Zaburi 150
BHNTLK

Zaburi 150

150
Zaburi ya kumsifu Mungu#150 Zaburi hii ya mwisho katika mkusanyo wa zaburi labda ilitungwa kwa lengo hilohilo, iwe ya mwisho kama matamshi ya sifa mwishoni mwa vitabu vinne vya kwanza vya zaburi (taz 41:13; 72:18-20; 89:52; 106:48). Zaburi inaanza na kumalizia kwa mwito wa kumsifu Mwenyezi-Mungu.
1Msifuni Mwenyezi-Mungu!
Msifuni Mungu katika patakatifu pake;
msifuni katika mbingu zake kuu.
2Msifuni kwa sababu ya matendo yake makuu;
msifuni kwa ajili ya utukufu wake mkuu.
3Msifuni kwa mlio wa tarumbeta;
msifuni kwa zeze na kinubi!#150:3-5 Aya hizi zinaorodhesha ala za muziki zilizotumiwa hekaluni kwa ibada.
4Msifuni kwa ngoma na kucheza;
msifuni kwa filimbi na banjo!
5Msifuni kwa kupiga matoazi.
msifuni kwa matoazi ya sauti kubwa.
6Kila kiumbe hai kimsifu Mwenyezi-Mungu!
Msifuni Mwenyezi-Mungu!#150:6 Mkusanyo wa Zaburi unamalizia kwa mwito wa viumbe vyote hai vimsifu Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli.

Copyright The Bible Society of Tanzania, 1993

The Bible Society of Kenya 1993

Learn More About Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza