128
Tuzo kwa jamaa imchayo Mungu
(Wimbo wa Kwenda Juu)
1Heri wote wamchao Mwenyezi-Mungu,
wanaoishi kufuatana na amri zake.
2Utapata matunda ya jasho lako,
utafurahi na kupata fanaka.
3Mkeo atakuwa kama mzabibu wa matunda mengi nyumbani mwako;
watoto wako kama chipukizi za mzeituni kuzunguka meza yako.
4Naam, ndivyo atakavyobarikiwa
mtu amchaye#128:1-4 Heri wote wamchao …atakavyobarikiwa mtu amchaye: Baraka za Mungu huwajia watu wanaotii amri zake. Baraka hizo ni pamoja na fanaka na familia yenye afya (taz 127:3-5). Mwenyezi-Mungu.
5Mwenyezi-Mungu akubariki kutoka Siyoni!
Uione fanaka ya Yerusalemu, siku zote za maisha yako.
6Uishi na hata uwaone wajukuu zako!
Amani iwe na Israeli!#128:5-6 Kutoka Siyoni …amani iwe na Israeli: Ilifikiriwa kwamba baraka za Mwenyezi-Mungu ziliwafikia watu kutoka Siyoni, yaani kwa jumla kutoka Yerusalemu, kwa vile huko ndiko kulikokuwa na hekalu la Mwenyezi-Mungu na makao yake hapa duniani.