Methali 10
BHNTLK

Methali 10

10
Methali za Solomoni#10:1 Methali za Solomoni: Taz 1:1 maelezo.
1Hizi ni methali za Solomoni:
Mtoto mwenye hekima ni furaha ya baba yake;
lakini mtoto mpumbavu ni huzuni ya mama yake.#10:1—29:27 Sehemu hii kubwa ya kitabu cha Methali inajulikana kama methali za Solomoni. Nyingi ya methali za sura 10—15 zina muundo wa mistari sambamba, mstari wa pili wa kila aya ukiwa kwa namna moja au nyingine sambamba na mstari wa kwanza. Methali za sura 16:1—22:16 zina mtindo wa sambamba pia lakini mstari wa pili wa kila aya kwa jumla huendeleza wazo la mstari wa kwanza. Methali nyingi zaidi zinahusu maisha adili, zinasifu fadhila, uaminifu, utaratibu wema na ukweli na kulaani uvivu, uongo, ujinga na dhambi. Methali nyingine kama inavyotazamiwa katika maandishi ya namna hii ni ngumu; tena pengine uhusiano kati ya mistari ya aya nyingine huwa si dhahiri.
2Mali iliyopatikana kwa njia mbaya haifai,
lakini uadilifu huokoa mtu kutoka kifoni.
3Mwenyezi-Mungu hawaachi waadilifu wapate njaa,
lakini huzipinga tamaa za waovu.
4Uvivu husababisha umaskini,#10:4-5 Uvivu husababisha umaskini …: Methali nyingi zinakemea na kulaani uvivu. Taz k.m., 6:6-11; 12:11-27; 13:4; 28:19.
lakini mkono wa mtu wa bidii hutajirisha.
5Mwenye busara hukusanya wakati wa mavuno,
kulala wakati wa kuvuna ni aibu.#10:5 … kulala wakati wa kuvuna ni aibu: Mkulima ataelewa vizuri zaidi maana ya methali hii: kuchelewa kuvuna wakati wake kunaweza kusababisha hasara kubwa kama vile kuoza kwa mavuno, n.k.
6Mwadilifu hujiletea baraka yeye mwenyewe,
lakini kinywa cha mwovu kimesongwa na ukatili.
7Waadilifu hukumbukwa kwa baraka,
lakini waovu watasahaulika kabisa.
8Mwenye hekima moyoni hutii amri,
lakini mpumbavu aropokaye ataangamia.
9Aishiye kwa unyofu huishi salama,
apotoshaye maisha yake atagunduliwa.
10Akonyezaye kwa nia mbaya#10:10 Akonyezaye kwa nia mbaya: Tafsiri hii imejaribu kuleta maana ya msemo ambao si dhahiri. Kitendo kinachotajwa katika mstari wa kwanza kina shabaha hasa ya kudanganya au kuzuia ukweli usijulikane (kama vile katika 6:13). Na mstari wa pili unafuata tafsiri moja ya kale ya Kiebrania, hali makala ya Kiebrania inarudia 10:8b, yaani: “mpumbavu aropokaye, ataangamia”. huzusha taabu,
lakini aonyaye kwa ujasiri huleta amani.
11Kinywa cha mwadilifu ni chemchemi ya uhai,
lakini kinywa cha mwovu kimesongwa na ukatili.
12Chuki huzusha ugomvi,
lakini upendo hufunika makosa yote.#10:12 … upendo hufunika makosa yote: Kuhusu msemo huu taz pia Yak 5:20; na 1Pet 4:8.
13Kinywani mwa mwenye ufahamu mna hekima,
lakini wasio na akili watachapwa viboko mgongoni.
14Wenye hekima huhifadhi maarifa,
lakini kuropoka kwa mpumbavu#10:8-14 Mpumbavu aropokaye …kuropoka kwa mpumbavu: Aya hizi zinasema juu ya kuropokaropoka kwa mpumbavu. Maneno anayosema mtu huwa yana nguvu ya kusababisha mema au mabaya. Maneno mema yanayotamkwa kwa hekima hufaa lakini maneno maovu humfanya anayeyasema aadhibiwe (10:13). Taz pia Mhub 10:12-14. huleta maangamizi haraka.
15Mali ya tajiri ndio ngome yake,
umaskini wa maskini humletea maangamizi.#10:15 Mali ya tajiri …ngome yake, umaskini wa maskini … maangamizi Msemo huu ni mgumu. Tajiri anajiona kuwa salama kwa mali yake ingawa si kila mara ni kweli. Lakini maskini naye anasemwa kuwa umaskini wake utamwangamiza. Hili nalo hutokea. Mwanamethali hapa anatamka bila kufafanua zaidi; anasema tu inavyoonekana kwa macho. Katika Meth 28:11, matajiri watatambua kwamba usalama wao wa mali na fedha ni ndoto ya kupita (11:4,28; 18:10-11; 23:4-5). Mwenyezi-Mungu ndiye peke yake aliye usalama kamili (3:5-6).
16Tuzo la mtu mwema ni uhai,
lakini mwovu huishia katika dhambi.
17Anayekubali maonyo anaelekea kwenye uhai,
lakini anayekataa kuonywa amepotoka.
18Amchukiaye mwingine kwa siri ni mnafiki,
anayemsingizia mtu ni mpumbavu.
19Penye maneno mengi hapakosekani makosa,
lakini aneyeuzuia ulimi wake ana busara.
20Maneno ya mwadilifu ni kama fedha bora;
akili ya mtu mwovu haina thamani yoyote.
21Maneno ya mwadilifu huwafaa watu wengi,
lakini wapumbavu hufa kwa kukosa akili.
22Baraka za Mwenyezi-Mungu ndizo ziletazo fanaka,
juhudi za mtu haziongezi hapo chochote.#10:22 Juhudi …chochote: Tafsiri yamkini kwa maana inayotolewa pia katika Zab 127:1-2. Kiebrania kina neno kwa neno ni “hachanganyi huzuni nayo”.
23Kwa mpumbavu kutenda maovu ni kama mchezo;
lakini watu wenye busara hufurahia hekima.
24Anachoogopa mtu mwovu ndicho kitakachompata,
lakini anachotamani mwadilifu ndicho atakachopewa.
25Kimbunga hupita na mwovu hutoweka,
lakini mwadilifu huimarishwa milele.
26Kama ilivyo siki kwa meno au moshi machoni,
ndivyo alivyo mvivu kwa bwana wake.
27Kumcha Mwenyezi-Mungu hurefusha maisha,
lakini miaka ya waovu itakuwa mifupi.#10:27 Ugumu wa aya hii ni kwamba mara nyingine watu wema hufariki hata kabla ya kuwa wazee, hali watu wabaya huwa na maisha marefu ingawa hatima ya hao waovu ni maangamizi.
28Tumaini la mwadilifu huishia kwenye furaha,
lakini tazamio la mwovu huishia patupu.
29Mwenyezi-Mungu ni ngome ya wanyofu,
lakini watendao maovu atawaangamiza.
30Waadilifu kamwe hawataondolewa nchini,
lakini waovu hawatakaa katika nchi.
31Kinywa cha mwadilifu hutoa mambo ya hekima,
lakini ulimi wa mtu mbaya utakatiliwa mbali.
32Midomo ya waadilifu hujua yanayokubalika,
lakini vinywa vya waovu husema tu maovu.

Copyright The Bible Society of Tanzania, 1993

The Bible Society of Kenya 1993

Learn More About Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza