11
Paulo Na Mitume Wa Uongo
1 #
Mt 17:17; 2Kor 5:13 Laiti mngenivumilia kidogo katika upumbavu wangu! Naam, nivumilieni kidogo. 2#Hos 2:19; Efe 5:26-27Ninawaonea wivu, wivu wa Kimungu, kwa kuwa mimi niliwaposea mume mmoja, ili niwalete kwa Al-Masihi kama mabikira safi. 3#Mwa 3:1-6; 1Tim 2:14; Ufu 12:5Lakini nina hofu kuwa, kama vile Hawa alivyodanganywa kwa ujanja wa yule nyoka, mawazo yenu yasije yakapotoshwa, mkauacha unyofu na usafi wa upendo wenu kwa Al-Masihi. 4#1Kor 3:11; Rum 8:15; Gal 1:6-9Kwa sababu kama mtu akija na kuwahubiria Isa mwingine ambaye si yule tuliyemhubiri, au kama mkipokea roho mwingine ambaye si yule mliyempokea, au Injili tofauti na ile mliyoikubali, ninyi mnaitii kwa urahisi. 5#2Kor 12:11; Gal 2:6Lakini sidhani ya kuwa mimi ni dhalili sana kuliko hao “mitume wakuu.” 6#1Kor 1:17; 2Kor 9:7; Efe 3:4Inawezekana mimi nikawa si mnenaji hodari, lakini ni hodari katika elimu. Jambo hili tumelifanya liwe dhahiri kwenu kwa njia zote.
7 #
2Kor 12:13; Rum 1:1; 1Kor 9:18 Je, nilitenda dhambi kwa kujishusha ili kuwainua ninyi kwa kuwahubiria Injili ya Mungu pasipo malipo? 8#Flp 4:15-18Niliyanyang’anya makanisa mengine kwa kupokea misaada kutoka kwao ili niweze kuwahudumia ninyi. 9#Flp 4:15; 2Kor 12:13-16Nami nilipokuwa pamoja nanyi, nikipungukiwa na chochote, sikuwa mzigo kwa mtu yeyote, kwa maana ndugu waliotoka Makedonia walinipatia mahitaji yangu. Kwa hiyo nilijizuia kuwa mzigo kwenu kwa njia yoyote, nami nitaendelea kujizuia. 10#Rum 9:1; Mdo 18:12; 1Kor 9:15Kwa hakika kama vile kweli ya Al-Masihi ilivyo ndani yangu, hakuna mtu yeyote katika Akaya nzima atakayenizuia kujivunia jambo hili. 11#Rum 1:9; 2Kor 12:15Kwa nini? Je, ni kwa sababu siwapendi? Mungu anajua ya kuwa nawapenda! 12#2Kor 9:12Nami nitaendelea kufanya lile ninalofanya sasa ili nisiwape nafasi wale ambao wanatafuta nafasi ya kuhesabiwa kuwa sawa na sisi katika mambo wanayojisifia.
13 #
Mt 7:15; Tit 1:10; Ufu 2:2 Watu kama hao ni mitume wa uongo, ni wafanyakazi wadanganyifu, wanaojigeuza waonekane kama mitume wa Al-Masihi. 14#Mt 4:10Wala hii si ajabu, kwa kuwa hata Shetani mwenyewe hujigeuza aonekane kama malaika wa nuru. 15#Mt 16:27; Flp 3:19Kwa hiyo basi si ajabu, kama watumishi wa Shetani nao hujigeuza ili waonekane kama watumishi wa haki. Mwisho wao utakuwa sawa na matendo yao yanavyostahili.
Paulo Anajivunia Mateso Yake
16 #
2Kor 11:1; 2Kor 12:6, 11 Nasema tena, mtu yeyote asidhani kwamba mimi ni mjinga. Lakini hata kama mkinidhania hivyo, basi nipokeeni kama mjinga ili nipate kujisifu kidogo. 17#1Kor 7:12, 25; 2Kor 11:21; 1Kor 7:6Ninayosema kuhusiana na huku kujisifu kwa kujiamini, sisemi kama vile ambavyo Bwana angesema, bali kama mjinga. 18#2Kor 5:16; 2Kor 10:4; Flp 3:3-4Kwa kuwa wengi wanajisifu kama vile ulimwengu ufanyavyo, mimi nami nitajisifu. 19#1Kor 4:10; 2Kor 11:1Ninyi mwachukuliana na wajinga kwa sababu mna hekima sana! 20#2Kor 11:1Kweli ni kwamba mnachukuliana na mtu akiwatia utumwani au akiwatumia kwa ajili ya kupata faida au akiwanyang’anya au akijitukuza mwenyewe au akiwadanganya. 21#2Kor 10:1; Flp 3:4Kwa aibu inanipasa niseme kwamba sisi tulikuwa dhaifu sana kwa jambo hilo!
Lakini chochote ambacho mtu mwingine yeyote angethubutu kujisifia, nanena kama mjinga, nami nathubutu kujisifu juu ya hilo. 22#Flp 3:5; Rum 9:4; 11:1; Lk 3:8Je, wao ni Waebrania? Mimi pia ni Mwebrania. Je, wao ni Waisraeli? Mimi pia ni Mwisraeli. Je, wao ni wazao wa Ibrahimu? Mimi pia ni mzao wa Ibrahimu. 23#1Kor 3:5; 1Kor 15:10; Mdo 16:23; 2Kor 6:4-5; Rum 8:36Je, wao ni watumishi wa Al-Masihi? (Nanena kiwazimu.) Mimi ni zaidi yao. Nimefanya kazi kwa bidii kuwaliko wao, nimefungwa gerezani mara kwa mara, nimechapwa mijeledi sana, na nimekabiliwa na mauti mara nyingi. 24#Kum 25:3Mara tano nimechapwa na Wayahudi viboko arobaini kasoro kimoja. 25#Mdo 16:22; Mdo 14:19; Mdo 27:1-44Mara tatu nilichapwa kwa fimbo, mara moja nilipigwa kwa mawe, mara tatu nimevunjikiwa na meli, nimekaa kilindini usiku kucha na mchana kutwa, 26#Mdo 20:3; Mdo 21:31; Gal 2:4katika safari za mara kwa mara. Nimekabiliwa na hatari za kwenye mito, hatari za wanyang’anyi, hatari kutoka kwa watu wangu mwenyewe, hatari kutoka kwa watu wa Mataifa; hatari mijini, hatari nyikani, hatari baharini; na hatari kutoka kwa ndugu wa uongo. 27#Mdo 18:3; Kol 1:29; 1Kor 4:11-12; 2Kor 6:5Nimekuwa katika kazi ngumu na taabu, katika kukesha mara nyingi; ninajua kukaa njaa na kuona kiu; nimefunga kula chakula mara nyingi; nimehisi baridi na kuwa uchi. 28#1Kor 7:17Zaidi ya hayo yote, nakabiliwa na mzigo wa wajibu wangu kwa makanisa yote. 29#Rum 14:1; 1Kor 2:3; Mt 5:29Je, ni nani aliye mdhaifu, nami nisijisikie mdhaifu? Je, nani aliyekwazwa, nami nisiudhike?
30 #
Gal 6:14; 2Kor 12:5-9; 1Kor 2:3 Kama ni lazima nijisifu, basi nitajisifia yale mambo yanayoonyesha udhaifu wangu. 31#Rum 1:25; Rum 9:5Mungu na Baba wa Bwana Isa, yeye ambaye anahimidiwa milele, anajua ya kuwa mimi sisemi uongo. 32#Mdo 9:24; Mdo 9:25Huko Dameski, mtawala aliyekuwa chini ya Mfalme Areta aliulinda mji wa Dameski ili kunikamata. 33Lakini nilishushwa kwa kapu kubwa kupitia katika dirisha ukutani, nikatoroka kutoka mikononi mwake.