1 Yohana Utangulizi
NMM

1 Yohana Utangulizi

Utangulizi
Waraka huu wa kibinafsi sana uliandikwa na Mtume Yohana akiwa mzee kwa waumini aliowapenda sana. Anawaita watoto wake wadogo, na kuwapa mawaidha ya jinsi ya kuishi maisha yanayofaa ya Kikristo. Anaanza kwa kutilia mkazo kuhusu uhakika wa kuzaliwa kwa Isa kama mwanadamu, na anaendelea kujenga amri juu ya ukweli kwamba wale wanaomfahamu Isa wanamfahamu Baba pia. Wale ambao hawamjui Isa hawamjui Baba, wala hawajui upendo wake Baba. Kwa upande mwingine, Wakristo wamejua upendo wa Mwenyezi Mungu maishani mwao, kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni upendo, nao hawana haja ya kuogopa lolote maishani haya wala yale yajayo.
Wazo Kuu
Katika waraka huu, Yohana anasisitiza kweli za kimsingi za imani ya Kikristo ili kuwatuliza na kuwatia moyo watoto wake katika imani. Mada za upendo, msamaha, ushirika, ushindi dhidi ya dhambi, hakikisho, usafi, na uzima wa milele zimeunganishwa kwa njia ya kipekee katika barua inayoangaza na mwanga wa Mwenyezi Mungu katika giza ya ulimwengu huu.
Mwandishi
Mtume Yohana.
Mahali
Hapajulikani, pengine ni Efeso.
Tarehe
Kati ya 85-96 B.K.
Mgawanyo
• Ushirikiano wa muumini na Mwenyezi Mungu (1:1-10)
• Amri mpya ya upendo (2:1-17)
• Maonyo dhidi ya anayempinga Al-Masihi, na dhidi ya uovu (2:18-29)
• Tabia za Kikristo (3:1-24)
• Walimu wa uongo (4:1-6)
• Upendo wa Mwenyezi Mungu (4:7-21)
• Ushindi wa imani (5:1-21).

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu