133
Uzuri wa umoja kati ya watu
(Wimbo wa Kwenda Juu, wa Daudi)
1Ni jambo zuri na la kupendeza sana
ndugu kuishi pamoja kwa umoja.
2Ni kama mafuta#133:2 Kama mafuta: Mafuta yalitumiwa kumweka wakfu kuhani mkuu. Taz 2:2 maelezo. Si rahisi kuelewa matumizi ya kitendo hicho cha kumpaka mafuta Aroni. Wengi wanafikiri kwamba kama vile hayo mafuta yalivyoenea ndivyo ulivyo uhusiano wa kudumu kati ya ndugu. Lakini hakuna maelezo ya kutosheleza kabisa juu ya mfano huu. mazuri yatiririkayo kichwani,
mpaka kwenye ndevu zake Aroni,
mpaka upindoni mwa vazi lake shingoni.
3Ni kama umande wa mlima Hermoni,
uangukao juu ya vilima vya Siyoni!#133:3 Umande wa mlima Hermoni …vilima vya Siyoni: Hapa pia si rahisi kujua mfano huo unatumiwa namna gani. Lakini Mwanazaburi hapa pia anaonesha kwa picha jinsi ilivyo vizuri sana uhusiano mwema kati ya ndugu.
Huko Mwenyezi-Mungu ameahidi kuwabariki watu wake,
kuwapa uhai usio na mwisho.