134
Msifuni Mungu#134 Zaburi hii ni ya mwisho ya fungu la zaburi zenye anwani “Wimbo wa Kwenda Juu” (taz Zab 120).
(Wimbo wa Kwenda Juu)
1Njoni kumsifu Mwenyezi-Mungu enyi watumishi wake wote,
enyi nyote mnaotumikia usiku nyumbani mwake.
2Inueni mikono kuelekea mahali patakatifu,
na kumtukuza Mwenyezi-Mungu!
3Mwenyezi-Mungu awabariki kutoka Siyoni;#134:3 Mwenyezi-Mungu awabariki kutoka Siyoni: Maneno haya huenda yalitamkwa na kuhani kuwatakia baraka mahujaji waliofika Yerusalemu kwa sikukuu fulani. Taz pia 104.
yeye aliyeumba mbingu na dunia.