Zaburi 125
BHNTLK

Zaburi 125

125
Usalama wa watu wa Mungu
(Wimbo wa Kwenda Juu)
1Wanaomtegemea Mwenyezi-Mungu, wako kama mlima Siyoni,
ambao hautikisiki bali wabaki imara daima.
2Kama Yerusalemu inavyozungukwa na milima,
ndivyo Mwenyezi-Mungu awazungukavyo#125:2 Yerusalemu inavyozungukwa na milima …Mwenyezi-Mungu awazungukavyo: Milima inayouzunguka mji wa Yerusalemu inaupatia ulinzi na mfano huo unatumiwa kwa Mungu ambaye ndiye anayewalinda watu wake kila upande. watu wake,
tangu sasa na hata milele.
3Waovu hawataendelea kutawala nchi ya waadilifu;
wasije waadilifu nao wakafanya maovu.
4Ee Mwenyezi-Mungu, uwe mwema kwa watu wema,
kwa wale wanaozitii amri zako.
5Lakini wanaogeuka na kufuata njia zao mbaya
uwakumbe#125:5 Uwakumbe: Yaani uwaadhibu au uwaondolee mbali. pamoja na watenda maovu.
Amani iwe na Israeli!

Copyright The Bible Society of Tanzania, 1993

The Bible Society of Kenya 1993

Learn More About Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza