15
Acheni ubinafsi
1Sisi#15:1 Sisi: Naye Paulo anajihesabu kati ya waamini wanaomwamini Kristo bila kuwa na mashaka. tulio imara katika imani tunapaswa kuwasaidia#15:1 Kuwasaidia: Yaani kutowakwaza kama aliyoeleza katika sura iliyotangulia. wale walio dhaifu wayakabili matatizo yao. Tusijipendelee sisi wenyewe tu. 2Kila mmoja wetu anapaswa kumpendeza jirani#15:2 Kumpendeza jirani: Ni maelezo ya 13:8-10. yake kwa wema ili huyo apate kujijenga katika imani.#15:2 Huyo apate kujijenga katika imani: Yaani yule ambaye imani yake ni dhaifu aweza kuwa na ushupavu wa kutoyumbayumba kiimani wala asikwazike kwa haraka. 3Maana Kristo hakujipendelea mwenyewe;#15:3 Maana Kristo hakujipendelea mwenyewe: Paulo amekwisha washauri wapendane na wasiishi kwa ajili yao wenyewe, kwa hiyo, ndiyo sababu anaanza na neno maana ni kana kwamba anataka waige mfano wake Yesu Kristo Mwokozi wao aliyewaita wamfuate. ila alikuwa kama yasemavyo Maandiko: “Kashfa zote walizokutolea wewe zimenipata mimi.” 4Maana, yote yaliyoandikwa#15:4 Yote yaliyoandikwa: Hapa Paulo anamaanisha maandiko ya Agano la Kale. yameandikwa kwa ajili ya kutufundisha sisi ili kutokana na saburi na faraja tupewayo na hayo Maandiko Matakatifu tupate kuwa na matumaini.#15:4 Matumaini: Baada ya kutaja mambo mawili: saburi na faraja ambayo alikwisha taja katika 5:2-5; 8:20,25; 12:12. Paulo anakaza hivyo anapowaandikia Wakolosai (Kol 1:11) na kwa Wathesalonike (1Thes 1:3-4; ling 1Tim 6:11; 2Tim 3:11; Tito 2:2; Ebr 10:36; Yak 1:4; 2Pet 1:6). 5Mungu aliye msingi wa saburi na faraja yote,#15:5 Hapo Paulo anawaeleza Waroma chanzo cha hayo mambo mawili saburi na faraja. Anataka kuwashauri kuwa waendelee kumwamini Mungu katika Kristo, ili waweze kuwa na matumaini na Mungu mwenyewe. Hoja yake ni kwamba kwa nguvu zao hawawezi kujivunia saburi na faraja (taz pia 15:13). awajalieni nyinyi kuwa na msimamo mmoja#15:5 Msimamo mmoja: Wapatane katika mambo ambayo yaweza kuvuruga umoja wao au wito wao kwa kuishi kwa amani. kufuatana na mfano wake Kristo Yesu,#15:5 Mfano wake Kristo Yesu: Anakumbusha habari za maisha ya Mwokozi wao bila kutaja kwa kirefu au kueleza kinaganaga jinsi Yesu Kristo alivyokuja ulimwenguni akavumilia taabu tangu kuzaliwa mpaka alipofufuka. 6ili nyinyi nyote,#15:6 Elekezo kwao wasomaji kuwa wakipata saburi na faraja kwa matumaini basi, wamsifu asili ya hayo. kwa nia moja na sauti moja,#15:6 Kwa nia moja na sauti moja: Ni mkazo huohuo uliomo katika aya 5. Hapo awali amekwisha sisitiza kuwa watumie vipaji vyao kujenga mwili wa Kristo, sasa anarudia kusisitiza kuwa wafanye vivyo hivyo kwa ushirikiano, utengano waweza kuharibu uhusiano kati yao wakakosa kumsifu Mungu wao. Naye Yesu alikwisha waombea waumini wake wawe na umoja (Yoh 17:21-22). Mkazo wa Paulo kuhusu umoja kati ya waumini ni kama wahenga walivyosema, katika methali ya Kiswahili, “Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu.” mumtukuze Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo.
Habari Njema kwa watu wote
7Basi, karibishaneni#15:7 Karibishaneni: Mkazo anaorudia mara kwa mara. Wanaokaribishana wasukumwa na upendo (taz pia 12:13; 14:1), wafanya hivyo kwa kumwigiza Mwokozi wao (taz 15:7). Paulo aongeza mkazo wake juu ya mafundisho ya Yesu Kristo (taz Mat 25:31-46). kwa ajili ya utukufu wa Mungu kama naye Kristo alivyowakaribisheni.#15:7 Kama naye Kristo alivyowakaribisheni: Yaani alipowaita wamfuate na pia alivyowapa matumaini ya kuwa naye mbinguni (taz k.m. Mat 11:28-30; 25:34-40,46b; Yoh 11:25; 17:24; ling Ufu 2:10b; 3:11-12). 8Maana, nawaambieni Kristo aliwatumikia Wayahudi#15:8 Kristo aliwatumikia Wayahudi: Tafsiri nyingine Kristo amefanyika mhudumu wa agano la kutahiriwa. Hoja ya Paulo ni kwamba Yesu Kristo kama Myahudi mzawa wa Abrahamu aliishi kama hao Wayahudi kwa sababu ya lengo la Mungu la kuokoa ulimwengu kwa njia yake. Naye Yesu alimtii Mungu, ambaye kila mara alimtaja kuwa Baba yake (taz k.m. Yoh 15:5-17,23-27; 16:1—17:26; 18:11). apate kuonesha uaminifu wa Mungu, na zile ahadi Mungu alizowapa babu zetu#15:8 Ahadi Mungu alizowapa babu zetu: Ahadi kwa Abrahamu, Isaka na Yakobo hasa kuwa kutokana na Abrahamu kutakuweko taifa kubwa na mtawala atazaliwa kati ya wazawa wake Abrahamu ambaye hata manabii walitabiri juu yake (taz k.m. Mwa 12:1-3; Isa 7:14; 9:6-7; 11:1-5; Mika 5:2; ling Isa 61:1-3). zipate kutimia; 9ili nao watu wa mataifa mengine wapate kumtukuza Mungu#15:9 Mataifa mengine wapate kumtukuza Mungu: Ndivyo Mungu alivyomwahidi Abrahamu kuwa mataifa ya ulimwengu yatabarikiwa kwa njia yake. Ni wazi kuwa yakibarikiwa yatapaswa kusifu baraka za Mwenyezi-Mungu. kwa sababu ya huruma yake.#15:9 Huruma yake: Mungu alilichagua taifa la Israeli na kulihurumia mara nyingi walipomkosea, ni kwa ajili ya agano lake kwao ili waendelee kuwa taifa lake teule na ili mataifa mengine yapate pia kubarikiwa. Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu:
“Kwa hiyo nitakusifu miongoni mwa watu wa mataifa.
Nitaziimba sifa za jina lako.”#15:9 Paulo ananukuu maneno ya Zab 18:49; ling 2Sam 22:50.
10Tena Maandiko yasema:
“Furahini, enyi watu wa mataifa;
furahini pamoja na watu wake.”
11Na tena:
“Enyi mataifa yote, msifuni Bwana;
enyi watu wote, msifuni.”
12Tena Isaya asema:
“Atatokea chipukizi katika ukoo wa Yese,#15:12 Ukoo wa Yese: Paulo hatoi maelezo kuhusu nukuu hii, lakini anajua wanaelewa kuwa inatokana na Isa 11:1. Hii ina historia yake ya pekee - Yese alimzaa Daudi. Naye Daudi anatajwa mara nyingi katika Agano la Kale na Agano Jipya, kwa kuwa Mungu alimchagua na akamweka kuwa mfalme wa watu wake, akawa mfano mzuri wa mtawala anayemtii na aliahidi kuwa ufalme wake utakuwa wa milele (taz 2Sam 7:11b-16, ling Zab 132:11-18; Eze 29:21). Naye Yesu alijulikana pia kama mwana wa Daudi (taz k.m. Mat 9:27; 22:23; 15:22; 20:30-31; 21:15; Marko 10:47-48; 12:35; Luka 18:36-39).
naye atawatawala watu wa mataifa;
nao watamtumainia.”
13Basi, Mungu aliye msingi wa matumaini,#15:13 Mungu aliye msingi wa matumaini: Taz maelezo ya aya ya 5. Maneno furaha, amani, tumaini yanasisitizwa sana na Paulo katika barua zake. Mkazo wake kuwa Mungu ni asili au msingi wa matumaini unaonesha jinsi anavyowashauri wasitegemee kuzaliwa kwao kuwa ni Wayahudi au wale wa mataifa mengine kuona kuwa kwa sababu Kristo amewaokoa nao wanaweza kujipatia matumaini. awajazeni furaha yote na amani kutokana na imani yenu; tumaini lenu lipate kuongezeka kwa nguvu ya Roho Mtakatifu.#15:13 Kwa nguvu ya Roho Mtakatifu: Kwa kuwa mtu hawawezi kujipatia furaha, amani, tumaini wajue kuwa mwenye kuwawezesha ni Mungu kwa njia ya Roho Mtakatifu. Kwa maneno mengine ni kwamba bila Roho Mtakatifu hakuna tumaini kamili. Hapa Paulo anakumbusha aliyokwisha sema kuhusu Roho Mtakatifu hapo awali katika barua hii, k.m. katika 8:9.
Huduma ya Paulo
14Ndugu zangu, mimi binafsi nina hakika kwamba nyinyi pia mmejaa wema,#15:14 Mmejaa wema: Paulo anasifu aliowaandikia ili asiwakatishe tamaa, kwani barua yote si juu ya kuwasifu, amewapa maongozi pia kuhusu wito wao na jukumu walilonalo kwa kuishi pamoja. elimu yote, na mnaweza kushauriana nyinyi kwa nyinyi. 15#15:15-21 Sababu ya kuwaandikia Waroma.Lakini nimewaandikia hapa na pale katika barua hii bila woga, nipate kuwakumbusheni juu ya mambo fulani.#15:15 Nipate kuwakumbusheni …mambo fulani: Paulo amewaandikia mambo mengi hii ni pamoja na kuhusu imani, kutahiriwa, ubatizo, kutobaguana, kushirikiana, kupendana, n.k. Nimefanya hivyo kwa sababu ya neema aliyonijalia Mungu 16ya kuwa mtumishi wa Yesu Kristo kwa watu wa mataifa.#15:16 Mtumishi wa Yesu Kristo kwa watu wa mataifa: Aeleza kuhusu wito wake, huduma hii anaitaja mara kadhaa katika barua zake (taz 11:13; 15:18; Fil 2:17; Gal 1:16; Efe 3:8; ling Gal 2:7; Mate 9:15; 13:2; 15:12; 22:21). Ni jukumu langu la kikuhani#15:16 Jukumu langu la kikuhani: Si kama makuhani wa Agano la Kale walivyohudumu katika hekalu, bali yeye ni mwenye kupita mipaka ya nchi yake kuhudumu kati ya watu wa mataifa. kuihubiri Habari Njema#15:16 Kuihubiri Habari Njema: Huduma ya Paulo anajieleza kama inavyosemwa kuhusu Yesu Kristo. Habari Njema ni kuhusu wokovu kwa watu wote. Wayahudi na wasio Wayahudi. Makuhani wa Agano la Kale hawakushughulika sana na kazi ya kuhubiri kwa hiyo hapa twaona wazo la maana kuwa wanaomfuata Yesu aliye kuhani wapaswa nao kuhubiri Injili, ni wajibu wao pia. ya Mungu ili watu wa mataifa mengine wapate kuwa tambiko inayokubaliwa na Mungu,#15:16 Tambiko inayokubaliwa na Mungu: Badala ya watu kutoa ng'ombe, mbuzi, kondoo, n.k. kama sadaka yao, jinsi walivyozoea tangu babu zao, wao wawe sadaka; wenye kupokelewa na Mungu kama watoto wapendwa na hapo Paulo anaeleza kuwa mwenye kufanya hivyo ndani yao ni Roho Mtakatifu, jambo ambalo amekwisha litaja mara kadhaa katika barua hii (taz 8:1-17,26-27; 15:13). Kwa upande mwingine ni kama Paulo anawataka kuwa tambiko, kwani yeye ni kuhani hapo anapowahubiria wakamrudia Mungu wao. tambiko iliyotakaswa na Roho Mtakatifu. 17Kwa hiyo, nikiwa nimeungana na Kristo Yesu,#15:17 Nimeungana na Kristo Yesu: Hapa Paulo anawaeleza, ingawa si kwa kirefu, kuwa amekubaliwa na Kristo. Hapo bila shaka anawakumbusha alivyokwisha sema kuhusu umuhimu wa ubatizo na nia ya kwamba ubatizo wake ulikuwa wa maana; alipobatizwa amekuwa wake Kristo kama wengine walivyo wake Kristo walipobatizwa (taz 6:3-8). naweza kujivunia huduma yangu kwa ajili ya Mungu. 18Sithubutu kusema kitu kingine chochote isipokuwa tu kile ambacho Kristo Yesu amekifanya kwa kunitumia mimi ili watu wa mataifa wapate kutii.#15:18 Watu wa mataifa wapate kutii: Ndiyo sababu ya Paulo kufanya huduma (ling 6:16; 16:19; 2Kor 9:13). Amefanya hivyo kwa maneno na vitendo,#15:18 Kristo Yesu …amefanya hivyo kwa maneno na vitendo: Jinsi alivyomtumia Paulo kati ya mataifa. 19kwa nguvu ya miujiza na maajabu, na kwa nguvu ya Roho wa Mungu.#15:19-21 Namna Kristo alivyomtumia Paulo. Ni maelezo zaidi ya aya ya 18. Basi, kwa kusafiri kila mahali, tangu kule Yerusalemu mpaka Iluriko,#15:19 Tangu kule Yerusalemu mpaka Iluriko: Ni maelezo kuhusu safari yake ya kwenda Yerusalemu mahali Injili ilipoanzia (ling Mate 1:8; Mat 28:18-20). Iluriko ni katika mkoa wa Roma huko kaskazini ya Makedonia panapojulikana leo kama Albania na Yugoslavia. Bahati mbaya hatupati maelezo ya kazi aliyofanya huko Iluriko, hasemi lolote katika barua yake wala Luka katika Matendo ya Mitume hakueleza chochote kuhusu kukaa kwake huko wala hataji kama alifika huko. nimeihubiri kikamilifu Habari Njema ya Kristo. 20Nia yangu imekuwa daima kuihubiri Habari Njema popote pale ambapo jina la Kristo halijapata kusikika, nisije nikajenga juu ya msingi wa mtu mwingine. 21Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu:
“Watu wote ambao hawakuambiwa habari zake wataona;
nao wale ambao hawajapata kusikia, wataelewa.”#15:21 Paulo ananukuu maneno ya unabii uliomo katika Isaya 52:15. Paulo anaelekeza unabii huo kwake, kwani ndiye ametumwa kwa watu wa mataifa, hao wasio Wayahudi wazawa wa Abrahamu kimwili.
Mpango wa Paulo wa kutembelea Roma
22Kwa sababu hiyo nilizuiwa mara nyingi#15:22 Nilizuiwa mara nyingi: Kwa ajili ya kazi ya mahali pengi alikopitia toka Yerusalemu mpaka Iluriko. Amekwisha taja vivyo hivyo alipoanza kuandika barua hii (taz Rom 1:10-15). kuja kwenu. 23Lakini maadamu sasa nimemaliza kazi yangu pande hizi, na kwa kuwa kwa miaka mingi nimekuwa na nia kubwa ya kuja kwenu, 24natumaini kufanya hivyo sasa. Ningependa kuwaoneni nikiwa safarini kwenda Spania#15:24 Nikiwa safarini kwenda Spania: Kwenda huko kwa mara ya kwanza (taz pia aya ya 28). na kupata msaada wenu kwa safari hiyo#15:24 Kupata msaada wenu kwa safari hiyo: Paulo alitumaini kuwa Kanisa la Roma litajishughulisha na huduma ya misioni likimtumia Paulo. baada ya kufurahia kuwa kwa muda pamoja nanyi. 25Lakini, kwa sasa nakwenda kuwahudumia watu wa Mungu#15:25 Kuwahudumia watu wa Mungu: Tafsiri nyingine ni: kuwahudumia watakatifu: Paulo anawataja hao waliomwamini Kristo walioko Yerusalemu. Sababu ya kurudi Yerusalemu inatajwa katika aya ya 26-28. kule Yerusalemu. 26Maana makanisa ya Makedonia na Akaya#15:26 Makanisa ya Makedonia na Akaya: Tayari wakati huo waumini waliokuwa Makedonia na Akaya walikwisha tambulika kuwa kundi linalojitegemea na hata kusaidia wengine. yemeamua kutoa mchango wao#15:26 Mchango wao: Hapa Paulo hataji aina za mchango bila shaka kwa kuwa ni ule uliotolewa kwa Wakristo anaowataja kuwa maskini wa huko Yerusalemu, huenda ni pesa na vitu vingine walivyokosa kwa maisha yao ya kawaida. Paulo alishauri mara kwa mara Wakristo watoe chochote walichonacho kwa uhuru, upendo ukarimu, n.k. (taz pia 1Kor 16:1-4; 2Kor 8—9), ni namna ya kuonesha upendo wao kwa wengine. kuwasaidia watu wa Mungu walio maskini huko Yerusalemu. 27Wao wenyewe wameamua kufanya hivyo; lakini, kwa kweli, hilo ni jukumu lao kwa hao.#15:27 Jukumu lao kwa hao: Wapaswa kuwajibika kuwatunza hao Habari Njema ilipoanzia. Maana, ikiwa watu wa mataifa mengine wameshiriki baraka za kiroho za Wayahudi,#15:27 Wameshiriki baraka za kiroho za Wayahudi: Kunakotajwa hapa ni kule kupata wokovu ulioahidiwa Wayahudi - kuja kwa Kristo Mkombozi; na ye yote mwenye kuamini apate uzima wa milele. wanapaswa nao pia kuwahudumia Wayahudi katika mahitaji yao ya kidunia. 28Nitakapokwisha tekeleza kazi hiyo na kuwakabidhi mchango huo uliokusanywa kwa ajili yao, nitawatembeleeni nyinyi nikiwa safarini kwenda Spania.#15:28 Yaelekea Paulo hakuwa na shabaha ya kukaa Yerusalemu. Ni dokezo kuwa yeye ametumwa kuwahudumia watu wa mataifa, ingawa hata kule kuwapelekea Wakristo wa Yerusalemu mchango ni kuwahudumia pia, lakini si kukaa na kuhubiri huku na kule. Pia ni wazi kuwa kulikuwepo mitume na wengi waliokuwa Wakristo tayari kwa miaka kadhaa; wahubiri walikuweko, kwa hiyo kutokuwako kwa Paulo si pigo kubwa. 29Najua ya kuwa nikija kwenu nitawaletea wingi wa baraka za Kristo.#15:29 Tumaini la Paulo kuwa kuhubiri Habari Njema kwaleta baraka.
30Basi, ndugu zangu, nawasihi kwa Bwana wetu Yesu Kristo na kwa upendo uletwao na Roho, mniunge mkono kwa kuniombea kwa Mungu.#15:30-32 Mkazo kuhusu umuhimu wa kuomba. Paulo naye alihitaji nguvu ya Roho Mtakatifu. 31Ombeni nipate kutoka salama miongoni mwa wale wasioamini walioko Uyahudi,#15:31 Ombeni nipate kutoka salama miongoni mwa wale wasioamini walioko Uyahudi: Yaelekea Paulo alikuwa na wasiwasi kuhusu hao wapinzani wa Injili ambao yeye anawafahamu vizuri shabaha zao, kwani alikuwa mmoja wao. Kulikuwako waliokuwa tayari kumpinga hii ni wazi kama anavyojieleza mwenyewe taz Mate 20:22-23; 21:7—28:31. nayo huduma yangu huko Yerusalemu ipate kukubaliwa#15:31 Huduma yangu huko Yerusalemu ipate kukubaliwa: Hatujui kwa uwazi anamaanisha nini, kama ni kuhubiri huko; lakini haielekei kama huo ulikuwa wajibu wake huko, labda ni namna ya kugawa mchango aliokuwa akiwapelekea. Kazi ambayo ilipaswa kufanywa vizuri wenye kupokea waridhike na kuufurahia na wenye kutuma wapate ripoti nzuri. na watu wa Mungu walioko huko. 32Hivyo, Mungu akipenda, nitaweza kuja kwenu na moyo wa furaha, nikapumzike pamoja nanyi.#15:32 Mara tatu katika sura hii anataja juu ya safari yake ya kuelekea Roma, na mara anapoitaja anadokeza kuwa atafurahi pamoja nao (taz 22,24,29). 33Mungu aliye chanzo cha amani na awe nanyi nyote! Amina!#15:33 Mwisho hapa wa barua yake Paulo. Mungu chanzo cha amani: tafsiri nyingine: Mungu wa amani. Hapa Paulo anakiri kuwa amani, asili yake ni Mungu tu, si kwa nguvu za kibinadamu; ndiyo sababu hata kwenda kwake Yerusalemu kulihitaji maombi ili asipatwe na fujo au mikasa ya aina yoyote. Mkazo huu kuwa Mungu ni chanzo cha amani unarudiwa mara kwa mara katika barua zake Paulo (taz 5:1; 16:20; 1Kor 7:15; 2Kor 13:11; Fil 4:7,9; 1Thes 5:23, 2Thes 3:16); na kule kutakia wengine amani ni kama ilikuwa tabia yake Paulo (taz pia Rom 12:18; 14:19; 15:13; 1Kor 1:3; 2Kor 1:2; Gal 1:3; Efe 1:2; Fil 1:2; Kol 1:2; 1Thes 1:1; 2Thes 1:2; Tito 1:4; File 3; Gal 6:16; Efe 6:23; 2Tim 2:22; 1Thes 5:13; 2Thes 3:16; 1Tim 2:2; 2Tim 2:22).