Zaburi 130
BHNTLK

Zaburi 130

130
Kuomba msaada#130 Zaburi hii ni maoombolezo ya mtu ambaye anayejua kwamba anataabika kwa sababu ya dhambi zake mwenyewe (aya 3) na za watu wake.
(Wimbo wa Kwenda Juu)
1Toka upeo wa unyonge wangu,
nakulilia, ee Mwenyezi-Mungu.
2Ee Bwana, sikia sauti yangu,
uitegee sikio sauti ya ombi langu.
3Kama, ee Mwenyezi-Mungu ungekumbuka maovu yetu#130:3 Kama …ungekumbuka maovu yetu …: Mwanazaburi anakiri na kuungama kwamba binadamu ni mwenye dhambi na ni kwa wema wa Mungu peke yake binadamu anaweza kusalimika.
nani, ee Bwana, angeweza kusalimika?
4Lakini kwako twapata msamaha,
ili sisi tukuheshimu.
5Namtumainia Mwenyezi-Mungu kwa moyo wangu wote;
nina imani sana na neno lake.#130:5-6 Neno lake: Hapa neno lake Mungu ni ahadi yake ya kuwasaidia wanaomwendea kumwomba. Marudio ya aya 5 katika aya 6 kuna shabaha ya kutilia mkazo jambo la kumngojea na kumtumaini Mungu.
6Ninamtumainia Mwenyezi-Mungu
kuliko walinzi wanavyongojea pambazuko;
kuliko walinzi wanavyongojea kuche asubuhi.
7Ee Israeli, umtumainie Mwenyezi-Mungu,
maana kwake Mwenyezi-Mungu kuna fadhili,
kwake kuna nguvu kubwa ya kutukomboa.
8Yeye atawakomboa watu wa Israeli
kutoka katika maovu yao yote.

Copyright The Bible Society of Tanzania, 1993

The Bible Society of Kenya 1993

Learn More About Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza