Methali 28
BHNTLK

Methali 28

28
1Waovu hukimbia japo hawafukuzwi na mtu,
lakini waadilifu ni hodari#28:1 Waovu hukimbia …waadilifu ni hodari: Watu wa aina hizi mbili, waadilifu na waovu, ni wazo linalorudiwa mara nyingi katika sura hii (28:4,10,12,18,28). kama simba.
2Taifa la fujo huzusha viongozi wengi,
lakini kwa kiongozi mmoja mwenye akili na maarifa huwa na utengemano
3Mtu mhitaji anayewadhulumu maskini,#28:3 Mtu mhitaji anayewadhulumu maskini …: Katika sura hii kuna methali kadhaa juu ya utajiri na umaskini (28:6,8,11, 19,22,25,27).
amefanana na mvua kubwa inayoharibu mimea.
4Watu wanaovunja sheria huwasifu waovu,
lakini wanaoishika sheria hupingana nao.
5Waovu hawajui maana ya haki,
lakini wamchao Mwenyezi-Mungu wanaielewa kabisa.
6Afadhali maskini aishiye kwa unyofu,
kuliko tajiri aishiye kwa upotovu.
7Mtoto ashikaye sheria ni mwenye hekima,
lakini rafiki wa walafi humwaibisha baba yake.
8Aongezaye mali yake kwa riba na kutoza faida
anamkusanyia mwingine mwenye kuwahurumia maskini.
9Anayekataa kuisikia sheria,
huyo hata sala yake ni chukizo kwa Mungu.
10Anayemshawishi mtu mwema#28:10 Anayemshawishi mtu mwema …: Kuhusu methali nyingine za namna hii taz 26:27 maelezo na pia lile onyo alilotoa Bwana Yesu katika Mat 18:6. kutenda mabaya,
ataanguka katika shimo lake mwenyewe.
Wasio na hatia wamewekewa mema yao.
11Tajiri hujiona mwenyewe kuwa mwenye hekima,
lakini maskini mwenye busara atamfichua.
12Watu wema wakipata madaraka maisha hufana,
lakini waovu wakitawala watu hujificha.
13Afichaye makosa yake hatafanikiwa;
lakini anayeungama na kuyaacha atapata rehema.#28:13 Afichaye makosa …anayeungama … atapata rehema: Methali hii inawatahadharisha wanaoendelea kutenda dhambi bila kutubu kwamba wataishia katika kupoteza walicho nacho (taz pia 3:33; 6:12-15; 10:16,28,29).
14Heri mtu amchaye Mwenyezi-Mungu daima;
lakini mkaidi wa moyo ataangukia maafa.
15Mtawala mwovu anayewatawala maskini,
ni kama simba angurumaye au dubu anayeshambulia.
16Mtawala asiye na akili ni mdhalimu mkatili;
lakini achukiaye mali ya udanganyifu atatawala muda mrefu.
17Mtu anayelemewa na hatia ya kuua mtu,
atakuwa mkimbizi mpaka kaburini;
mtu yeyote na asijaribu kumzuia.
18Aishiye kwa unyofu atasalimishwa,
lakini mdanganyifu ataanguka kabisa.
19Anayelima shamba lake atapata chakula kingi,
bali anayefuata yasiyofaa atapata umaskini tele.#28:19 Anayelima shamba lake …anayefuata yasiyofaa … umaskini tele: Aya hii inafanana na 12:11.
20Mtu mwaminifu atapata baraka tele,
lakini mwenye pupa ya kuwa tajiri hataepa adhabu.
21Si vizuri kumbagua mtu;#28:21 Kumbagua mtu: Kinachosemwa hapa ni sawa na methali ya 18:5 na pia 24:23.
watu hufanya mabaya hata kwa kipande cha mkate.
22Mtu bahili hukimbilia mali,
wala hajui kwamba ufukara utamjia.
23Amwonyaye mwenzake hatimaye hupata mema#28:23 Amwonyaye mwenzake hatimaye hupata mema …: Kumkosoa mtu ni alama ya urafiki maana hutaki aangamie katika kosa (15:31; 27:5). zaidi,
kuliko yule anayembembeleza kwa maneno matamu.
24Anayeiba mali ya baba yake au mama yake, akasema si kosa,
hana tofauti yoyote na wezi wengine.
25Mchoyo huchochea ugomvi,
lakini anayemtegemea Mwenyezi-Mungu atafanikiwa.
26Anayetegemea akili yake mwenyewe ni mpumbavu;
lakini anayeishi kwa hekima atakuwa salama.
27Aliye mkarimu kwa maskini hatatindikiwa kitu,
lakini anayekataa kuwaangalia atalaaniwa kwa wingi.
28Waovu wakitawala watu hujificha,
lakini wakiangamia, waadilifu huongezeka.

Copyright The Bible Society of Tanzania, 1993

The Bible Society of Kenya 1993

Learn More About Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza