24
1Sasa Balaamu alitambua kwamba Mwenyezi-Mungu alipenda kuwabariki Waisraeli, kwa hiyo hakwenda kupiga bao tena,#24:1 Hakwenda kupiga bao tena: Taz Hes 22:7-8 maelezo. Lakini si yamkini hata kidogo kwamba Balaamu alitumia uchawi wakati alipopata ujumbe wa Mwenyezi-Mungu mara mbili. akawa anaangalia jangwani.#24:1 Jangwani: Yaani jangwa lililoko kaskazini mwa Bahari ya Chumvi, upande wa mashariki wa Mto Yordani (taz 23:28). 2Alitazama juu akawaona Waisraeli wamepiga kambi, kila kabila mahali pake. Kisha roho ya Mungu ikamjia,#24:2 Roho ya Mungu ikamjia: Taz 11:25 maelezo. 3naye akatamka kauli hii ya kinabii:
Kauli yangu mimi Balaamu mwana wa Peori
kauli ya mtu aliyefumbuliwa#24:3 Aliyefumbuliwa: Au: “aonaye vema”, au: “aliyefumbwa macho”. Kwa maana hii ya pili huenda mwandishi alitaka kusema kwamba Balaamu alikuwa katika hali ya maono au njozi. macho;
4kauli ya mtu aliyesikia maneno ya Mungu
mtu aliyeona maono ya Mungu Mwenye Nguvu,#24:4 Mungu Mwenye Nguvu: Mojawapo ya majina ya Mungu ya sifa. Taz orodha ya majina ya Mungu pale baada ya Kut 3:14.
mtu anayesujudu na kuona wazi.
5Hema zako zapendeza namna gani enyi watu wa Yakobo;
naam, kambi zenu enyi watu wa Israeli!
6Ni kama mabonde yanayotiririka maji,
kama bustani kandokando ya mto,
kama mishubiri#24:6 Mishubiri: Neno ambalo linatafsiri namna ya mti ambao utomvu wa maganda yake ulithaminiwa kwa harufu yake nzuri. aliyopanda Mwenyezi-Mungu,
kama mierezi kandokando ya maji.
7Watakuwa na hazina ya kutosha ya maji,#24:7 Watakuwa …hazina ya kutosha ya maji: Makala nyingine ya Kiebrania: “maji yatiririka kutoka ndoo zake …”
mbegu yao itapata maji mengi,
mfalme wao atakuwa mkuu kuliko Agagi,#24:7 Agagi: Huyu alikuwa mfalme mwenye nguvu zaidi kati ya wafalme wa Waamaleki (taz 13:29 maelezo).
na ufalme wake utatukuka sana.
8Mungu aliwachukua kutoka Misri,
naye huwapigania kwa nguvu kama nyati.
Atayateketeza mataifa yaliyo adui zao,
atavunjavunja mifupa yao,
atawachoma kwa mishale yake.
9Ataotea na kulala chini kama simba,
nani atathubutu kumwamsha?
Abarikiwe yeyote atakayewabariki nyinyi Waisraeli,#24:9 Maneno ya mwisho ya Balaamu yanarudia ahadi ya Mungu ambayo inatajwa katika Mwa 12:3.
alaaniwe yeyote atakayewalaani.
10Balaki akawaka hasira dhidi ya Balaamu, akakunja mikono kwa ghadhabu na kumwambia, “Nilikuita uwalaani adui zangu, lakini mara hizi zote tatu umewabariki! 11Sasa! Nenda zako. Nilikuwa nimekuahidi kukupa zawadi nyingi, lakini Mwenyezi-Mungu hakukujalia kupata zawadi hizo, amekunyima!”
12Balaamu akamjibu Balaki, “Je, sikuwaambia wajumbe uliowatuma kwangu 13kwamba hata kama ungenipa nyumba yako imejaa fedha na dhahabu, mimi sitaweza kukiuka agizo la Mwenyezi-Mungu, kwa kufanya jambo lolote, jema au baya kwa hiari yangu mwenyewe? Nilisema, atakachosema Mwenyezi-Mungu ndicho nitakachokisema.
14“Sasa ninarudi kwa watu wangu, lakini kabla sijaondoka, acha nikuambie mambo ambayo watu hao watawatendea watu wako siku zijazo.” 15Basi, Balaamu akatamka kauli hii:
“Kauli yangu mimi Balaamu mwana wa Beori,
kauli ya mtu aliyefumbuliwa macho,
16kauli ya mtu aliyesikia maneno ya Mungu,
na mtu ajuaye maarifa ya Mungu Mkuu,
mtu aonaye maono ya Mungu Mwenye Nguvu,
mtu anayesujudu, macho wazi.#24:16 Katika aya hii majina mawili ya Mungu ya sifa yanatumiwa. “Mungu Mkuu” ni tafsiri ya maneno ya Kiebrania “El Elyon” na “Mungu Mwenye Nguvu” ni tafsiri ya neno la Kiebrania “Shadday”. Taz orodha ya majina ya Mungu pale baada ya Kut 3:14.
17Ninamwona, atakayekuja, lakini baadaye,
namwona, lakini hayuko karibu.
Nyota itatokea kwa wazawa wa Yakobo,
atatokea mfalme miongoni mwa Waisraeli.
Kwa fimbo yake atawachapa viongozi wa Wamoabu
atawaangamiza wazawa wote wa Sethi.#24:17-19 Sehemu hii inadokezea ushindi juu ya Wamoabu. Miaka mingi baadaye, mfalme Daudi aliwashinda Wamoabu na Waedomu (2Sam 8:2,13-14).
18Edomu#24:18 Edomu: Taz 20:14 maelezo. itamilikiwa naye,
Seiri#24:18 Seiri: Hili ni jina lingine la Edomu. itakuwa mali yake,
Israeli itapata ushindi mkubwa.
19Mmoja wa wazawa wa Yakobo atatawala
naye atawaangamiza watakaonusurika wa Ari.”
20Kisha Balaamu akawaangalia Waamaleki, akatoa kauli hii:
“Amaleki ni taifa lenye nguvu kuliko yote,
lakini mwishoni litaangamia kabisa.”
21Kisha Balaamu akawaangalia Wakeni, akatoa kauli hii:
“Makao yenu ni salama, enyi Wakeni,
kama kiota juu kabisa mwambani.
22Lakini mtateketezwa, enyi Wakeni.
Mtachukuliwa mateka na Ashuru#24:21-22 Wakeni …Ashuru: Makala ya Kiebrania ya aya hizi ni ngumu na tafsiri yake si dhahiri. “Wakeni” walikuwa watu wa kabila la Wakanaani ambao waliishi eneo la kusini la nchi ya Israeli (taz Mwa 15:19). Inasemekana kuwa wao walikuwa wazawa wa shemejiye Mose, yaani Hobabu mwana wa Reueli (au kwa jina lingine, Yethro). Waashuru walikuwa taifa lenye nguvu sana nyakati za Biblia. Lakini hatuna kumbukumbu yoyote nyingine kwamba Waashuru walipata kuwashinda Wakeni. mpaka lini?”
23Tena Balaamu akatoa kauli hii:
“Lo! Nani ataishi, Mungu atakapofanya hayo?
24Meli zitafika kutoka Kitimu,
wataishambulia Ashuru na Eberi,#24:24 Kitimu …Ashuru na Eberi: Baadhi ya wataalamu wa mambo ya Biblia wanafikiri Kitimu hapa ni sawa na kisiwa cha Kupro katika Bahari ya Mediteranea (taz Yer 2:10). Na kuhusu “Eberi” huenda inahusu nchi huko Mesopotamia. Katika Mwa 10:21-31 “Eberi” anatajwa kama mmojawapo wa mababu wa Waisraeli.
lakini nao pia wataangamia milele.”
25Basi, Balaamu akaondoka, akarudi nyumbani; Balaki pia akaenda zake.