1
Sulemani Aomba Hekima
(1 Wafalme 3:1-15)
1 #
1Fal 2:26; 2Nya 12:1; Mwa 39:2; Hes 14:43; 1Nya 29:25; Mwa 21:22; 1Nya 17:8; Mt 28:20 Sulemani mwana wa Daudi alijiimarisha kwenye milango yote! Katika ufalme wake, kwa kuwa Bwana Mwenyezi Mungu wake alikuwa pamoja naye, naye akamfanya mkuu mno.
2 #
1Nya 28:1; 2Nya 29:20; 2Nya 30:2 Ndipo Sulemani akasema na Israeli wote, majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia, waamuzi na viongozi wote katika Israeli, pamoja na wakuu wa jamaa. 3#Law 17:4; Kut 36:8; 40:18; 1Fal 3:4Naye Sulemani na kusanyiko lote wakakwea mpaka mahali pa juu pa kuabudia huko Gibeoni, kwa kuwa huko ndiko Hema la Kukutania la Mungu lilipokuwa, ambalo Musa mtumishi wa Bwana alikuwa amelitengeneza huko jangwani. 4#2Sam 6:2, 17; 1Nya 15:25Basi Daudi alikuwa amelipandisha Sanduku la Mungu kutoka Kiriath-Yearimu mpaka mahali alipokuwa amepatengeneza kwa ajili yake, kwa sababu alikuwa amesimamisha hema kwa ajili ya hilo Sanduku huko Yerusalemu. 5#Kut 38:2; 31:2; 1Nya 13:3Lakini yale madhabahu ya shaba ambayo Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, alikuwa ametengeneza yalikuwa huko Gibeoni mbele ya Maskani ya Bwana Mwenyezi Mungu, hivyo Sulemani na kusanyiko lote walimtafuta Mungu huko. 6#1Fal 3:4Sulemani akapanda huko yalikokuwa madhabahu ya shaba mbele za Bwana katika Hema la Kukutania, na kutoa dhabihu 1,000 za sadaka za kuteketezwa juu yake.
7 #
2Nya 7:12; Isa 58:9; 1Fal 3:5; Mit 3:5 Usiku ule Mungu akamtokea Sulemani na kumwambia, “Omba lolote utakalo nikupe.”
8 #
1Nya 23:1; 28:5 Sulemani akamjibu Mungu, “Umemwonyesha baba yangu Daudi fadhili nyingi, nawe umeniweka niwe mfalme mahali pake. 9#2Sam 7:25; 1Fal 8:25; Mwa 12:2Sasa, Bwana Mwenyezi Mungu, ahadi yako kwa baba yangu Daudi na ithibitike, kwa kuwa umenifanya mimi mfalme juu ya watu ambao ni wengi kama mavumbi ya nchi. 10#Hes 27:17; Mit 8:15-16; Kum 31:2; 1Fal 3:9; Za 119:34; Mit 3:13; Yak 1:5Nakuomba unipe mimi hekima na maarifa, ili niweze kuongoza watu hawa, kwa kuwa ni nani awezaye kutawala hawa watu wako walio wengi hivi?”
11 #
Kum 17:17; 1Sam 16:7; 1Fal 3:11; 8:18 Mungu akamwambia Sulemani, “Kwa kuwa jambo hili ndilo shauku ya moyo wako na hukuomba mali, utajiri au heshima, wala kifo kwa ajili ya adui zako, nawe kwa kuwa hukuomba maisha marefu, bali umeomba hekima na maarifa ili kuongoza watu wangu ambao nimekufanya uwe mfalme juu yao, 12#1Nya 29:12-25; Neh 13:26; Efe 3:20; 2Nya 9:22; Za 34:9-10; Mt 6:33; Mhu 2:9kwa hiyo utapewa hekima na maarifa. Tena nitakupa pia mali, utajiri na heshima, ambavyo hakuna mfalme yeyote aliyekuwepo kabla yako amewahi kuwa navyo, na hakuna yeyote baada yako atakayekuwa navyo.”
Fahari Ya Sulemani
(1 Wafalme 10:26-29)
13Ndipo Sulemani akaenda mpaka Yerusalemu kutoka mahali pa juu pa kuabudia huko Gibeoni, kutoka mbele ya Hema la Kukutania. Naye akatawala Israeli.
14 #
1Sam 8:11; 1Fal 9:19; 4:26 Sulemani akakusanya magari ya vita na farasi. Alikuwa na magari 1,400 na farasi 12,000, ambayo aliyaweka katika miji ya magari na mengine akawa nayo huko Yerusalemu. 15#1Fal 9:28; Isa 60:5; Ay 22:24; 1Fal 10:27Mfalme akafanya fedha na dhahabu kuwa vitu vya kawaida kama mawe huko Yerusalemu, mierezi akaifanya kuwa mingi kama mikuyu vilimani. 16Farasi wa Sulemani waliletwa kutoka Misri na kutoka Kue.#1:16 Yaani Kilikia. Wafanyabiashara wa mfalme waliwanunua kutoka Kue. 17#Wim 1:9Waliagiza magari kutoka Misri kwa bei ya shekeli 600#1:17 Shekeli 600 za fedha ni sawa na kilo 7. za fedha, na farasi kwa shekeli 150.#1:17 Shekeli 150 ni sawa na kilo 1.7. Pia waliwauza nje kwa wafalme wote wa Wahiti na wa Waaramu.