Methali 17
BHNTLK

Methali 17

17
1Afadhali mkate mkavu kwa amani,
kuliko karamu katika nyumba ya ugomvi.
2Mtumwa mwenye busara atachukua nafasi ya mwana mpumbavu,
atapata sehemu ya urithi wa jamaa#17:2 Mtumwa mwenye busara atachukua …urithi wa jamaa: Sheria ya Waisraeli haikutoa nafasi ya mtumwa kurithi mali, lakini mtumwa mwangalifu aliweza kutendewa vizuri kuliko mtoto wa nyumbani. hiyo.
3Ubora wa dhahabu ama fedha hupimwa kwa moto,#17:3 Dhahabu …hupimwa kwa moto: Madini kama vile dhahabu kwa kawaida huwekwa katika tanuri ili kuondoa chochote kisicho dhahabu (rejea Meth 27:21; Sira 2:5). Mtunzi wa methali anachukua kitendo hicho kuelezea anavyofanya Mungu anapoyapima mawazo ya watu wake. Picha hiyo ni ya kawaida katika maandishi ya manabii (rejea Yer 9:6-7; 11:20; 12:3; 17:10; Zek 13:9). Rejea pia Eze 22:18-22; 1Pet 1:7:25.
lakini Mwenyezi-Mungu ndiye apimaye mioyo ya watu.
4Mtenda maovu husikiliza maneno mabaya,
mwongo hutegea sikio ulimi mdanganyifu.
5Anayemdhihaki maskini anamtukana Muumba wake;#17:5 Anayemdhihaki maskini anamtukana Muumba wake: Taz 14:31 maelezo.
anayefurahia maafa hatakosa kuadhibiwa.
6Wazee huwaonea fahari wajukuu zao;
watoto huwaonea fahari wazazi wao.
7Maneno mazuri si kawaida kinywani mwa mpumbavu,
sembuse maneno ya uongo kinywani mwa kiongozi!
8Kwa mhongaji, hongo ni kama hirizi;
kila afanyacho hufanikiwa.#17:8 Mhongaji, hongo …hufanikiwa: Lengo la methali hii sio kuhalalisha utoaji wa hongo (jambo hilo linalaaniwa mahali pengi katika Biblia k.m. Meth 17:23; Kut 23:8; Kumb 16:19 n.k.) bali inaonesha kwamba kitendo hicho kilichofanyika mara nyingi kilifanikiwa. Taz pia 18:16; 21:14.
9Anayesamehe makosa hujenga urafiki,
lakini anayekumbusha makosa hutenga rafiki.
10Onyo kwa mwenye busara lina maana,
kuliko mapigo mia kwa mpumbavu.
11Afanyalo mtu mwovu ni kuasi tu;
mjumbe mkatili atatumwa dhidi yake.
12Afadhali kukutana na dubu jike aliyenyang'anywa watoto wake,
kuliko kukutana na mpumbavu katika upumbavu wake.
13Mwenye kulipiza mema kwa mabaya,
mabaya hayataondoka nyumbani mwake.
14Kuanzisha ugomvi ni kama kufanya ufa kwenye bwawa;
achana na ugomvi kabla haujafurika.
15Kumsamehe mwenye hatia na kumwadhibu asiye na hatia
yote mawili ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu.#17:15 Aya hii yawahusu wenye madaraka ya kuhukumu kama mahakimu na waamuzi. Neno linalotumiwa hapa kama “chukizo” ni lile lile linalotumiwa kusema kuhusu kitendo cha kuabudu miungu ya uongo, jambo ambalo ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu. Hapa inaonekana dhahiri jinsi ilivyo vibaya mno mbele ya Mungu kumhukumu mtu aliye na hatia kwamba hana hatia na asiye na hatia kwamba ana hatia.
16Ya nini mpumbavu kuwa na fedha mkononi kununulia hekima,
wakati yeye mwenyewe hana akili?
17Rafiki wa kweli ni rafiki siku zote,
ndugu huzaliwa asaidie wakati wa taabu.
18Si jambo la akili kuweka rehani,
na kuwa mdhamini wa mtu mwingine.#17:18 … kuwa mdhamini wa mtu mwingine: Rejea Meth 6:1-3 maelezo.
19Anayependa ugomvi anapenda dhambi;
anayejigamba#17:19 Anayejigamba: Au, “Mtu anayejivunia mali yake.” anajitafutia maangamizi.
20Mwenye moyo mpotovu hafanikiwi,
na msema uongo hupatwa na maafa.
21Mtoto mpumbavu ni huzuni kwa baba yake,
na baba wa mpumbavu hana furaha.
22Moyo mchangamfu ni dawa,
bali moyo wenye huzuni hudhoofisha mwili.
23Mtu mbaya hupokea hongo kwa siri
ili apate kupotosha haki.
24Mtu mwenye busara lengo lake ni hekima,
lakini mpumbavu hupania kila kitu duniani.
25Mtoto mpumbavu ni huzuni kwa baba yake,
na uchungu kwa mama yake mzazi.
26Si vizuri kumtoza faini mtu asiye na hatia;
ni kosa kumchapa viboko muungwana.
27Asiyesema sana ana maarifa;
mtu mtulivu ni mwenye busara.#17:27-28 Yobu 13:5; Meth 10:19; 12:23. Aya hizi mbili zinaendana pamoja, ya pili ikitilia mkazo usemi wa aya iliyotangulia ambayo inasema juu ya tabia ya mwenye hekima.
28Hata mpumbavu akinyamaza huonekana ana hekima;
akifunga mdomo wake huonekana kuwa mwenye akili.

Copyright The Bible Society of Tanzania, 1993

The Bible Society of Kenya 1993

Learn More About Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza