129
Sala dhidi ya maadui wa Israeli
(Wimbo wa Kwenda Juu)
1“Nimesumbuliwa vibaya tangu ujana wangu…”
Kila mtu katika Israeli na aseme:
2“Nimesumbuliwa vibaya tangu ujana wangu,#129:2 Tangu ujana wangu: Labda yahusu wakati Waisraeli walipokuwa bado Misri.
lakini hawakufaulu kunishinda.
3Walinijeruhi vibaya mgongoni mwangu,
wakafanya kama mkulima anayelima shamba.
4Lakini Mwenyezi-Mungu ni mwadilifu;
amezikata kamba za hao watu waovu.”#129:4 Kamba za hao watu waovu: Fungu hili la maneno linatumiwa kimfano kuashiria uwezo wa watu waovu kuwafanya wengine kuwa watumwa na kuwatendea kwa ukatili.
5Na waaibishwe na kurudishwa nyuma,
wote wale wanaouchukia mji wa Siyoni.
6Wawe kama nyasi juu ya paa la nyumba,#129:6 Nyasi juu ya paa la nyumba: Nyumba za huko Palestina wakati huo zilikuwa kwa wingi na mapaa yaliyo bapa. Mara nyingine majani yaliota juu yake, lakini mara nyingi joto la jua na ukosefu wa udongo wa kutosha uliyafanya kunyauka na hata kukauka kabisa.
ambazo hunyauka kabla hazijakua,
7hakuna anayejishughulisha kuzikusanya,
wala kuzichukua kama matita.
8Hakuna apitaye karibu atakayewaambia:
“Mwenyezi-Mungu awabariki!
Twawabariki kwa jina la Mwenyezi-Mungu!”#129:8 Miongoni mwa laana ambazo Mwanazaburi anawatakia waovu ni kutopata baraka, na hilo ni balaa maana bila baraka hakuna atakayestahimili.