124
Mungu kinga yetu
(Wimbo wa Kwenda Juu, wa Daudi)
1“Kama Mwenyezi-Mungu asingalikuwa upande wetu…”
Semeni nyote mlio katika Israeli:
2“Kama Mwenyezi-Mungu asingalikuwa upande wetu,
wakati ule tuliposhambuliwa na maadui,#124:2-4 Mwenyezi-Mungu asingalikuwa …tuliposhambuliwa na maadui: Mazingira ya mashambulio hayo hayatajwi lakini inaonekana ile sala iliyotajwa katika 123:4 Mungu aliisikiliza. Matumizi ya “gharika” na “mto wa maji” ni ya kimfano kuashiria nguvu za hao maadui.
3hakika tungalimezwa tukiwa hai,
wakati hasira zao zilipotuwakia.
4Tungalikumbwa na gharika,
tungalifunikwa na mto wa maji,
5mkondo wa maji ungalituchukua!”
6Atukuzwe Mwenyezi-Mungu,
ambaye hakutuacha makuchani mwao.
7Tumeponyoka kama ndege mtegoni;
mtego umeteguliwa, nasi tukaokoka.
8Msaada wetu watoka kwa Mwenyezi-Mungu,
aliyeumba mbingu na dunia.