na wale waandishi wengine wa Injili. Ufalme wa mbinguni wa Mungu, ni utawala wa Mungu kati ya watu. umekaribia.” 3Huyu Yohane ndiye yule ambaye nabii Isaya alinena juu yake aliposema:
“Sauti ya mtu anaita jangwani:
‘Mtayarishieni Bwana njia#3:3 Mtayarishieni Bwana Njia …: Taz Isa 40:3 sehemu ambayo imedondolewa hapa kufuatana na makala ya kale ya Kigiriki ya Septuajinta (LXX). yake,
nyosheni barabara zake.’”
4Yohane alivaa vazi lililoshonwa kwa manyoya ya ngamia, na ukanda wa ngozi kiunoni mwake. Chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwituni. 5Basi, watu kutoka Yerusalemu, kutoka pande zote za Yudea na sehemu zote za kandokando ya mto Yordani, walimwendea, 6wakaziungama dhambi zao, naye akawabatiza#3:6 Akawabatiza: Ibada yenyewe ya kutumia maji ilikuwa ishara ya kutakaswa rohoni na kujiweka tayari kwa hukumu ya Mungu. katika mto Yordani.
7Lakini alipowaona Mafarisayo wengi na Masadukayo#3:7 Mafarisayo na Masadukayo: “Mafarisayo” walikuwa kikundi cha Wayahudi ambao walisisitiza sana kuzingatia sheria na mapokeo ya Wayahudi mara nyingine kwa unafiki. “Masadukayo” kwa upande mwingine walikuwa zaidi hasa wanasiasa na walihitilafiana na Mafarisayo kwa vile walikana kuweko ufufuo wa wafu, roho na malaika (taz Mate 23:8). wanamjia ili awabatize, aliwaambia, “Enyi kizazi cha nyoka!#3:7 Kizazi cha nyoka: Msemo wa kukaripia, sawa na kusema kwa mfano: “wajeuri wabaya kama nyoka”. Ni nani aliyewadokezea muikimbie ghadhabu#3:7 Ghadhabu (ya Mungu): Hapa inamaanisha “hukumu”. inayokuja? 8Onesheni kwa vitendo kwamba mmetubu. 9Msifikiri na kujisemea, ‘Baba yetu ni Abrahamu!’#3:9 Baba yetu ni Abrahamu: Ling na Yoh 8:33-39. Waisraeli walifikiri kwamba kule kuwa na Abrahamu kama mzee wao kwa nasaba kuliwafanya wawe watu wa Mungu, lakini nasaba ya kiroho ndilo jambo muhimu zaidi (Rom 9:6-8; Gal 3:9). Nawaambieni hakika, Mungu anaweza kuyafanya mawe haya yawe watoto wa Abrahamu. 10Basi, shoka liko tayari kwenye mizizi ya miti; hivyo, kila mti usiozaa matunda mazuri utakatwa na kutupwa motoni. 11Mimi ninawabatizeni kwa maji kuonesha mmetubu. Lakini anayekuja baada yangu ana nguvu kuliko mimi, nami sistahili hata kubeba viatu vyake. Yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.#3:11 Kwa Roho Mtakatifu na kwa moto: “Roho Mtakatifu” ni zawadi ya Mungu kwa watu wake (Yoe 2:28-29; Mate 2:16-18); “moto” watumika hapa kama ishara ya adhabu na uteketezaji wa wakosefu wasiotubu (18:9). 12Yeye anashika mkononi chombo cha kupuria nafaka,#3:12 Chombo cha kupuria nafaka: Aya yenyewe ina lengo la kuonesha “hukumu”; (taz Isa 17:5; Yer 13:24; Amosi 4:12-13). ili aipure nafaka yake; akusanye ngano yake ghalani, na makapi ayachome kwa moto usiozimika.”
Yesu anabatizwa
(Marko 1:9-11; Luka 3:21-22)
13Wakati huo Yesu alitoka Galilaya akafika katika mto Yordani, akamwendea Yohane ili abatizwe naye. 14Lakini Yohane alijaribu kumzuia akisema, “Je, wewe unakuja kwangu? Mimi hasa ndiye ninayehitaji kubatizwa nawe.” 15Lakini Yesu akamjibu, “Acha tu iwe hivyo kwa sasa, maana ndivyo inavyofaa tuyatekeleze yale yote Mungu anayotaka.”#3:15 Yote Mungu anayotaka: Au, “uadilifu wote” (rejea Mat 5:6,10,20; 6:33). Hapo Yohane akakubali.
16Mara tu Yesu alipokwisha batizwa, alitoka majini; na kumbe mbingu zikafunguka, akaona Roho wa Mungu akishuka kama njiwa na kutua juu yake. 17Sauti kutoka mbinguni ikasema, “Huyu ndiye Mwanangu mpendwa,#3:17 Huyu ndiye mwanangu mpendwa …: Inawezekana pia kuelewa maneno hayo kwa maana ya “Mwanangu wa pekee”. Ling na Zab 2:7; Isa 42:1. Maneno hayo kutoka mbinguni yanamdhihirisha Yesu kuwa Mtumishi wa Mungu (Isa 42:1; 52:13-53:12 ambapo yahusu Mtumishi wa Mwenyezi-Mungu anayeteseka), Mwana wa pekee wa Mungu (Zab 2:7; ling Mwa 22:2). Taz pia Mat 12:18; 17:5; Marko 1:11. nimependezwa naye.”

Copyright The Bible Society of Tanzania, 1993

The Bible Society of Kenya 1993

Learn More About Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza