3
1 #
Yn 3:16; 15:21 Tazameni ni pendo kuu namna gani alilotupa Baba, kwamba sisi tuitwe wana wa Mungu! Na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye. 2#Rum 8:29; 2Pet 1:4; Za 17:15Wapendwa, sasa tu wana wa Mungu, lakini bado haijadhihirika tutakavyokuwa, lakini twajua ya kwamba yeye atakapodhihirishwa, tutafanana naye, kwa maana tutamwona kama alivyo. 3#2Kor 7:1; 2Pet 3:13, 14Kila mmoja mwenye matumaini haya ndani yake hujitakasa, kama vile yeye alivyo mtakatifu.
4 #
1Yn 5:17; Mt 7:23; Rum 4:15 Kila mtu atendaye dhambi afanya uasi, kwa kuwa dhambi ni uasi. 5#2Kor 5:21; 1Yn 1:2; Isa 53:5, 6, 11; 1Tim 1:15; Ebr 1:3; 9:26; 1Pet 2:24Lakini mwajua ya kuwa yeye alidhihirishwa ili aziondoe dhambi, wala ndani yake hamna dhambi. 6#1Yn 5:18; 3Yn 1:1; 1Yn 2:4Kila mtu akaaye ndani yake hatendi dhambi. Kila mtu atendaye dhambi hakumwona yeye wala hakumtambua.
7 #
1Yn 2:1; 1Yn 2:26; 1Yn 2:29 Watoto wapendwa, mtu yeyote asiwadanganye. Kila mtu atendaye haki ana haki, kama yeye alivyo na haki. 8#Yn 1:13; Za 119:3; 1Pet 1:23Yeye atendaye dhambi ni wa ibilisi, kwa sababu ibilisi amekuwa akitenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili aziangamize kazi za ibilisi. 9#Yn 1:13; 1Yn 3:6; Za 119:3; 1Yn 5:18; 1Pet 1:23Yeyote aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wa Mungu wakaa ndani yake, wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa na Mungu. 10#1Yn 3:1, 2; Yn 1:12; 1Yn 3:8; 1Yn 4:8; 1Yn 2:9Kwa jinsi hii tunaweza kujua dhahiri watoto wa Mungu na pia watoto wa ibilisi. Yeyote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.
Mpendane Ninyi Kwa Ninyi
11 #
1Yn 1:5; Yn 15:12 Hili ndilo neno mlilolisikia tangu mwanzo: Kwamba imetupasa tupendane sisi kwa sisi. 12#Mwa 4:8; Mt 5:37; Za 38:20; Mit 29:10Msiwe kama Kaini aliyekuwa wa yule mwovu akamuua ndugu yake. Basi kwa nini alimuua? Ni kwa sababu matendo yake Kaini yalikuwa mabaya na ya ndugu yake yalikuwa ya haki. 13#Yn 15:18, 19; Yn 17:14Ndugu zangu, ninyi msistaajabu kama ulimwengu ukiwachukia. 14#Yn 5:24; 1Yn 2:9Sisi tunajua ya kwamba tumepita mautini kuingia uzimani, kwa sababu tunawapenda ndugu. Kila asiyempenda ndugu yake akaa mautini. 15#Mt 5:21, 22; Gal 5:20, 21; Yn 3:16Yeyote amchukiaye ndugu yake ni muuaji, nanyi mwajua ya kwamba muuaji hana uzima wa milele ndani yake.
16 #
Yn 10:11; 15:13; Flp 2:17; 1The 2:8 Kwa namna hii twaweza kulijua pendo la Mungu: Kwa sababu Isa Al-Masihi aliutoa uhai wake kwa ajili yetu. Nasi imetupasa kuutoa uhai kwa ajili ya hao ndugu. 17#Yak 2:15, 16; 1Yn 4:20Ikiwa mtu anavyo vitu vya ulimwengu huu na akamwona ndugu yake ni mhitaji lakini asimhurumie, upendo wa Mungu wakaaje ndani ya mtu huyo? 18#1Yn 2:1; Eze 33:1; Rum 12:9Watoto wapendwa, tusipende kwa maneno au kwa ulimi bali kwa tendo na kweli. 19#Yn 18:37; 1Yn 1:8Basi hivi ndivyo tutakavyoweza kujua ya kuwa sisi tu wa kweli na hivyo twaithibitisha mioyo yetu mbele za Mungu 20#1Kor 4:4kila mara mioyo yetu inapotuhukumu. Kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mioyo yetu, naye anajua kila kitu.
21 #
Efe 3:12; 1Kor 10:14; 1Yn 5:14 Wapendwa, kama mioyo yetu haituhukumu, tunao ujasiri mbele za Mungu, 22#Mt 7:7; Ebr 13:21lolote tuombalo, twalipokea kutoka kwake, kwa sababu tumezitii amri zake na kutenda yale yanayompendeza. 23#Yn 6:23; Yn 13:34Hii ndiyo amri yake: kwamba tuliamini Jina la Mwanawe, Isa Al-Masihi, na kupendana sisi kwa sisi kama yeye alivyotuamuru. 24#1Yn 4:15; 1The 4:8Wale wote wanaozishika amri zake hukaa ndani yake na yeye ndani yao. Hivi ndivyo tunavyojua kwamba anakaa ndani yetu. Nasi twajua hili kwa njia ya Roho yule aliyetupa.