1 Nyakati 1
NMM

1 Nyakati 1

1
Kumbukumbu Za Historia Kuanzia Adamu Hadi Ibrahimu
(Mwanzo 5:1-32; 10:1-32; 11:10-26)
Adamu Hadi Wana Wa Nuhu
1 # Mwa 5:1-32; Lk 3:36-38 Adamu, Sethi, Enoshi, 2#Mwa 5:9; Mwa 5:12; Mwa 5:15Kenani, Mahalaleli, Yaredi, 3#Mwa 5:18; Yud 1:14; Mwa 5:21; 5:25; 5:29Idrisi, Methusela, Lameki, Nuhu.
4 # Mwa 6:10; 10:1; 5:32 Wana wa Nuhu walikuwa:
Shemu, Hamu na Yafethi.
Wana Wa Yafethi
5Wana wa Yafethi walikuwa:
Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki na Tirasi.
6Wana wa Gomeri walikuwa:
Ashkenazi, Rifathi na Togarma.
7Wana wa Yavani walikuwa:
Al-Yasa, Tarshishi, Kitimu na Rodanimu.
Wana Wa Hamu
8 # Mwa 16:10 Wana wa Hamu walikuwa:
Kushi, Misri,#1:8 Yaani Misri. Putu na Kanaani.
9Wana wa Kushi walikuwa:
Seba, Havila, Sabta, Raama na Sabteka.
Wana wa Raama walikuwa:
Sheba na Dedani.
10 # Mwa 10:8, 13 Kushi akamzaa
Nimrodi, ambaye alikua akawa mtu shujaa katika nchi.
11Misri akawazaa:
Waludi, Waanami, Walehabi, Wanaftuhi, 12#Mwa 10:14; Kum 2:23; Yer 47:4; Amo 9:7Wapathrusi, Wakasluhi (hao ndio asili ya Wafilisti) na Wakaftori.
13Wana wa Kanaani walikuwa:
Sidoni, mzaliwa wake wa kwanza, na Hethi, 14Wayebusi, Waamori, Wagirgashi, 15Wahivi, Waariki, Wasini, 16Waarvadi, Wasemari na Wahamathi.
Wana Wa Shemu
17 # Mwa 9:23-26; 10:22; 11:10 Wana wa Shemu walikuwa:
Elamu, Ashuru, Arfaksadi, Ludi na Aramu.
Wana wa Aramu walikuwa:
Usi, Huli, Getheri na Mesheki.
18Arfaksadi akamzaa Shela,
Shela akamzaa Eberi.
19Eberi alipata wana wawili:
Mmoja wao aliitwa Pelegi,#1:19 Pelegi maana yake Mgawanyiko. kwa kuwa wakati wake dunia iligawanyika; nduguye aliitwa Yoktani.
20Wana wa Yoktani walikuwa:
Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera, 21Hadoramu, Uzali, Dikla, 22Obali, Abimaeli, Sheba, 23Ofiri, Havila na Yobabu. Wote hawa walikuwa wana wa Yoktani.
24 # Mwa 10:21-29; Lk 3:34-36 Wana wa Shemu walikuwa Arfaksadi, Shela,
25 # Mwa 11:15; Hes 24:24; Lk 3:35 Eberi, Pelegi, Reu,
26Serugi, Nahori, Tera,
27 # Mwa 17:5; 2Nya 20:7; Isa 41:8; 51:2; Rum 4:16 Tera akamzaa Abramu (yaani, Ibrahimu).
Jamaa Ya Ibrahimu
28 # Mwa 21:2-3; 16:11, 15 Ibrahimu alikuwa na wana wawili:
Isaka na Ishmaeli.
Wazao Wa Hagari
(Mwanzo 25:12-16)
29 # Mwa 25:13-26 Hawa ndio waliokuwa wazao wa Hagari:
Nebayothi mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli, Kedari, Adbeeli, Mibsamu, 30Mishma, Duma, Masa, Hadadi, Tema, 31Yeturi, Nafishi na Kedema. Hao ndio wana wa Ishmaeli.
Wazao Wa Ketura
32 # Mwa 22:24; 10:7 Wana waliozaliwa na Ketura suria wa Ibrahimu walikuwa:
Zimrani, Yokshani, Medani, Midiani, Ishbaki na Shua.
Wana wa Yokshani walikuwa:
Sheba na Dedani.
33Wana wa Midiani walikuwa:
Efa, Eferi, Hanoki, Abida na Eldaa.
Wote hao walikuwa wa uzao wa Ketura.
Wazao Wa Sara
34 # Lk 3:34; Mwa 21:2-3; Mdo 7:8; Mwa 18:5; 25:25-26 Ibrahimu alikuwa baba wa Isaka.
Wana wa Isaka walikuwa:
Esau na Israeli.
Wana Wa Esau
(Mwanzo 36:1-19)
35 # Mwa 36:19; 36:4; Kum 2:22; Rum 9:13; Ebr 12:16; Mal 1:2-3 Wana wa Esau walikuwa:
Elifazi, Reueli, Yeushi, Yalamu na Kora.
36 # Kut 17:14; Mwa 36:11 Wana wa Elifazi walikuwa:
Temani, Omari, Sefo, Gatamu na Kenazi;
Elifazi kwa Timna akamzaa Amaleki.
37 # Mwa 36:17 Wana wa Reueli walikuwa:
Nahathi, Zera, Shama na Miza.
Watu Wa Seiri Waliokuwa Edomu
(Mwanzo 36:20-30)
38 # Mwa 36:20 Wana wa Seiri walikuwa:
Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana, Dishoni, Eseri na Dishani.
39 # Mwa 36:22 Wana wa Lotani walikuwa wawili:
Hori na Homamu. Lotani alikuwa na dada yake aliyeitwa Timna.
40 # Mwa 36:2 Wana wa Shobali walikuwa:
Alvani,#1:40 Maandishi ya Kiebrania yanamwita Alian. Manahathi, Ebali, Shefo na Onamu.
Wana wa Sibeoni walikuwa:
Aiya na Ana.
41 # Mwa 36:25-26 Mwana wa Ana alikuwa:
Dishoni.
Nao wana wa Dishoni walikuwa:
Hemdani, Eshbani, Ithrani na Kerani.
42Wana wa Eseri walikuwa:
Bilhani, Zaavani na Akani.
Wana wa Dishani walikuwa:
Usi na Arani.
Watawala Wa Edomu
(Mwanzo 36:31-43)
43 # Mwa 36:31; 49:10 Hawa ndio wafalme waliotawala Edomu kabla hajatawala mfalme yeyote wa Waisraeli:
Bela mwana wa Beori, ambaye mji wake ni Dinhaba.
44Bela alipofariki, Yobabu mwana wa Zera kutoka Bosra akawa mfalme baada yake.
45 # Mwa 36:11 Yobabu alipofariki, Hushamu kutoka nchi ya Watemani akawa mfalme baada yake.
46 # 1Fal 11:14 Hushamu alipofariki, Hadadi mwana wa Bedadi, aliyeshinda Midiani katika nchi ya Moabu, akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Avithi.
47Hadadi alipofariki, Samla kutoka Masreka akawa mfalme baada yake.
48 # Mwa 36:37 Samla alipofariki, Shauli kutoka Rehobothi ng’ambo ya Mto Frati, akawa mfalme baada yake.
49Shauli alipofariki, Baal-Hanani mwana wa Akbori akawa mfalme baada yake.
50 # Mwa 36:39 Baal-Hanani alipofariki, Hadadi akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Pau, na mkewe aliitwa Mehetabeli binti Matredi, binti Me-Zahabu. 51#Mwa 36:40; Kut 15:15Naye Hadadi pia akafa.
Wakuu wa Edomu walikuwa:
Timna, Alva, Yethethi, 52Oholibama, Ela, Pinoni, 53Kenazi, Temani, Mibsari, 54Magdieli na Iramu. Hao ndio wakuu wa makabila ya Edomu.

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu