1
Neno La Uzima
1 #
Yn 1:2; 2Pet 1:16; Yn 20:27 Tunawajulisha lile lililokuwepo tangu mwanzo, lile tulilosikia, ambalo tumeliona kwa macho yetu, ambalo tumelitazama na kuligusa kwa mikono yetu, kuhusu Neno la uzima. 2#Yn 14:6; 1Pet 1:20Uzima huo ulidhihirishwa; nasi tumeuona na kuushuhudia, nasi twawatangazia uzima wa milele, ambao ulikuwa pamoja na Baba, nao ukadhihirishwa kwetu. 3#1Kor 1:9; 1Yn 1:1; Mdo 4:20; Yn 17:21; 1Yn 2:24Twawatangazia lile tuliloliona na kulisikia, ili nanyi mwe na ushirika nasi. Na ushirika wetu hasa ni pamoja na Baba na Mwanawe, Isa Al-Masihi. 4Tunaandika mambo haya ili furaha yetu ipate kuwa timilifu.
Kutembea Nuruni
5 #
1Yn 3:11; 2Yn 12 Huu ndio ujumbe tuliosikia kutoka kwake na kuwatangazia ninyi: kwamba Mungu ni nuru na ndani yake hamna giza lolote. 6#Efe 5:8; 1Yn 4:20Kama tukisema kwamba twashirikiana naye huku tukienenda gizani, twasema uongo, wala hatutendi lililo kweli. 7#Ufu 7:14; Ebr 9:14; Ufu 1:5Lakini tukienenda nuruni, kama yeye alivyo nuruni, twashirikiana sisi kwa sisi na damu yake Isa, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote.
8 #
Yer 2:35; Yn 8:44 Kama tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe wala kweli haimo ndani yetu. 9#Mit 28; 13; Za 32:5; 51:2; Mit 28:13; 1Yn 1:7; Mik 7:18-20; Ebr 10:22Kama tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki, atatusamehe dhambi zetu na kutusafisha kutoka kwenye udhalimu wote. 10#1Yn 5:10; Yn 5:38; 1Yn 1:8; 5:10; Yn 5:38; 2:15Kama tukisema hatukutenda dhambi, twamfanya yeye kuwa mwongo na neno lake halimo ndani yetu.