131
Kumtumainia Mungu kwa utulivu#131 Katika zaburi hii Mwanazaburi anatumia picha ya maneno murua kabisa kuelezea anavyomtegemea Mungu na anawahimiza Waisraeli wenzake wamtumainie Mungu vivyo hivyo.
(Wimbo wa Kwenda Juu, wa Daudi)
1Ee Mwenyezi-Mungu, sina moyo wa kiburi;
mimi si mtu wa majivuno.
Sijishughulishi na mambo makuu,
au yaliyo ya ajabu mno kwangu.
2Ila nafsi yangu imetulia na kuwa na amani,
kama mtoto mchanga alivyotulia na mama yake;#131:2 Kama mtoto mchanga alivyotulia na mama yake: Wataalamu wengine wa mambo ya Biblia wanafikiri Zaburi hii huenda ilitungwa na mwanamke. Kuhusu picha ya Mungu kama mama taz Isa 66:12-13; Hos 11:3-4; Luka 13:34.
ndivyo nafsi yangu ilivyo tulivu.
3Ee Israeli, umtumainie Mwenyezi-Mungu,
tangu sasa na hata milele.