Methali 6
BHNTLK

Methali 6

6
Maonyo manne#6:1-3 Kama umejitolea kumdhamini jirani yako: Aya hizi zahusu mtu na jirani yake, au mwenzake katika biashara, n.k. (lakini sio rafiki wa ndani au mtu wa jamaa). Kujitolea kumdhamini mtu wa namna hiyo kulikuwa na athari zake kwa vile mdhamini angaliweza kuishia kuwa mtumwa wa mdai anayehusika.
1Mwanangu, kama umejitolea kumdhamini jirani yako,
ikiwa umetoa ahadi yako kwa ajili ya mtu huyo,#6:1-19 Maonyo manne. Onyo la kwanza ni juu ya kuepuka madeni (rejea 6:1-5); ling 11:15; 17:18; 20:16; 22:26-27. Onyo la pili ni juu ya uvivu (6:6-11); ling 10:4-5; 24:30-34; 26:13-16; 27:23-27; 31:13-27; onyo la tatu ni juu ya uongo (6:12-15), na la nne ni juu ya tabia Mungu anayoichukia (6:16-19).
2umejibana kwa maneno yako mwenyewe,
umejinasa kwa ahadi uliyofanya.
3Ujue kwamba uko chini ya mamlaka ya mwenzio,
lakini mwanangu, ukitaka kujiokoa, basi fanya hivi:
Mwendee mtu huyo mara moja umsihi akupe uhuru wako.
4Jitahidi usiache macho yako yapate usingizi,
wala kope za macho yako zisinzie.
5Jiokoe kwa kujitoa katika mtego huo,
mithili ya paa ama ndege amtorokavyo mwindaji.
6Ewe mvivu! Hebu ukamchungulie sisimizi,
fikiria namna yake ya kuishi ukapate hekima.
7Sisimizi hana kiongozi, ofisa, wala mtawala;
8lakini hujiwekea chakula wakati wa kiangazi,
hujikusanyia akiba wakati wa mavuno.
9Ewe mvivu, utalala hapo mpaka lini?
Utaamka lini katika usingizi wako?
10Wasema: “Acha nilale kidogo tu,
acha nisinzie kidogo!
niache nikunje mikono nipumzike kidogo!”
11Wakati huo umaskini utakuvamia kama mnyang'anyi,
ufukara utakufuata kama jambazi.#6:10-11 Acha nilale kidogo …jambazi: Hili ni onyo kuhusu kuwa mvivu au kutojali kazi inayohitajika kufanywa; (taz pia 10:4-5; 19:15; 20:4,13; 24:33-34). Katika vitabu vyote vya Biblia, Kitabu cha Methali ndicho chenye kutaja kwa wingi zaidi (mara 230) uvivu kama jambo la kulaaniwa.
12Mtu mwovu, mtu asiyefaa kitu,
huzururazurura akisema maneno mapotovu.
13Hukonyeza jicho kuwakosesha wengine,
huparuza kwa nyayo,
na kuashiria watu kwa vidole.#6:13 Hukonyeza jicho …na kuashiria watu kwa vidole: Maana halisi ya kitendo hicho si rahisi kuielewa. Huenda yahusu tabia ya udanganyifu ya waongo au wafanyabiashara ambao hukonyezea wenzao kuwapunja wateja wao. Taz pia 16:30.
14Akiwa amejaa ulaghai moyoni hutunga maovu,
huzusha ugomvi kila mahali.
15Kutokana na hayo maafa yatamvamia ghafla,
ghafla atadhurika vibaya asiweze kupona tena.
16Kuna vitu sita anavyochukia Mwenyezi-Mungu;
naam, vitu saba ambavyo ni chukizo kwake:
17Macho ya kiburi,
ulimi mdanganyifu,
mikono inayoua wasio na hatia,
18moyo unaopanga mipango miovu,
miguu iliyo mbioni kutenda maovu,
19shahidi wa uongo abubujikaye uongo,
na mtu achocheaye fitina kati ya ndugu.
Onyo dhidi ya uasherati
20Mwanangu, shika maagizo ya baba yako,
wala usisahau mafundisho ya mama yako;
21yaweke daima moyoni mwako,
yafunge shingoni mwako.#6:21 … yafunge shingoni mwako: Yamkini ni msemo unaosisitiza kwamba mafundisho hayo ni lazima yazingatiwe daima kama mkufu anaovaa mtu daima bila kuutoa. Taz pia 3:1,3.
22Yatakuongoza njiani mwako,
yatakulinda wakati ulalapo,
yatakushauri uwapo macho mchana.
23Maana amri hiyo ni taa,
na sheria hiyo ni mwanga.
Maonyo hayo na nidhamu yatuweka njiani mwa uhai.#6:23 Amri hiyo ni taa …yatuweka njiani mwa uhai: Rejea Zab 119:105.
24Yatakulinda mbali na mwanamke mbaya,
yatakuepusha na maneno matamu ya mwanamke mgeni.
25Usimtamani mwanamke huyo kwa uzuri wake,
wala usikubali kunaswa kwa kope za macho yake.
26Mtu hupoteza kipande cha mkate kwa malaya,
lakini kwa mke wa mtu mwingine utapoteza uhai#6:26 Hupoteza …mkate kwa malaya, lakini kwa mke wa mtu … uhai: Mwandishi anaelezea uharibifu unaotokana na uzinzi. Kujamiiana na mke au mume wa mtu mwingine adhabu ilikuwa ni kifo (Lawi 20:10). wako wote.
27Je, waweza kuweka moto#6:27 Moto: Mifano ya moto na makaa ya moto ilifaa sana kuelezea tamaa kubwa za mwili. kifuani
na nguo zako zisiungue?
28Je, waweza kukanyaga makaa ya moto
na nyayo zako zisiungue?
29Ndivyo alivyo mwanamume alalaye na mke wa mwenzake;
yeyote anayemgusa mwanamke huyo hataacha kuadhibiwa.
30Watu hawambezi sana mtu akiiba kwa sababu ya njaa;
31lakini akipatikana lazima alipe mara saba;#6:31 Alipe mara saba: Idadi “saba” inatumiwa mara nyingi katika Biblia kuashiria idadi kamilifu.
tena atatoa mali yote aliyo nayo.
32Mwanamume anayezini na mke wa mtu hana akili kabisa;
huyo hujiangamiza yeye mwenyewe.
33Atapata majeraha na madharau;
fedheha atakayopata haitamtoka.
34Maana wivu wa mume humfanya kuwa mkali kabisa;
wakati atakapolipiza kisasi hana cha kuhurumia.
35Hatakubali fidia yoyote;
wala kutulizwa na zawadi zako nyingi.

Copyright The Bible Society of Tanzania, 1993

The Bible Society of Kenya 1993

Learn More About Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza