1 Nyakati Utangulizi
NMM

1 Nyakati Utangulizi

Utangulizi
Vitabu vya 1 na 2 Mambo ya Nyakati vinajumuishwa katika Bibilia ya Kiebrania na vimeandikwa kutoka kwa mtazamo wa kikuhani. Kwa njia hii vinajaliza vitabu vya 1 na 2 Wafalme ambavyo viliandikwa kutoka kwa mtazamo wa kinabii. 1 Mambo ya Nyakati inaanza kwa kutoa mfululizo wa orodha zinazopeana historia ya jamii ya Mfalme Daudi na uzao wa Lawi kuhani. Hii inafuatwa na kifo cha Sauli na utawala wa Daudi, huku hali ya kidini kitaifa ikitiliwa mkazo kwa njia spesheli. Kitabu hiki kinafikia kikomo kwa Sulemani kufanywa mfalme.
Wazo Kuu
Kwa kuwa 1 Mambo ya Nyakati iliandikwa kwa mtazamo wa kikuhani, mambo mengi yanayohusu dini ya Kiyahudi yametolewa ili kuongezea historia inayopatikana katika vitabu vya Wafalme. Mkazo ni kuhusu umuhimu mkuu wa ibada kwa Mwenyezi Mungu na matokeo yake mema katika maisha ya taifa. Mwenyezi Mungu hubariki mataifa yanayoweka tumaini lao kwake.
Mwandishi
Hajulikani.
Tarehe
Karne ya 5 K.K.
Mgawanyo
• Orodha ya vizazi (1:1–9:44)
• Kifo cha Sauli (10:1-14)
• Utawala wa Daudi (11:1–23:23)
• Hekalu na Walawi (23:24–27:34)
• Miaka ya mwisho ya Daudi (28:1–29:30)

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu